Nakinzana na wanaotaka tuite Amirati Jeshi Mkuu badala ya Amiri Jeshi Mkuu

Ebu na wewe kuwa mwelewa, huyu haitwi AMIR (kiarabu), anaitwa AMIRI (kiswahili) Sasa hayo uliyoandika kuwa ni Amir ambalo ni kiarabu uko sahihi sisi hatutumii kiarabu kwahiyo hakukuwa na haja ya kuandika hayo uliyoandika.
Sasa alichoandika mtoa mada sindio ulichoandika sasa umepinga umeunga alichoandika JF bana inachekesha
 
Sio ukomavu bali ni udhaifu wa lugha ya kiswahili. Ukweli utabaki kuwa lugha hii haijitoshelezi katika maneno bali kwa asilimia kubwa maneno yake yamekopwa kutoka lugha nyingi tofauti.

Lakini kusema eti kiswahili hakitambui jinsia si kweli kwakuwa baadhi ya maneno kama vile biharusi na bwanaharusi, shemeji na wifi yanatambulisha jinsia.
 
Amirati ndiyo mambo gani?

Lugha yetu ya Kiswahili siyo kiarabu

Imetohoa maneno kutoka kwenye lugha mbalimbali za kiafrica, kireno, kiarabu etc lakini kiswahili kinabaki kuwa ni kiswahili!

Sasa tusiigeuze lugha yetu mtumwa wa lugha nyingine

Kwetu sisi Amiri ni Amiri, hatujali jinsia yake!
 
Kuna maneno machache sana ambayo huwezi kugeneralize kwamba kiswahili kina masculine na feminine. Lugha kama kifaransa kila kitu kipo masculine na feminine. Labda unielewe kwa hapo maana mie ni mtaalamu wa lugha nimemaliza chuo miaka zaidi ya kumi na mbili sasa nafanyia kazi kiswahili ndio maisha yangu.
 
Kelele zote hizi mpaka Zitto akupe nondo za kuandika humu Jf.
 
Ebu na wewe kuwa mwelewa, huyu haitwi AMIR (kiarabu), anaitwa AMIRI (kiswahili) Sasa hayo uliyoandika kuwa ni Amir ambalo ni kiarabu uko sahihi sisi hatutumii kiarabu kwahiyo hakukuwa na haja ya kuandika hayo uliyoandika.
Umesema kweli. Nashangaa watu wanaokwenda kuelezea mambo ya lugha ya kiarabu wakati sisi tunatumia kiswahili. Kiarabu hakina neno ''Amiri''. Na ''Amiri'' tunayotumia sisi siyo kiarabu bali ni kiswahili, japo tunaweza kusema lilichukuliwa kutoka huko uarabuni zamani sana, lakini limeshakuwa letu na ni la kiswahili. Ni kama neno ''shule''. Hili ni neno la kijerumani linatokana na neno ''schule''. Kijerumani wingi wa shule ni ''schulen''. Sisi kiswahili wingi wa ''shule'' ni ''shule''. Neno likishachukuliwa kutoka lugha nyingine linakuwa la ile lugha nyingine na wana uhuru wa kulitumia wanavyotaka.
 
Sahihi! Amiri si neno la Kiarabu. Ni neno la Kibantu na Kiswahili lenye asili ya Kiarabu. Kama kweli lilipokuwa la Kiarabu lilimaanisha mwanaume pekee hiyo ni juu yao. Maneno hubadilika maana kadri ya matumizi, na hili ni neno la Kiswahili sasa ambalo halina ukakasi likitumika kwa jinsia zote mbili. Samia ni Rais na Amiri Jeshi Mkuu. Tukubali hivyo. Tutazoea tu.
Ebu na wewe kuwa mwelewa, huyu haitwi AMIR (kiarabu), anaitwa AMIRI (kiswahili) Sasa hayo uliyoandika kuwa ni Amir ambalo ni kiarabu uko sahihi sisi hatutumii kiarabu kwahiyo hakukuwa na haja ya kuandika hayo uliyoandika.
 
Huyo hatakuelewa ulichozungumzia. Kuna lugha nyingi tu hazitofautishi kama ilivyo kiingereza kwa ''he'' and ''she''
 
Umeongea Point sana. uzuri umenukuu hadi katiba. Unataka twende kinyume na Katiba? Nashauri Katiba ifanyiwe Marekebisho ili kuendana na Wakati. Vinginevyo tutaendelea kumuita Amiri Jeshi Mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…