Nakula mlo mmoja kupunguza mwili. Je ni sahihi?

JOYSTICK

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2014
Posts
221
Reaction score
57
Wadau,

Nina 102kgs, nimeamua kuanza kula mlo mmoja wa mchana tu, huku jioni nikipitisha na maji tu. Breakfast nayo ni Mara moja moja. Lengo langu ni kufika 85kgs.

Je, nini hasara ya njia hii ya kupunguza mwili? Faida pia napenda kuzijua.
 
Mimi nijuavyo sio vizuri kuacha kula, ila inabidi ule kiasi kidogo sana cha chakula<milo yote mitatu> Kunywa maji mengi angalau lita 3 kwa siku.
 
Wadau Nina 102kgs

Una urefu kiasi gani?

nimeamua kuanza kula mlo mmoja wa mchana tu huku jioni nikipitisha na maji tu.Breakfast nayo ni Mara moja moja.Lengo langu ni kufika 85kgs.

Kutokula haimaanishi kuwa ndio dawa ya kupunguza uzito wa mwili...

Mtu anaweza kuendelea kula kama kawaida na uzito wake ukapungua...

Hili linawezekana kama tu ukifuata kanuni sahihi ya ulaji mlo kamili pamoja na mazoezi ya kupunguza nishati ya ziada mwilini...

Jaribu kufuata utaratibu huu,

Asubuhi jitahidi upate matunda au juisi halisi ya matunda, wanga kidogo sana...

Mchana kula mlo kamili wenye wanga, hamirojo na vitamini...

Usiku kula chakula chenye hamirojo tu na vitamini, usilie wanga...

Zingatia kunywa maji na usiache mazoezi ya mwili angalau kwa siku mara moja...

Je nini hasara ya njia hii ya kupunguza mwili?

Utapata hasara za kiafya ambazo badala ya kupungua mwili utadhoofu mwili kwa kukosa virutubisho stahiki...

Unaweza ukaishia kupata vidonda vya tumbo na magonjwa mengine yasiyo ya kuambukiza...

Faida pia napenda kuzijua.

Hakuna faida ya kiafya...

Labda sana kama ni mbahili utasema una-save pesa...
 
Mkuu kuna njia moja rahisi na huhitaji kusweat kwanza ondoa wanga completely kwenye menu yako, kula mara sita kwa siku high protein foods, size ya ngumi yako. Mara 3 kati ya hizo sita tumia protein snacks, google home made protein snacks utaona zipi unaweza kujitengenezea.

Tembea about 5km kila siku, say jioni baada ya kazi. Maji kwa wingi na sukari as minimal as possible. Mwezi unaweza punguza 6kg, I have been there done that!!!
 
Kula mlo mmoja si njia sahihi ya kupunguza uzito. Kabla sijaanza kutoa somo if you don't mind naomba unipe urefu wako ili tujue your BMI na ideal weight... Then tutaendelea
 
Mimi nilikuwa na kilo 87 nikaaanza maozoezi ya kupanda ngazi za gorofa asubuhi kila siku monday to friday kutoka floor number one to floor number ten taratibu wala sio kwa jogging wala kukimbia ila natembea taratibu.

Nikifika floor number ten nakuwa nime sweat sana, nakaa napumzika halafu nakunywa maji kama glass mbili au tatu halafu jioni natembea kwa miguu kurudi nyumbani wala sio mbali ni kama kilo mita 15, na pia sinywi soda but only once nikijisikia tu.

Huwezi amini ndani ya wiki tatu nime lose kilo 4. Mwili bado ni mkubwa kiasi ila tumbo kwisa kutoka size 38 to 36. Nakula mlo wote asubuhi chai ya tangawizi au asali, mchana nakula soup, wali kidogo ila nyama NO once a week jioni naweza kunywa maziwa ya mtindi au, ugali kidogo sana au wali.

Sijinyimi chakula hata siku moja ila kikumbwa ni kupunguza wingi wa chakula kama ulikuwa unakula wali sahani full kula robo na maji mengi na ukiendelea hivyo utazoea tu. Mazoezi yangu ni kutembea tu.
 
Very good Mildred...

Losing weight is all about life style changes not dieting. Jitahid ule mboga za majani na matunda ya kutosha katika kila mlo. Pia usile chakula cha usiku muda mfupi kabla ya kulala...

Kabla hujalala kunywa maji angalau glass moja
 
kutokula haitasaidia,itakuletea vidonda vya tumbo tuu,..unahitaji kula healthy food (mboga mboga,carbohydrates kidogo,matunda etc) hizi soda sijui mikaangizo unahitaji kuacha,ni vigumu kuacha ila anza na kupunguza,..punguza portion za kula, unaweza kula hata mara 5 kwa siku ila kiwe chaakula au snacks zinazoleta afya...usisahau mazoezi na kunya maji.. ukiamua iwe lifestyle yako na si tu upungue alafu uanze tena kula kula mbona utajipendaa
 
Nikama uko na aneroxia nervosa/bulimia....just google that plus utafte advise on management
 
ukifeel kula kula, kula matunda na mbogamboga za kutosha, usijitese hivyo
 
Pole. suala hapa ni kuwa unakula nini na kiwango gani! unaweza kula mlo mmoja wenye wanga mwingi,mafuta mengi nk badala ya kula mlo wenye rishe bora, kwa mwili na uzito huo inabidi ujue uzito sahihi unaostaili kadili aya urefu wako pia (yaani body mass index). nadhani unatakiwa kushauriwa au soma namna ya kula mlo kamili wenye. matunda na mbogamboga kwa wingi na wanga kidogo na mafuta kwa mwili bado unahitaji vyakula hivyo kidogo. Lakini nadhani wengi huwa tunasahau kuwa tunahita kupunguza uzito na kusafisha mwili wako pia kutokana kula sumu nyingi zinazotokana na vyakula,madawa na uvutaji wa hewa chafu. nadhani pengina utashangaa kama mwili unatakiwa kusafishwa kwa kunya maji mengi na vyakula vingine na pia kuna program za kusafisha mwili.kikawaida huwa tunasafisha nguo.nyumba zetu, magari nk lakini huwa tunasahau kusafisha miili yetu. ukitaka ushauri zaidi 0689 417 472
 
Kupunguza unene sio kula mlo mmoja kwanza kazma ujue unene unasababshwa na nn......maelezo zaidi 0714.912390
 
Wadau,

Nina 102kgs, nimeamua kuanza kula mlo mmoja wa mchana tu, huku jioni nikipitisha na maji tu. Breakfast nayo ni Mara moja moja. Lengo langu ni kufika 85kgs.

Je, nini hasara ya njia hii ya kupunguza mwili? Faida pia napenda kuzijua.

Dah kumbe wewe umeacha kula kwa raha zako! Lowasa akiingia madarakani atahakikisha watanzania wanakula milo minane kwa siku badala ya mmoja!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…