Nakaribisha maswali kuhusu Tiba / Dawa

Niliwahi kukuuliza dawa ya sunzua au wart kwa umombo lakini ulipotezea, haya na leo naomba majibu. Please
 
Hello,
  1. Nakushauri utumie Clindamycin(dalacin liniment) au benzoylperoxide au combination ya benzoylperoxide+ adapelen kupaka usoni!
  2. Nawa uso mara mbili kwa siku tumia sabuni yenye pH ya 6,5 kunawaia na water based facial cream kupaka usoni,Ukitumia ointment yenye mafuta mengi au mfano mafuta ya mgando inaworsen chunusi.
  3. Epuka kutumbua hizo chunusi au kuzigusa gusa
  4. Epuka kula vyakula vyenye viungo vingi,sukari nyingi na mafuta mengi
 

Sio lazma awe amepata mlo,muda wowote tu na hali hii ilianza kumtokea akiwa mdogo (13years)


Maumivu yapo chini ya kitovu(yaani kati ya kitovu na ilipo jinsia-nadhani umenielewa vizuri)


Hasumbuliwi na gas tumboni.

Hicho kipimo hajawahi kufanyiwa.
 
Ndugu zangu,kwa wale wenye chunusi za muda mrefu au matatizo ya ngozi na dokta wetu (Mungu ambariki saaaana)akamshauri atumie Clindamycin(Dalacin) basi usipoteze muda!fasta nenda kanunue hiyo dawa....binafsi nilipata machunusi kibao+ mba sugu+ nikawa na rangi mbili mbili usoni.....nikaenda Idara ya ngozi- KCMC wakaniandikia hiyo dawa!! Yaani ndani ya mwezi 1 tu nimerudia ngozi yangu ya utotoni,kiukweli nimependeza ( japo natakiwa niendelee kuitumia kwa miez mingine minne)

GHARAMA:-
Licha ya hii dawa kuwa nzuri saaaana,ila jipange.. Ni dawa ghari kiukweli.

Binafsi inanicost kama 120,000/=@mwezi.

NB:- Hakikisha umeangalia tarehe ya kutengenezwa na ku-expire maana siku kila kitu kinafanywa kisanii sanii.

Byeeee
 
Dr.mimi nasumbuliwa na fangasi sehemu za siri pamoja na tumbo kujaa gesi na kutopata choo kwa muda.

Nlivyofanya vipimo hospital wakaniambia nina candidemia na nikapewa fluconazole kumeza mwezi mzima.lakini naona hazijanisaidia coz tatizo lilipungua kidogo baadae hali imejirudia na kuongezeka zaidi.

Naomba unisaidie kama kuna dawa nyingine mbadala tofauti na fluconazole.Na je hii candidemia ni tofauti na systematic fungus?
 

Nashukuru sana dokta kwa msaada. Nitajitahid kutafuta hizo dawa hadi nizipate
 

Ahsante pia kwa kukazia ushauri wa dokta.

Kama unafahamu naomba unijuze; Ni hospitali gani kwa hapa Dar es salaam ni nzuri kwa magonjwa ya ngozi hususani chunusi?
 
Niliwahi kukuuliza dawa ya sunzua au wart kwa umombo lakini ulipotezea, haya na leo naomba majibu. Please
Nilishajibu swali hilo...Rudi sehem za mwanzo za uzi huu!!
 
Candidemia ndio hio systemic fungus(fungus iliyopo kwenye damu).Je umeshajaribu kutibu hio fungus locally yaani kwa kutumia creams mfano?

Kuhusu tumbo kujaa gesi na kutopata choo nimeandika kuhusu IRRITABEL BOWEL SYNDROME na kuhusu CONSTIPATION jaribu kusoma post za nyuma.
 
Dr.nashukuru sana kwa ku-respond maelezo yangu,naomba usichoke kutuhudumia.Kuhususu dawa ya kupaka nmetumia GENTRISONE cream.

Sorry,kuhusu FLUCONAZOLE kushindwa kumaliza tatizo na kama kuna dawa mbadala naona kama umesahau kunipa maelezo.Pamoja na maelezo yako mazuri uliyotupatia ktk kurasa za awali,unaweza kuongelea kuhusu kushindwa kwa FLUCONAZOLE na kama kuna dawa mbadala,plse!
 
Kuna vidonge vinaitwa maxman vya kuongeza nguvu za kiume vya kichina jamaa yangu anavitumia.naitaji juwa madhara yake kiafya
 
Ahsante pia kwa kukazia ushauri wa dokta.

Kama unafahamu naomba unijuze; Ni hospitali gani kwa hapa Dar es salaam ni nzuri kwa magonjwa ya ngozi hususani chunusi?

