Nakinzana na wanaotaka tuite Amirati Jeshi Mkuu badala ya Amiri Jeshi Mkuu

Nakinzana na wanaotaka tuite Amirati Jeshi Mkuu badala ya Amiri Jeshi Mkuu

Ebu na wewe kuwa mwelewa, huyu haitwi AMIR (kiarabu), anaitwa AMIRI (kiswahili) Sasa hayo uliyoandika kuwa ni Amir ambalo ni kiarabu uko sahihi sisi hatutumii kiarabu kwahiyo hakukuwa na haja ya kuandika hayo uliyoandika.
Sasa alichoandika mtoa mada sindio ulichoandika sasa umepinga umeunga alichoandika JF bana inachekesha
 
Kama ungesoma lugha ya kiswahili ungeelewa kwamba lugha yetu haina maneno ya feminine na masculine, ipo neutral neno moja laweza kutumika kwa jinsia zote tofauti na lugha kama kifaransa au kimasai. Masai hata salamu ya mwanamke ni tofauti na salamu ya mwanaume na ya kijana kwa mzee kila kitu lugha yao imechambua na hii akisalimia hata kama humuoni unajua Nani anaongea na nani hii haihusiani na haya Mambo yenu ya mfumo jike au dume au sijui mfumo gani . Hii ni ukomavu wa lugha. Kifaransa ni lugha ya siku nyingi sana nadhani kiingeleza kimechukua maneno mengi kwenye kifaransa. So ni ukomavu wa lugha tu haihusiani na haya Mambo yenu ya mifumo.
Sio ukomavu bali ni udhaifu wa lugha ya kiswahili. Ukweli utabaki kuwa lugha hii haijitoshelezi katika maneno bali kwa asilimia kubwa maneno yake yamekopwa kutoka lugha nyingi tofauti.

Lakini kusema eti kiswahili hakitambui jinsia si kweli kwakuwa baadhi ya maneno kama vile biharusi na bwanaharusi, shemeji na wifi yanatambulisha jinsia.
 
Amirati ndiyo mambo gani?

Lugha yetu ya Kiswahili siyo kiarabu

Imetohoa maneno kutoka kwenye lugha mbalimbali za kiafrica, kireno, kiarabu etc lakini kiswahili kinabaki kuwa ni kiswahili!

Sasa tusiigeuze lugha yetu mtumwa wa lugha nyingine

Kwetu sisi Amiri ni Amiri, hatujali jinsia yake!
 
Sio ukomavu bali ni udhaifu wa lugha ya kiswahili. Ukweli utabaki kuwa lugha hii haijitoshelezi katika maneno bali kwa asilimia kubwa maneno yake yamekopwa kutoka lugha nyingi tofauti.

Lakini kusema eti kiswahili hakitambui jinsia si kweli kwakuwa baadhi ya maneno kama vile biharusi na bwanaharusi, shemeji na wifi yanatambulisha jinsia.
Kuna maneno machache sana ambayo huwezi kugeneralize kwamba kiswahili kina masculine na feminine. Lugha kama kifaransa kila kitu kipo masculine na feminine. Labda unielewe kwa hapo maana mie ni mtaalamu wa lugha nimemaliza chuo miaka zaidi ya kumi na mbili sasa nafanyia kazi kiswahili ndio maisha yangu.
 
Nimeona Mjadala sehemu kwamba tubadili tuite Amirat badala ya Amir ,sababu amir ni kwa mwanaume na Amirat ni kwa mwanamke. Kwamba Mh.Rais,Samia Suluhu Hassan tumuite Amirati Jeshi Mkuu.

Nina kinzana na wanaotoa hoja ya kuita Amirati badala ya Amiri ,mbali na hoja ya kikatiba ibara ya 33 (2) inayo mtambua Rais Kama kiongozi wa nchi , kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu ,naomba nijadili suala hili kwa minajili ya kilugha tuu Kama linavyohojiwa na kujadiliwa kwa minajili ya kilugha.

Amir / Ameer ni neno la kiaribu kweli likiwa limelenga mwanaume kiongozi “leader”,Kamanda “commander”, Mtawala “ruler”, au chifu “chief”,.

Neno hili limetokana na neno la kiarabu A-M-R.(Kuamrisha au to command).

Neno hili ni la kiarabu, ila katika lugha yetu ya kiswahili tumelitohoa na kulitumia yaani tumelikopa na kuwa "Amiri" .Yaani ni neno mkopo .

Neno mkopo ni kipengele cha kileksika kutoka lugha chagizi kinachoingizwa katika lugha pokezi ili kiweze kutumika kama neno rasmi la lugha pokezi ,mara nyingi huweza kufanyiwa marekebisho au mabadiliko maalumu ya kifonolojia/kimofolojia aidha upande wa sauti,Silabi au irabu ili kukidhi mahitaji au maana ya msingi inayokuzudiwa katika lugha pokezi.

