Nakuchukia Baba yangu

holoholo

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2023
Posts
1,859
Reaction score
2,986
Wakuu,

Nimelelewa na mama yangu kwa asilimia 90 mpaka hapa nilipo.

Baba yangu aliondoka nyumbani mwaka 2011 akamuacha mama yangu akiwa amejifungua wiki mbili akaenda kusikojulikana na mwanamke mwingine, akatuacha hakuna chakula wala matumizi yoyote ya mama na sisi wanafunzi, Ilibidi mama aanze vibarua ili tule na tusome mimi na dada yangu ninaemfuata.

Hata sisi tulipotoka shule ilibidi twende kwenye vibarua kwa ajili ya chakula na madaftari, sabuni na matumizi mengine.

Nimepitia mateso makuu sana mpaka nimefika hapa nilipo kwa sababu ya baba yangu! Siku nyingine nitawaletea mkasa mzima ila kifupi namchukia mno baba yangu!
 
Hapo anajua yeye ni baba tu ipo siku mtamtumia pesa akipata shida..Mfumo wa kuzaana ni mateso tu hapa duniani ni mengi sana .

Kuna mambo mtu unakaa kimya bora ya wale mayatima ,unakuta wazazi wametengana mama yako mzazi kaolewa hataki mfike kwake mnaweza kumuharibia ndoa yake ,kila kitu atashughulia baba yenu.
Kiufupi kuzaana ni utapeli kila binadamu ni mbinafsi ,anazaa watoto kama ulinzi wake wa baadaye ila hana juhudi za kulinda furaha yao kabisa.
 
Una umri gani sasa?
 
Kataa Ndoa wanaokimbia familia hapa Hutawaona
 
Subiri na wewe uwe baba ndo utajua masahibu aliyokua anapitia baba yako!!!

Wanawake ni miongoni mwa viumbe hatari especially hawa single mingle mazazi
mama yangu tangu aolewe na baba mwaka 1986 hadi leo hawawahi kuzaa na mwanamme mwngn tofauti na baba yangu mimi, na tuko watoto 8 je mama ni singe maza?
 
Father alikuwa akipata pesa anaondoka na kutokomea kusikojulikana maisha yanatuchapa tukiwa na mama, lakini after all nimeamua kumsamehe chuki ni jela ya nafsi.
Ulitaka ukimchukia ndio atakufa.

Unamsamehe tu ila hapati kitu changu chochote........hii kubembelezana ni kulea ujinga.

Pesa zako unakula na mademu na pombe mimi za jasho langu uje kula bure tu? Huu ujinga mimi nilishaacha.

Sikufanyi kitu, wala sifatilii mambo yako ila changu cha jasho langu utakisikia kwenye redio. Maisha yanaendelea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…