sema ni kwa sababu ya kuwa ana fanya biashara lakini... sikuwa nime muelewa tangu post yake ya kwanza... kuna sehemu ukimuuliza kitu ana kinganisha na tiles ndo hapo napata shida kumuelewa...
Tiles kuna za wachina wanakata majabali haya kama kule mwanza na zina toka tiles za hatari angalia makazi mengi bado watu wanazielewa tiles na fashion hupita, sasa unapo sema tanga ztone zitakuwapo milele fashion haito isha ndio una toa ulinganishi wa namna hii kwa mteja daaah
napata wasiwasi sana kama wewe sio dalali una tafuta kazi na kwenda kuwapa vibarua wafanye sina uhakika...
Mkuu kwanza nafurahi kwa kwa kuchangia kwenye tangazo. Tanga stone siku hizi zinakatwa kwa size tofauti tofauti kulingana hitaji la mtu. Hivyo hapa tiles zinaingia kwasababu mtu akikupa kazi ya Tanga stone za kukata anataka kulinganisha na garama za ujenzi wa tiles.
Suala la kusema kwamba ukinipa kazi unataka nifanye kwa mkono wangu, haya si mawazo ya ki maendeleo hata kidogo, maana yake ikiwa wewe ni fundi cherehani kwenye flame yako inahitajika Cheleheni moja tu. Kwa msingi huo hutakiwi kuanzisha huduma hiyo sehemu nyingine.
Kwa mawazo ya aina hii nikikwambia mimi ni fundi rangi ukikutana na mimi unataka uone shati langu limesheheni matone ya rangi ndo uamini mimi ni fundi rangi.
Si hivyo tu, Ukimuita Mturuki akakwambia anajenga sqm moja kwa tsh. 35,000 unaona ni sahihi, mimi mswahili kwa tsh. 15,000 unaniita Dalali, Mturuki unampa kazi ananipa mimi nifanye bado yeye humuoni dalali.
Mturuki akija site kwako ana ku charge stie visiting tena kwa $ unaona ni sasa, lakini nikija mimi mswahili, unashindwa kuheshimu muda wangu hata nauri hutoi unasema natafuta kazi. Kazi hizi hizi wakija weupe wanawakaanga fedha nyingi na mnaona ni sahihi kuwalipa na mwisho wa siku zinafanywa na sisi waswahili, bado mnaona ni sahihi na mnajinadi kwamba weupe wame husika kwenye Project zenu.
Sent using
Jamii Forums mobile app