Nakubaliana na Rais Magufuli kwa sababu enzi za "mitishamba" afya za Watanzania zilikuwa imara!

Unadhani dawa za mabeberu wanazitoa kwenye mwezi bwashee?!

Ni hii hii mitishamba.
Sawa ni mitishamaba, lakini tumeshindwa nini sasa, hadi tuzitegemee dawa zao??na kutoka hapa sio suala la kuamka tu na kujipa matumaini tu, dawa za mabeberu ni mbaya!!KABLA YA KWENDA MBALI, sana, namuomba meko atangaze kuanzia kesho ni marufuku kwa daktari kumchoma mgonjwa sindano ya GANZI, na zote zilizopo nchini ziteketezwe !!pale anapomtoa jino mgonjwa , na wazalendo wote tumuunge mkono kwa hilo!!ili itumike ile yetu ya asili, sijui inaitwa KANYAMPASIRA KIBOKO YA GANZI!!!!
 
Mkuu sijakataa uwepo wa Ventilator kama mgonjwa atahitaji. Hapa nasemea Issue ni kupambana immune ikae vizuri hata vikiingia virus vigonge mwamba au viishie njiani. Yaani kutumia asili kuboresha kinga. Pia dawa asili zipo za kuponyesha magonjwa mbalimbali ambayo hospital unaweza kutumia muda mrefu bila kupona na mwishowe dawa ni sumu hizo. Anyway, maisha na afya ya mtu iko mikononi mwake hivyo uamuzi ni wa mtu binafsi na hakuna anayelazimishwa. Binafsi chanjo sitapiga kabisa hiyo. Pamoja na umri nilio nap mkubwa ninaendelea kuimarisha silaha za mwili, kujikinga kufuata maelekezo ya wataalam na kumuomba Mungu.
 
wazungu wametuwin kifikra tu bt hawana lolote, hata leo wakituacha huru kifikra na kiutawala tutawafunika kwa kila kitu.
 
Wewe dish litakuwa limecheza,maada iliyopo mezani ndio hii unayoongelea wewe?, Anzisha uzi unaohusu hili la kwako,usituchafulie mada sisi,
 
Hizi ndizo hoja zinazotakiwa kwenye mijadala km hii,kosoa lkn utoe mbadala wake,km taifa nini tufanye,
 
Ujinga ni mzigo, kuutua ni ahueni kubwa. Tiba za jadi zipo tangu enzi, ziliokoa maisha. Maendeleo ya tiba kuvumbuliwa chanjo na kuboresha dawa za asili kumeimarisha afya na kupunguza vifo na kuongeza umri wa kuishi. Leo magonjwa ni mengi na kuleta hoja ya kubeza chanjo ni aibu. Za kuambiwa ongeza na zako. Wanasiasa wanakusanya watu wengi kwenye mikutano, majukwaa yao yapo mbali na umati, speaker zinafikisha ujumbe, anaeongea humwoni. Tena sasa kuna majukwaa mawili, wageni waalikwa wana jukwaa lao mbali.
 
Vyote poteza, lakini akili hapana.
 
Hospitali zetu zote, japo za umma ni zaidi, ni vituo vya magonjwa. Ukilazwa ukabahatika kutibiwa ugonjwa uliokulaza uanatoka na mwingine. Mbu kila kona, vyoo vichafu, mende na kunguni wanavinjari.
 
Hiyo mitishamba ilitibu polio,ndui,kifua kikuu,kifaduru,e.t.c?Au umeamu tu kujitoa ufahamu kama walivyo CCM wengine?
 
Naunga mkono hoja...ila siwezi fanyia kazi ushauri kama huo toka kwa mtu anayeweza tibiwa popote duniani....samahani kwa hili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…