Wakuu,
Nimelelewa na mama yangu kwa asilimia 90 mpaka hapa nilipo.
Baba yangu aliondoka nyumbani mwaka 2011 akamuacha mama yangu akiwa amejifungua wiki mbili akaenda kusikojulikana na mwanamke mwingine, akatuacha hakuna chakula wala matumizi yoyote ya mama na sisi wanafunzi, Ilibidi mama aanze vibarua ili tule na tusome mimi na dada yangu ninaemfuata.
Hata sisi tulipotoka shule ilibidi twende kwenye vibarua kwa ajili ya chakula na madaftari, sabuni na matumizi mengine.
Nimepitia mateso makuu sana mpaka nimefika hapa nilipo kwa sababu ya baba yangu! Siku nyingine nitawaletea mkasa mzima ila kifupi namchukia mno baba yangu!