Nakuchukia Baba yangu

Pata na story ya upande wa pili,itakusaidia ku balance nani wa kumchukia kati ya Mama na Baba!!
 
Vijana ndio mnakuja hapa na mada zenu za kukataa ndoa, mnategemea watoto wazaliwe na kukuzwa kwa namna gani?

Kataa ndoa italeta single mamaz wa kutosha, watoto wanaolelewa na mama peke yao, jamii ya hovyo kabisa.

Endeleeni kukataa ndoa!
 
Ulikuwa na wiki mbili ulijuaje kama kakimbia na mwanamke mwengine? Wazee miyeyisho wapo, ila nimejifunza kuwa makini sana tunapowatuhumu wazee wetu, wengi wamebeba siri nzito sana ambayo wakikuambia utajikana na utaishi maisha ya upweke sana.
mama alikuwa na wiki mbili tangu ajifungue. Wakati mimi nasoma darasa la tatu 2011 rudia kusoma post yangu mkuu.
 
Asije akawa mama Yako alikuwa nakamdomodomo sana,geuza na upande wa pili Mkuu!
 
Pole kwa yote uliyopitia!

Inaumiza mzazi kukutelekeza ama kutokupatia kitu fulani hasa kipindi Cha utotoni na wakati wa kukua hapa na inapelekea watoto wengi kuwa na maumivu, chuki, hasira na wengine hata ubinafsi!

Lakini jitahidi upate kupona, majeraha hayo ya kutokupata malezi na matunzo ya baba mzazi!

Kumbuka binadamu yeyote anakosea hivyo mzazi naye anakosea Tena pakubwa tuu, msamehe mzee.....

Najua mama yako alikulisha maneno na kumsema mshua, sana na ninyi watoto kuyachukua maneno mazima mazima na kujenga uadui kati yenu na baba yenu...... Acha kushikilia maneno ya mama yako au sumu aliyoiweka juu ya mumewe!

wewe fanya hivi hakikisha unapona unakuwa na amani ukimuona mzee wako usisikie kuumia!

Ikiwa yupo hai kamsalimie, mpe zawadi, mpe hela ondoa kinyongo wacha yeye apokee hukumu ya alichokifanya kwenu lakini wewe usiwe hakimu wa kumhukumu!

Muheshimu mpende mzee wako! Hakuna baba mwingine mzee,

Pia huwez jua tatizo lililomfanya akimbie ni nini ukiwa wewe ni wa kiume unayaelewa maisha basi nenda taratibu Jenga mahusiano mazuri na baba yako mzazi! Ikawe khery
 
Achana na mambo ya kuchukia mtoto wa kiume umekuja kupambana, kikubwa uko Hai pambana, miaka 23 umri bado sana huo unaweza fanya makubwa, ya maza na mdingi yaache
 
Mkuu shem alichepuka ukamsamehe.
 
Haisaidii, subiri uingie kwenye taasisi ya ndoa,utakuja kukiri hapa kuwa baba Yako alikuwa sahihi kumkimbia mama Yako,wakati mwingine sisi wanaumw tunapitia mambo magumu sana kwenye ndoa ila hatusemi Wala kumwambia mtu
 
Vijana ndio mnakuja hapa na mada zenu za kukataa ndoa, mnategemea watoto wazaliwe na kukuzwa kwa namna gani?

Kataa ndoa italeta single mamaz wa kutosha, watoto wanaolelewa na mama peke yao, jamii ya hovyo kabisa.

Endeleeni kukataa ndoa!
Tunakataa kufunga ndoa sio kuishi na mwanamke.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…