Nakaribisha maswali kuhusu Tiba / Dawa


Me nadhani kuna haja ya kumaliza dozi na pia ukienda hospitali waambie ufanye kitu kinaitwa culture and sensitivity itasaidia kujua huyo mdudu dawa gani inamuondoa kwa asilimia zote
 
naomba kujua dawa effective ya kutoa mimba ya wiki 3-4
gharama zake na zinapatikana wapi

Wiki tatu mpaka nne misoprostol inaweza kutoa
Ila jiulize kwann utoe mkuu fikiri mara mbili mpaka tatu
 
Vidonda via tumbo dawa yake ni Nini dr please [emoji120] reply

Vidonda vya tumbo mara nyingi havitibiki ila inategemea na kisababishi chake kama ni bacteria utapewa dawa zitakazomuondoa huyo mdudu na kukupa afadhali pia kuna dawa za kupunduza acid na kadha wa kadha
Cha muhimu fuata management ulopewa na daktari wako ili vidonda visizidi kuongezeka ukubwa
 

Kafanye culture and sensitivity wanaweza jua dawa gani ni effective
Na kutokana na kua umetumia dawa nyingi za kila aina pengine wadudu wamekua sugu na dawa
And by the way anza na either flucanozole au griseofulvini wakati unaendelea kufanya hiyo test niliyokuambia
 

Kutakua na tatizo kwenye mfumo wako wa umeng’enyaji nenda hospitali kwa maelezo zaidi
 
Polen na majukum wakuu . Ninatatizo la pre-mature ejaculation & nakumbhka o-level nlikuwa mwanachama wa chaputa 6years ago sasa ni victim wa pre-ejaculation naomba msaada. Mazoez nafanya sana
 
Naomba msaada niliumia mkono kwenye maungio nikafungwa p.o.p kwa wiki 4 sasa Jana wametoa lakini mkono bado auko vizuli naomba kama kuna dawA naweza kutumia picha apo chini za X ray na mkono ulivyo sasa
 
griseofulvin nimeitumia miezi miwili but hamna mabadiliko
 
Mkuu sifahamu Culture and sensitivity ni nini....nipe maelezo zaidi
 
griseofulvin nimeitumia miezi miwili but hamna mabadiliko

Unapoitumia hakikisha unakula vyakula vyenye mafuta kwa wingi ili iweze kufanya kazi, vinginevyo utakua unaitumia kama kiburudisho tu. Kama hayo yote umezingatia na haijasaidia basi inaweza tatizo lako lisiwe fungal infection
 
Unapoitumia hakikisha unakula vyakula vyenye mafuta kwa wingi ili iweze kufanya kazi, vinginevyo utakua unaitumia kama kiburudisho tu. Kama hayo yote umezingatia na haijasaidia basi inaweza tatizo lako lisiwe fungal infection
Mkuu, Naweza kupima hii kitu? vipimo gani? Maana nimeenda kwa Dermatologist Muhimbili, haja propose kuhusu vipimo, ananipa dawa tu hizo cream
 
Mtoto wangu wa mwaka mmoja na nusu
akilia ama kwa hasira au kwa mstuko
hukakamaa na kupindua macho na kupoteza fahamu kwa muda.
Je hii ni degedege?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nikila chakula naskia kutapika. Ingawa nimeshawahi tapika mara 3 Tuu hizo nyingine najizuia na hali hii hutokea wakati wa kula tuu iwe asubuh,mchana au jioni.

Nilienda hospital nikapewa dawa za minyoo lakini hakuna mafanikio, ni mwezi wa sita sasa hii hali ipo kwangu.

Mwenye uwezo wakunisaidia nini tatizo anisaidie au kama kuna mtu aliewahi kumbana na tatizo kama hili pia anaweza akashare na mimi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ninaharisha tu maji maji bila tumbo kuuma...sasa nimetumia 'loperamide' wakati huo huo nina dose ya kifua ya Koflyn(Diphenhydramine) pamoja na amoxlyn(Antibiotics)...

Sasa naona mafua yameanza mpaka macho yanauma nikifumbua sana...na kifua ndio kama kawaida...sasa nahofia kunywa hiyo dose yangu...nikihofia REACTION itakayotokea...na diclofenac ya maumivu pia nimepewa...

Sasa ninafanyaje...maana dawa ni nyingi sana...je hakuna madhara yoyote yatakayotokea...?

NB: NI JANA NIMETOKA KITUO CHA AFYA WAMEPIMA MALERIA UTI HAKUNA SASA...WAKANAMBIA NIRUDI WACHECK LABDA NA TYPHOID...ILA KIFUA TU NDIO WAKANIANDIKIA HIZO DAWA(wakati huo kuharisha kulikuwa bado...maana kumeanza usiku huu).

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Samahan Nina tatizo najihis homa pia kichwa kinauma pia joto limepanda tatizo nn
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…