ndege JOHN
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 21,643
- 51,642
Wananchi tunafanya kazi kwa bidii na tunapenda haki lakini viongozi wetu hawaonyeshi kuwa na nia ya kututetea wametuacha katika mazingira duni hawatusaidii kuboresha hali zetu na ndio sababu miaka ya nyuma watu walikuwa wanajiunga na migomo.
Viongozi wetu (wa kisiasa na dini) wanaishi maisha ya anasa lakini bado wanatuomba chakula na pesa ilihali sisi nako tunapambana tupate mahitaji yetu ya kila siku.
Mambo ni mengi na ya ajabu yanashangaza sana. Mtu ana uwezo lakini bado anaongezewa anasa. Sio haki hata kidogo. Ni bora kama mtu ana mshahara na maisha mazuri basi hizo pesa ikafanyie Jambo lingine kusaidia masikini.
Pima mara mbili kata mara moja ili kuhakikisha lililo jema na lenye hekima kati ya Benz moja la rais mstaafu au kujenga masoko ya kisasa katika tarafa 5.