Nakerwa na mafuta ya nywele anayotumia mke wangu

Nakerwa na mafuta ya nywele anayotumia mke wangu

MAULA

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2012
Posts
1,056
Reaction score
170
Jamani nakerwa na harufu ya madawa/mafuta anayotumia mpenzi wangu kwenye nywele zake ila ndo sina jinsi sasa maana nikimwambia anyoe nywele kichwa ndo tatizo tena.

Sasa wanaume wenzangu hili mnalivumiliaje hususani mda wa kulala usiku au nyie wamama wa humu ndani mnafanyaje kuondoa tatizo hili.

Maana hata mvae makofia yenu ya nywele yale ila bado harufu coz yanaharufu kali sana haya madawa/mafuta yenu ya nywele
.
 
swala ni harufu.
Nipe jina unayotumia
 
Mm mke wang nilimnyoa kipara tu...🙂
 
Kuna shida kubwa sana juu ya matumizi ya vipodozi na mafuta yatumikayo kutengenezea nywere za kina mama.
Moja ya shida hiyo ni kuwa kuna mafuta ambayo mwanamke akitumia na anapolala na mwenzi wake ile (shombo) harufu anapovuta umdhuru na mojawapo ni kupunguza uwezo wa kujamiana, hivo si rahisi kunielewa ila ukweli ni huo.

TATIZO LAKO.
Kuna baadhi ya chemicals za kina mama zina harufu sana (nakuunga mkono) lakini sasa kama ni mkeo inabidi muongee nyie wenyewe muelewane, laiti hatokuelewa basi ana matatizo huyo.

USHAURI:
Kuna mafuta na vifaa vya kienyeji ambavyo ukitumia vinatunza nywere na havina shombo wala madhara.

Asante.
 
Sasa si umwambie abadilishe au mtafutie yenye harufu nzuri.
 
Kwani nywele zake katengenezaje..........?........kama ni weave basi hajaosha........
 
ni harufu tu au kuna kingine???

ha ha ha wanasema kama mme/mke toka mwanzo alikuwa anakoroma usiku na unaona sawa, siku ukianza kuona hilo ni tatizo basi ujue mapenzi yameisha!!

Jamaa awe mkweli, je tatizo ni harufu tu!?
 
Back
Top Bottom