Uso wa nyoka
JF-Expert Member
- Mar 17, 2014
- 4,791
- 2,375
Habari zenu wanajf!
Nategemea msaada mkubwa sana kutoka kwenu; nikijua siwezi kupata msaada
mwingine zaidi ya hapa. Mie ni mkazi wa iringa ingawa sasa nipo
Dodoma kimasomo. Nina tatizo la koo: tatizo limedumu kama mwaka na nusu
na mara kadhaa nimejaribu kupata matibabu lakini sijafanikiwa.
kuna kipindi nimewahi kupigwa x-ray iitwayo barium swallow katika
- Koo linauma,
- kuna muda nashindwa kumeza chakula (au kinapita kwa tabu),
- mahohozi hayaishi kooni.
hospitali ya rufaa mbeya lakini Daktari alinambia hakuna tatizo lolote.
Kweli tatizo linanitesa mno. Kuna kipindi niliwahi kuongea na jamaa
yangu mmoja alinambia inawezekana ni saratani ya koo, niliogopa sana
ingawa nilipojaribu kugoogle na kuona dalili za saratani ya koo ziliona
zinaendana.
Wajameni naomba ushauri wenu katika uchunguzi wa hili tatizo ikiwezekana
hata kuja Dar kupata vipimo.
Kula mastafeli na matopetope kwa wingi. Pia saga kabeji mbichi iwe juisi unywe glasi moja mara 3 kwa siku, tumia kwa mwezi mfululizo utashangaa utakachokiona.
Epuka mafuta ya ng'ombe, chumvi na vitu vya kiwandani na upendelee kula matunda na mboga mbichi hasa nyanya.