Nakuja Dar kutafuta maisha, nimechoka kukaa nyumbani

Biashara;
1. Utanunua Matunda mazuri utayakata na kuwawekea kwenye vikontena na Toothpick kwa gharama ya 1500,

2. Uza Samaki wa Kukaanga au Pweza na Ngisi

3. Uza Kuku wa kukaanga vipande.

4. Uza Mishikaki na Ndizi

5. Mayai ya Kuchemsha, kuna Mashine zipo Mayai yanakua hayapoi, wateja unawamenyea na kuwawekea chumvi (sijajua mashine zauzwa kiasi gani)

NB: Wafanyabiashara wadogo wadogo siku hizi hawatakiwi mjini, utapambana upate sehemu nzuri usisumbuliwe.
 
Fursa unaziacha Mwanza mkuu usije mjini
 
Asante
 
Njoo nikuunganishe ukavue samaki Baharini.
Kwa siku mkipata unaweza kusahau umasikini na ukikosa unakosa kweli.

Uvivu kamali
Mtaji nguvu
Kama upo Tayar ncheki PM
Na je biashara ya uvuvi una ujuzi nao?ukitaka kuingia rasmi unaitajika uweje kuanzia mtaji?
Nauliza hivi sababu kuna kipindi nikikuwa naenda beach maeneo ya warioba

Ni kila siku nikawa nawaona wavuvi mida ya jioni wanaingiza boti zao mida kama sa nane wakirudi inakuwa kama saa 12 jion na samaki

Wanaanza kutoa kwanza samaki za boss then za kwao wanauza pale pale wanaondoka na elf 50
Kwa kipindi kile niliona ni biashara nZuri kuliko hata daladala

Ningeomba ushauri wako asee
 
Hapo aeleze kiundani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…