Nakubaliana na Rais Magufuli kwa sababu enzi za "mitishamba" afya za Watanzania zilikuwa imara!

Nakubaliana na Rais Magufuli kwa sababu enzi za "mitishamba" afya za Watanzania zilikuwa imara!

Unadhani dawa za mabeberu wanazitoa kwenye mwezi bwashee?!

Ni hii hii mitishamba.
Sawa ni mitishamaba, lakini tumeshindwa nini sasa, hadi tuzitegemee dawa zao??na kutoka hapa sio suala la kuamka tu na kujipa matumaini tu, dawa za mabeberu ni mbaya!!KABLA YA KWENDA MBALI, sana, namuomba meko atangaze kuanzia kesho ni marufuku kwa daktari kumchoma mgonjwa sindano ya GANZI, na zote zilizopo nchini ziteketezwe !!pale anapomtoa jino mgonjwa , na wazalendo wote tumuunge mkono kwa hilo!!ili itumike ile yetu ya asili, sijui inaitwa KANYAMPASIRA KIBOKO YA GANZI!!!!
 
Unajua vina ya afya wanapiga je pesa?

Wauguao ni wachache sana kuliko wanaougua.

Pana watu wapo kwa hata miaka zaidi ya 10 hawajaugua wala kutumia dawa yoyote. Je nao unapendekeza waanze kupiga debe kuachana na mambo ya tiba kabisa?

Mkuu usitukane mamba. Changamoto za kupumua zinahitaji ventilator!

Kwenye tiba asikilize mnazo?
Mkuu sijakataa uwepo wa Ventilator kama mgonjwa atahitaji. Hapa nasemea Issue ni kupambana immune ikae vizuri hata vikiingia virus vigonge mwamba au viishie njiani. Yaani kutumia asili kuboresha kinga. Pia dawa asili zipo za kuponyesha magonjwa mbalimbali ambayo hospital unaweza kutumia muda mrefu bila kupona na mwishowe dawa ni sumu hizo. Anyway, maisha na afya ya mtu iko mikononi mwake hivyo uamuzi ni wa mtu binafsi na hakuna anayelazimishwa. Binafsi chanjo sitapiga kabisa hiyo. Pamoja na umri nilio nap mkubwa ninaendelea kuimarisha silaha za mwili, kujikinga kufuata maelekezo ya wataalam na kumuomba Mungu.
 
wazungu wametuwin kifikra tu bt hawana lolote, hata leo wakituacha huru kifikra na kiutawala tutawafunika kwa kila kitu.
 
Kwasasa Nchi ina Changamoto ya upungufu wa Madarasa, upatikanaji wa maji upungufu wa Matundu ya vyoo na Changamoto hii ni yamiaka ming sanaa miaka60 ya Uhuru bado tunaongelea hizo changamoto Halafu Anatokea Mjinga Mmoja Anasema eti Rais aongezewe muda hata kama hatak Alazimishwe!
Wewe dish litakuwa limecheza,maada iliyopo mezani ndio hii unayoongelea wewe?, Anzisha uzi unaohusu hili la kwako,usituchafulie mada sisi,
 
Ingekua vyema kama kwenye border kungekua na ukaguzi mkali leo hii magonjwa kama
UTI
TYPHOD
AMOEBA

Na mengine mengi yasingekua bongo kwani haya yote yaliletwa.
Wizara ya afya badala ya kutenga budget kubwa za madawa ingewaza upande wa pili wa jinsi ya kutokomeza baadhi ya maradhi kama Malaria

Sidhani kama budget ya kufanya famigation kuua mazalia ya mbu ni kubwa kama budget ya kununua dawa za Malaria

Sidhani kama budget ya ku’treat’ maji kuua mazalia ya Typhod na Amoeba ni kubwa kama kununua Dawa na sindano za kutibu hayo magonjwa

Miti shamba ni jambo zuri lakini tukae kujua kwamba miti shamba reaction yake kwa magonjwa huchukua muda kutibu kulinganisha na dawa na sindano

Pia kuna baadhi ya magonjwa huwezi kutikwa miti shamba i.e mgonjwa kuhutaji oxygen

Serikali ianze kua na vipaumbele vya kutokemeza haya magonjwa sumbua kama Malaria. Toka unazaliwa mpaka unakufa unasikia kila siku Malaria ni mbaya Malaria inaua
Hizi ndizo hoja zinazotakiwa kwenye mijadala km hii,kosoa lkn utoe mbadala wake,km taifa nini tufanye,
 
Anachokisema Rais Magufuli ni kwamba Watanzania tusipaparikie chanjo bali tuimarishe kinga zetu kwa kutumia tiba na njia za asili ambazo zimekuwepo kwa muda mrefu.

