nakonda/napungua uzito msaada jaman

kirama00

Member
Joined
Jan 25, 2013
Posts
27
Reaction score
0
habari wakuu mimi n kijana mwenye miaka 21 nipo chuo na uzito wa 50kg thn nqa uref wa 5.4 nashindwa kuelewa kwa nini uzito wang ni mdogo kiasi hicho wakati nakula vizur bila ya hata kupitisha mlo na huwa hata siumwi mara kwa mara zaid ya mafua ya kuja na kupotea kila m2 huwa ananiambia cku znavyozd kwenda nazd kupungua but na mshukuru mungu mwaka jana mwshon nlipima hili gonjwa letu kubwa sina sasa wakuuu nshaurin nfabye nn maana nakereka mno ....asanten
 
Wenzio tunalipa hela kukonda na kupungua uzito wewe unalalamika!!
 

Kama huumwi, kuwa na amani. Hata mimi nilikuwa na kilo kama 50, katika ujana wangu, lakini sasa nina 84. May be genetic make up yako ni hiyo. Usilazimishe. Huwezi kuwa na HIV maana dalili zake ziko wazi bila kificho.
 
Punguza kupiga punyeto.

halafu wewe ndugu yangu unamajanga mengi mara uzito mara uso?

Pole sana ndugu yangu mpendwa!!!
 
jee una stress zozote?umeshawahi kupima kisukari?kuna kitu kinaitwa thyroid hormones level.mimi sio dokta ila kuna kipimo chake,sijui hizo hormones zikizidi mwilini au kupungua zinasababisha kupungua uzito.
 

Ndugu yangu wala usiwe na wasiwasi. Tena nakuomba unachokula usibadilishe kwa kuwa uko fiti sana (kama vipimo vikubwa umefaulu)

Sababu:

Utapiamlo na utipwatipwa unapimwa kutumia kipimo cha BMI, BODY MASS INDEX (kiasi cha mafuta mwilini kwa umbile lako).

Hii inapimwa hivi: BMI = UZITO(kg)/UREFU(m)squared

BMI chini ya 18.5 = utapiamlo
18.5 - 25 Normal
25 - 30 Overweight
zaidi ya 30 = Obese

Kwa vipimo vyako ulivyotoa your BMI ni 18.9 ambayo ni nzuri sana.

Usitafute unene bwana. Kuupata ni rahisi sana lakini kuupunguza ni zahama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…