Nakaribia kubaki skeleton, nifanyeje kurudisha mwili wangu?

Nakaribia kubaki skeleton, nifanyeje kurudisha mwili wangu?

Simple tu punguza ngono. Vijana wengi wa kiume hawajua kuwa kugongana sana kunakausha ....

Punguza ngono alaf relax, mambo yenyewe yataenda....
[emoji23][emoji23][emoji23]Asante mkuu japo sipo addicted sana kwenye hivyo vitu
 
Kula vyakula vya wanga kwa wingi

Kula vyakula vya sukari kwa wingi

Punguza mazoezi

Usilale sana, kupumzika vya kutosha kunasababisha weight kupungua (Kuna watakaoguna hapa)
Kuna mmoja alinambia na kuoga kila siku kuna punguza uzito. Je hili nalo lipoje naomba ufafanuzi wako Tafadhari
 
Embu kula mbuzi katoliki na ndizi 3 (ya kuchoma iko poa zaidi) na bia deile, then after 2 month ukuje hapa
Mbona bia situmii kiongozi, hakuna mbadala wowote naweza tumia zaidi ya gambe?
 
Kuna mmoja alinambia na kuoga kila siku kuna punguza uzito. Je hili nalo lipoje naomba ufafanuzi wako Tafadhari
Hamna mahusiano kaka

Kuna makabila primitive Tanzania, wanaishi maporini, sitataja majina wengi wao hususani vijana ni wembamba na hao kuoga kwao ni hiari

Wewe komaa na ushauri huo hapo juu

Japo, watu wengi wanataka kupungua mwili kwako naona ipo kinyume
 
Hamna mahusiano kaka

Kuna makabila primitive Tanzania, wanaishi maporini, sitataja majina wengi wao hususani vijana ni wembamba na hao kuoga kwao ni hiari

Wewe komaa na ushauri huo hapo juu

Japo, watu wengi wanataka kupungua mwili kwako naona ipo kinyume
Ooh! Nimekupata kaka! Shukrani
 
Unataka kuwa kama mimi?
b0dffac8a1bdd82932a50c47b7d30e6e.jpg
Duuuh! [emoji4][emoji4]Hiyo level yako sina hakika kama nitaifikia
 
Hamna mahusiano kaka

Kuna makabila primitive Tanzania, wanaishi maporini, sitataja majina wengi wao hususani vijana ni wembamba na hao kuoga kwao ni hiari

Wewe komaa na ushauri huo hapo juu

Japo, watu wengi wanataka kupungua mwili kwako naona ipo kinyume
Watu tunatofautiana sana. Wengine tumejaribu kupunguza miili hadi tumekata tamaa imeshindikana wengine wanataka kuongezeka
 
Hujaandika umepungua uzito kwa kiasi gani ( umelose kg ngapi?)
Ila yote kwa yote, nenda hospitali nzuri tu ukachekiwe.
 
Mbona bia situmii kiongozi, hakuna mbadala wowote naweza tumia zaidi ya gambe?
Mkuu kwanza pole kwa changamoto hio. Kuna dawa moja ni nzuri sana kwa kuleta hamu ya chakula. Sijajua upo mkoa gani maana ni adimu kidogo kuipata hasa mikoani. Hii dawa inaitwa APETAMIN SYRUP. Bei yake imesimama. Kwa Dar es Salaam niliinunua 60,000.
 

Attachments

  • images.jpeg
    images.jpeg
    22.7 KB · Views: 24
Usiforce sana kunenepa kiongozi elewa tu kwamba kila kitu kinakuja kwa wakati baada ya kupitia mambo ya fulani! Kikubwa tu kwa sasa wewe kuwa na amani ya moyo na uridhike na ulichonacho. My brother alikuwa mwembamba sana pesa ya kula na kufanya chochote kile kizuri alikuwa nayo lakini hakuwahi kunenepa mpaka alikata tamaa ila baada ya kuoa na kuingia kwenye ndoa sasahv amekuwa sio mwenzetu tena kanenepa na ka kitambi kametokea!! Hata mimi natarajia nije ninenepe one day niwe na mwili fulani wa kishua kwa sasa nimeshindwa maana napitia changamoto nyingi!!!!!
 
Siku ukiacha kutojali kuhusu wembamba wako na kuacha kabisa kujihangaisha ili unenepe basi ndio hapo utaanza kunenepa.
 
Hello JF salaam!

Nimekuja kwenu nipate mawili matatu huenda nikawa na tatizo. Nilikuwa na mwili wa wastani siyo bonge sana wala mwembamba sana.Kimbembe kimeanza kama miaka miwili nyuma naona mwili wangu unazidi kupromoka tu siku hadi siku japo chakula napata na pia naupa mwili muda mwingi wa kupumzika hasa nyakati za usiku.

Mwanzoni nilihisi labda ni kwa sababu ya misongo ya mawazo ndipo nikaamua kujijengea desturi ya kuepuka mambo yanayoweza kunisababishia hizo stress kwa kujumuika na marafiki zangu wa karibu, kufanya mazoezi ya mwili na viungo na pia kufanya mambo ambayo yanaupa moyo wangu furaha(hobbies). Nimefanya hivyo yapata miezi saba mpaka sasa lakini hola tu sioni changes na mwili ndo hivyo unazidi kuyoyoma tu.

Infact, sipendi kuwa bonge nataka niendelee kumaintain mwili niliokuwa nao lakini kwa dalili hizi za karibia kila ninaekutana nae ananiuliza mbona umepungua hivyo nahisi ni dhahiri shairi nimepunguwa kwa kiasi kikubwa. Hii hali kwakweli inanitisha imefikia mahala umenifanya nianze kuonekana mdogo hata kwa niliowazidi umri hata pale napoongozana na dogo langu anaonekana mkubwa mi mdogo japo siyo vibaya lakini kwa upande wangu inanitafakarisha sana ukizingatia kwamba sikuwa hivyo hapo kabla.

Kiafya niko vizuri kabisa na huwa nina desturi ya kuchukua vipimo kila baada ya muda fulani na mpaka naandika uzi huu nilianza kwenda kucheki afya kwanza kabla ya kuja kwenu kuwaomba mawili matatu. By the way, nisiwe more talkative kiasi cha kuwakera naomba kusikia toka kwenu ni kwa namna gani naweza kurudisha mwili wangu(mwili wa wastani) kutoka kwenye huu nilio nao kwa sasa?? Na pengine ni kipi hasa kinaweza kuwa kimechangia mwili wangu kupungua kama nilivyoeleza huko juu??

Karibuni niko tayari kupokea ushauri wenu na kufanyia kazi.
Usiamini kitambi ni afya!!!
 
Back
Top Bottom