Nijuavyo mimi kitengo cha utafiti wa tiba za asili kimekuwepo tangu 1971 kabla hata ya hii NIMR iliyoasisiwa miaka ya 1980s na dawa za asili zimeponya na kuimarisha kinga za watanzania wengi.

Nakubaliana na Rais Magufuli kwamba tuchukue tahadhari kwa mbinu zetu za ndani badala ya kukimbilia chanjo ambazo hatuna uhakika nazo.

Hata kuku wa kienyeji kinga yake ni tofauti na kuku wa kisasa kama unabisha waulize wafugaji watakuelimisha.

Maendeleo hayana vyama!
Ujinga ni mzigo, kuutua ni ahueni kubwa. Tiba za jadi zipo tangu enzi, ziliokoa maisha. Maendeleo ya tiba kuvumbuliwa chanjo na kuboresha dawa za asili kumeimarisha afya na kupunguza vifo na kuongeza umri wa kuishi. Leo magonjwa ni mengi na kuleta hoja ya kubeza chanjo ni aibu. Za kuambiwa ongeza na zako. Wanasiasa wanakusanya watu wengi kwenye mikutano, majukwaa yao yapo mbali na umati, speaker zinafikisha ujumbe, anaeongea humwoni. Tena sasa kuna majukwaa mawili, wageni waalikwa wana jukwaa lao mbali.
 
Kwasasa Nchi ina Changamoto ya upungufu wa Madarasa, upatikanaji wa maji upungufu wa Matundu ya vyoo na Changamoto hii ni yamiaka ming sanaa miaka60 ya Uhuru bado tunaongelea hizo changamoto Halafu Anatokea Mjinga Mmoja Anasema eti Rais aongezewe muda hata kama hatak Alazimishwe!
Vyote poteza, lakini akili hapana.
 
Ingekua vyema kama kwenye border kungekua na ukaguzi mkali leo hii magonjwa kama
UTI
TYPHOD
AMOEBA

Na mengine mengi yasingekua bongo kwani haya yote yaliletwa.
Wizara ya afya badala ya kutenga budget kubwa za madawa ingewaza upande wa pili wa jinsi ya kutokomeza baadhi ya maradhi kama Malaria

Sidhani kama budget ya kufanya famigation kuua mazalia ya mbu ni kubwa kama budget ya kununua dawa za Malaria

Sidhani kama budget ya ku’treat’ maji kuua mazalia ya Typhod na Amoeba ni kubwa kama kununua Dawa na sindano za kutibu hayo magonjwa

Miti shamba ni jambo zuri lakini tukae kujua kwamba miti shamba reaction yake kwa magonjwa huchukua muda kutibu kulinganisha na dawa na sindano

Pia kuna baadhi ya magonjwa huwezi kutikwa miti shamba i.e mgonjwa kuhutaji oxygen

Serikali ianze kua na vipaumbele vya kutokemeza haya magonjwa sumbua kama Malaria. Toka unazaliwa mpaka unakufa unasikia kila siku Malaria ni mbaya Malaria inaua
Hospitali zetu zote, japo za umma ni zaidi, ni vituo vya magonjwa. Ukilazwa ukabahatika kutibiwa ugonjwa uliokulaza uanatoka na mwingine. Mbu kila kona, vyoo vichafu, mende na kunguni wanavinjari.
 
Hiyo mitishamba ilitibu polio,ndui,kifua kikuu,kifaduru,e.t.c?Au umeamu tu kujitoa ufahamu kama walivyo CCM wengine?
 
Naunga mkono hoja...ila siwezi fanyia kazi ushauri kama huo toka kwa mtu anayeweza tibiwa popote duniani....samahani kwa hili.
 
Back
Top Bottom