Daaah ndugu mimi sio dokta aisee,ila siku zote kwa hapa Tz najisikia AMANI nikitibiwa KCMC ya Moshi au SELIAN ya Arusha,

Kwa mambo ya Ngozi (ikiwemo chunusi nakushauri nenda KCMC maana wana department kabisa ya Ngozi, kuna wataalam wengi wa ngozi na wanahudumia kwa ufanisi kwakweli-unasikilizwa, unapimwa, wana madawa ambayo mengine wanatengeneza pale pale nadhani (maana hayapatikani hata kwenye maduka makubwa ya dawa).

Hivyo nakushauri nenda KCMC kama upo karibu na Moshi..

Thanks
 
Dokta pole kwa kazi nzuri,

Naomba urejee page ya 41,unisaidie kunipa jibu baada yakutoa maelezo ya ziada uliyotaka.

Thanks na kazi njema
 
Docta nasubiri majibu tafadhali

Hio maxman sio dawa ilivyo kuwa declared.Ina kiwango cha sildenafil ambacho hakijathibitishwa inaweza kuwa na madhara kwa afya yako.

Kama una hitaji tiba sahihi nakushauri uende hosp upewe prescription ya sildenafil inayotambulika au phosphodiesterase inhibitors nyingine.
 
Kuna sababu tofauti za kwann hukupata tiba mbadala!

Aidha hukula dawa ipasavyo,dozi sahihi na ulimiss dose, hukumaliza tiba yote uliishia katikati. Ukifanya hivo fungus inakuwa sugu na haitibiki!

Au inawezekana unahitaji tiba na antifungal ambayo ipo more potent. Hio fungus unayo muda gani?ulichukuliwa vipimo vya damu kabla hujaanza tiba?
 
Sio lazma awe amepata mlo,muda wowote tu na hali hii ilianza kumtokea akiwa mdogo (13years)


Maumivu yapo chini ya kitovu(yaani kati ya kitovu na ilipo jinsia-nadhani umenielewa vizuri)


Hasumbuliwi na gas tumboni.

Hicho kipimo hajawahi kufanyiwa.
Jinsi unavyonieleza ni kama ana maumivu maeneo ya kizazi,namshauri aende hospitali akafanyiwe check up.Je hali hio inatokea baada ya tendo la ndoa au inakuja wenyewe tu??
Maumivu ya chini ya kitovu yana weza kusababishwa na mambo tofauti kama
  • Ovarian cysts
  • UTI
  • Infection kwenye kibofu cha mkojo
  • Irritable bowel syndrome
  • Bacterial or viral intestinal infection
  • Colon polyps
  • Apendicitis
  • Cancer ya utumbo mpana
  • Food poisoning n.k
 
Hello Dr.

Mi nataka kufahamu haya;

1-Je Peripheral neuropathy iliyosababishwa na vitamin B deficiency inatibika kabisa mtu akarudi kwenye hali yake ya kawaida? (nazungumzia mtu aliyeko kwenye wheelchair hawezi hata kusimama)

2-Dawa zipi ni nzuri zaidi kwa mwenye hilo tatizo?

3-What's the cause of (GBS) Gorain Barre Syndrome[not sure with the spellings] na nini tiba yake?

Thanks in advance.
 
Hellow NDAGLA,
Peripheral neuropathy inayosababishwa na vitamin B deficiency inaweza kutibika ikiwahiwa mapema ili kurestore nerve damage.Mapungufu ya vitamin b12 yanasababisha damage kwenye myelin sheath inayoilinda nerves.Ni muhimu achukuliwe vipimo ili ijulikane how much damage is done so far.Tiba ni Vitamin B12 suppmelents kwa formulations tofauti.Kwa stage alofikia sina uhakika kama inaweza kusaidia but it is worth a try.
  • Milo kama nyama,samaki,mayai,n.k,
  • Vidonge vya Vitamin B12
  • Vitamin B12 intramuscular injections
Guillain-Barre syndrome ni autoimmune disease ambapo inasemekana immune system ya mwili inavamia myelin sheath ya nerve cells.Inasababisha muscle weakness,loss of reflexes,kupoteza hisia kwenye uso,miguu,mikono na hata sehem nyingine za mwili.Tiba pekee inayoweza kutumika ni intravenous immunoglobulin.
 
Last edited by a moderator:

Toka hali ilivyoanza ni miaka 3 sasa.Kabla ya kupima kuna vidonge flani (sivikumbuki jina) nlikula kwa siku kumi kwa maelezo ya Dr.nlipoona hakuna mabadiliko ndo nikarudi nikapima na kupewa hizo fluconazole lakini naona na zenyewe hazijasaidia!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…