Nakopesha kwa riba

ameline

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2013
Posts
2,292
Reaction score
1,151
habari zenu wadau...pamoja na shughuli zangu ninazofanya za kibiashara vilevile nilivutiwa na rafiki yangu aliekua anakopesha fedha kwa riba na kupata faida kubwa kwa haraka...yeye alianza na mil 30 na alikua maarufu sana hata wafanyabiashara wanaokwama marejesho na kodi hukimbilia kwake...basi mimi sikua na mtaji mkubwa sana nilianza na mil 10 nikawa nakopesha kuanzia laki 5 kwa riba ya laki...sasa mtaji wa kukopesha umekua mpaja mil 22 kwa miaka .ingawaje kuna changamoto za hapa na pale lakini nikavumilia tu ingawaje sijawahi kurushwa...

OMBI:
Naomba kwa yeyote mwenye uelewa na hizi microfinance institution anisaidie mfano kama finca, opportunity, brac n.k nafikiria kuanzisha Taasisi yangu pia ila sijui ni mtaji kias gani unatakiwa na vigezo gani..kwani natamani hata vijana wajiunde kwenye vikundi ili niwape hela za kuanzia polepole ila kwa hi style yangu ya kukopesha kienyeji sitaweza kwa hili.
Naomba mwenye uelewa anisaidie tafadhali..hata kuonana nae ikiwezekana..nipo arusha..wengi wenye hizo taasisi ukiomba ushauri wanadharau tu na kukejeli..JF nimeona ndo kimbilii langu...Ahsanteni
 
Biashara yeyote ina startup costs, kama kupanga ofisi, kuajiri wafanyakazi, kufanya registration BOT na nyinginezo. Kwa huo mtaji wako ni mdogo, unajikuta unakula mtaji hadi unaishia kwenye kuanzishia kampuni. (unless una other plan). Kuna insuarance za kukata, pia kumbuka risk ni kubwa sana. Jichange hadi ifike kama 100-200 mil.
Wish u luck pia.

Sent from my Nokia Lumia using Tapatalk
 
Mtafute mtaalamu wa microfinance kwa ushauri japo atakutoza fees kidogo lakini ninao uhakika atakuonesha njia ya kupita. Hajaniomba nimsemee lakini mpigie 0714000023. Kila la kheri.
 
Ndugu angalia sana Biashara za riba ni machukizo kwa Mungu!
 
=>still monitoring it, the biz intresting me too! can i star it with o/d monies
 
Naomba unikopeshe hizo ulizano basi,huku ukifuatilia kusajiri
 
=>still monitoring it, the biz intresting me too! can i star it with o/d monies

kama imeandikwa kwa kiswahili na wewe ukasoma ukaelewa:; kwann ujibu kwa kingereza?? halafu lugha za.kifacebook huku hazimo ndugu..andika kwa kirefu neno lieleweke..sasa biz...marao o/b sio kila mtu anaelewa..
 
Mkuu unaweza kunikopesha na Mimi nahitaji millioni moja tu...
 
mkuu ningependa nijue ni kwa jinsi gan unahakikisha hela zako zinarud kwa wakat maana nataka nianze na mimi hii biashara
 
unakopesha kwa riba ya asilimia ngap na kwa mda gani? Nipo arusha, nahitaji pesa na nina mali isiyohamishika. Tiririka hapa tufanye biashara mwayego.
 
Bwana Johny Cash...(John Fedha)

Utaishia Hivi






 
Biashara Nzuri ni Siasa tu... hata ukilala pesa zinaingia kila siku... bila kusahau ukikaa pia ni pesa
 
Ndugu angalia sana Biashara za riba ni machukizo kwa Mungu!

Hivi hii imekaaje? Niliwahi kufikiria kuingia kwenye hii biashara, lakini nikakumbuka mahali fulani nilisoma kuwa Mungu hafurahii mambo ya riba, nikapata ethical dilema nikaacha hiyo biashara. But I think its a lucrative business ukipata wateja productive!
 
Hata hizo islamic bank zinatoza riba kinachofanyika ni wanabadili jina la riba tu, kama unabisha nenda kakope hata laki uone kama utawarudishia laki tu
 
Ukiachia mungu kukataza biashara hii pia kuna sheria ambayo kama sijakosea hairuhusu mtu binafsi kufanya hii Biashara. Kwa maelezo zaidi hii biashara ndo ambayo inamtesa papaa msofe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…