Nakiona kifo changu! Msaada wenu unahitajika

Nakiona kifo changu! Msaada wenu unahitajika

Sayidaas

Member
Joined
Apr 3, 2019
Posts
35
Reaction score
64
Wakuu habarini! Nimeshare shaver jana na mgongwa wa UKIMWI bila kujua bahati mbaya wakati natumia nilijikata.

Leo ameenda kuoga na yeye akatumia hiyo shaver kumuuliza akasema hiyo niyake na huwa anatumia yeye ikabidi niangalie kwa makini nikagundua nikweli mimi ndio nilikosea nikatumia yake.

Nimemuuliza ushawahi kujikata na shaver yako akasema nikawaida huwa anajikata yani hapa tumbo limepata joto msaada wenu nifanye nini
 
Mkuu relax, nenda hosptal ya karibu kama unahisi umekua exposed waelezee utapewa utaratibu then upewe PEP na kama alikua positive uwezi kupata maambukizi. Na hata kama utakua umepata(japo ni ngumu ukifata huo ushauri) uwezi kufa haraka haraka ivyo kama unavyofikiria. Asante
 
Ni mpaka kuwe na mgusano wa damu zote mbili ndio unaweza kupata maambukizi, na kama yuko tayari kwenye dozi hupaswi kuogopa sana.

Ingia mitandaoni upate elimu ya ukimwi usije ukafa na hofu bure.. Hofu inauwa ..hofu ni ugonjwa hatari kuliko hata huo ukimwi
 
Nenda hospital acha kelele huku watu tumepumzisha mafuvu yetu
 
Mkuu pole sana. Nenda Hospitali mapema (kabla ya saa72 kupitia).Watakupima kwanza ili wajue kama ulikuwa na Ngoma kabla ya tukio hilo.

Wakikuta kuwa huna Ngoma watakupa vidonge 30 vya PEP umeze mwezi mzima. Hii itakulinda kupata maambukizi ya virusi kutoka kwenye hiyo shaver.Ahsante.
 
Mnaweka nyembe sehemu ili iweje?
Kwanin usifiche chako au ukatupa kabisa ukihitaji unanunua kipya unatupa
 
umeshakufa mpaka hapo we katafute jeneza sanda anza na kujichimbia shimo mwenyewe kabla hujasumbua watu kuchimba sana
 
Unanikumbusha kisa cha jamaa mmoja aliyepata ugonjwa wa akili baada ya kuhisi kaambukizwa UKIMWI.
Acha ushamba wewe utakufa kihoro huku huyo mgonjwa anaendelea kula kuku
 
Back
Top Bottom