Katika dhana ya neno Ameer ,Amir lugha changizi ni kiarabu ,Lugha pokezi ni Kiswahili.

Tulivyochukua neno Ameer ,Amir kutoka lugha chagizi ya kiarabu tuliongeza irabu ktk lugha yetu Amir ,tukaongeza i (Amiri) .

Pia tulibeba maana ya msingi "Kamanda " na bila kujali kamanda huyo awe wa kike au wakiume ,sisi tuliangalia maana zaidi bila kuangalia linatumika kwa Jinsia gani. Na sisi tukalitumia kama Amiri Jeshi Mkuu tukiwa na maana Commander in Chief (C in C).

Tukisema tuangalie kubadili kuita Amirat ,kwa kubadili maana kwamba Sasa hivi aliyeshika madaraka ni mwanamke,tutaleta mchanganyiko sana ,Amirat hiyo ina maana nyingi sana Amirat ina maana ya kiongozi ,wengine Amirat hujulikana Kama First lady (Yaani Mke wa Rais ) , Princess (Binti Mfalme.

Sasa ili tumuite Amirat itatupaswa kutohoa neno hilo kutoka ktk kiarabu na kulipa maana mahususi kulingana na muktadha wa sasa ,sababu neno hilo lina maana nyingi ,hivyo maana rasmi itafanya watumiaji wajue kwanini tunatumia Amirat ,sawa na sasa hakuna maana zaidi ya kutumia Amiri zaidi ya neno "Kamanda " bila kujali jinsia aidha wa kike au kiume.View attachment 1733410
Kelele zote hizi mpaka Zitto akupe nondo za kuandika humu Jf.
 
Ebu na wewe kuwa mwelewa, huyu haitwi AMIR (kiarabu), anaitwa AMIRI (kiswahili) Sasa hayo uliyoandika kuwa ni Amir ambalo ni kiarabu uko sahihi sisi hatutumii kiarabu kwahiyo hakukuwa na haja ya kuandika hayo uliyoandika.
Umesema kweli. Nashangaa watu wanaokwenda kuelezea mambo ya lugha ya kiarabu wakati sisi tunatumia kiswahili. Kiarabu hakina neno ''Amiri''. Na ''Amiri'' tunayotumia sisi siyo kiarabu bali ni kiswahili, japo tunaweza kusema lilichukuliwa kutoka huko uarabuni zamani sana, lakini limeshakuwa letu na ni la kiswahili. Ni kama neno ''shule''. Hili ni neno la kijerumani linatokana na neno ''schule''. Kijerumani wingi wa shule ni ''schulen''. Sisi kiswahili wingi wa ''shule'' ni ''shule''. Neno likishachukuliwa kutoka lugha nyingine linakuwa la ile lugha nyingine na wana uhuru wa kulitumia wanavyotaka.
 
Sahihi! Amiri si neno la Kiarabu. Ni neno la Kibantu na Kiswahili lenye asili ya Kiarabu. Kama kweli lilipokuwa la Kiarabu lilimaanisha mwanaume pekee hiyo ni juu yao. Maneno hubadilika maana kadri ya matumizi, na hili ni neno la Kiswahili sasa ambalo halina ukakasi likitumika kwa jinsia zote mbili. Samia ni Rais na Amiri Jeshi Mkuu. Tukubali hivyo. Tutazoea tu.
Ebu na wewe kuwa mwelewa, huyu haitwi AMIR (kiarabu), anaitwa AMIRI (kiswahili) Sasa hayo uliyoandika kuwa ni Amir ambalo ni kiarabu uko sahihi sisi hatutumii kiarabu kwahiyo hakukuwa na haja ya kuandika hayo uliyoandika.
 
Kuna maneno machache sana ambayo huwezi kugeneralize kwamba kiswahili kina masculine na feminine. Lugha kama kifaransa kila kitu kipo masculine na feminine. Labda unielewe kwa hapo maana mie ni mtaalamu wa lugha nimemaliza chuo miaka zaidi ya kumi na mbili sasa nafanyia kazi kiswahili ndio maisha yangu.
Huyo hatakuelewa ulichozungumzia. Kuna lugha nyingi tu hazitofautishi kama ilivyo kiingereza kwa ''he'' and ''she''
 
Umeongea Point sana. uzuri umenukuu hadi katiba. Unataka twende kinyume na Katiba? Nashauri Katiba ifanyiwe Marekebisho ili kuendana na Wakati. Vinginevyo tutaendelea kumuita Amiri Jeshi Mkuu.
 
Back
Top Bottom