Abdul Nondo
JF-Expert Member
- Oct 28, 2016
- 520
- 2,930
Nimeona Mjadala sehemu kwamba tubadili tuite Amirat badala ya Amir, sababu amir ni kwa mwanaume na Amirat ni kwa mwanamke. Kwamba Mh. Rais, Samia Suluhu Hassan tumuite Amirati Jeshi Mkuu.
Nina kinzana na wanaotoa hoja ya kuita Amirati badala ya Amiri, mbali na hoja ya kikatiba ibara ya 33 (2) inayo mtambua Rais Kama kiongozi wa nchi, kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu, naomba nijadili suala hili kwa minajili ya kilugha tuu Kama linavyohojiwa na kujadiliwa kwa minajili ya kilugha.
Amir / Ameer ni neno la kiaribu kweli likiwa limelenga mwanaume kiongozi “leader”, Kamanda “commander”, Mtawala “ruler”, au chifu “chief”,.
Neno hili limetokana na neno la kiarabu A-M-R.(Kuamrisha au to command).
Neno hili ni la Kiarabu, ila katika lugha yetu ya kiswahili tumelitohoa na kulitumia yaani tumelikopa na kuwa "Amiri" .Yaani ni neno mkopo.
Neno mkopo ni kipengele cha kileksika kutoka lugha chagizi kinachoingizwa katika lugha pokezi ili kiweze kutumika kama neno rasmi la lugha pokezi, mara nyingi huweza kufanyiwa marekebisho au mabadiliko maalumu ya kifonolojia/kimofolojia aidha upande wa sauti,Silabi au irabu ili kukidhi mahitaji au maana ya msingi inayokuzudiwa katika lugha pokezi.
Katika dhana ya neno Ameer ,Amir lugha changizi ni kiarabu ,Lugha pokezi ni Kiswahili.
Tulivyochukua neno Ameer ,Amir kutoka lugha chagizi ya kiarabu tuliongeza irabu ktk lugha yetu Amir, tukaongeza i (Amiri) .
Pia tulibeba maana ya msingi "Kamanda" na bila kujali kamanda huyo awe wa kike au wakiume, sisi tuliangalia maana zaidi bila kuangalia linatumika kwa Jinsia gani. Na sisi tukalitumia kama Amiri Jeshi Mkuu tukiwa na maana Commander in Chief (C in C).
Tukisema tuangalie kubadili kuita Amirat ,kwa kubadili maana kwamba Sasa hivi aliyeshika madaraka ni mwanamke,tutaleta mchanganyiko sana ,Amirat hiyo ina maana nyingi sana Amirat ina maana ya kiongozi ,wengine Amirat hujulikana Kama First lady (Yaani Mke wa Rais ) , Princess (Binti Mfalme.
Sasa ili tumuite Amirat itatupaswa kutohoa neno hilo kutoka ktk kiarabu na kulipa maana mahususi kulingana na muktadha wa sasa ,sababu neno hilo lina maana nyingi ,hivyo maana rasmi itafanya watumiaji wajue kwanini tunatumia Amirat ,sawa na sasa hakuna maana zaidi ya kutumia Amiri zaidi ya neno "Kamanda " bila kujali jinsia aidha wa kike au kiume.
www.jamiiforums.com

Mama Samia ni Amir jeshi Mkuu au Amirat Jeshi Mkuu?
Wakuu, hii kitu imenichanganya, Marais wa kiume huitwa Amir jeshi mkuu. Msingi wa neno Amir ni neno la kiarabu ambalo lina maana kiongozi. Kwa kiarabu kiongozi wa kiume huitwa Amir na wakike huitwa Amirat .Je kwa mama Samia ataitwa Amir jeshi mkuu au Amirat? Wazee wa Itifaki naomba ufafanuzi...