Ajira ndio hizo tumeshapigwa bao, basi hata tuwe suppliers of fresh produce kama mboga mboga, mayai nk. Pia iwe chachu ya ushindani kwa bidhaa zetu (super brands) kushindana na za wenzetu kwa ku stock bidhaa zetu huko Nakumatt. Bado tuna safari ndefu mpaka tutoke kwenye usingizi wa kibiashara.
mkuu siunaona machezo wanayopiga wabongo pale mlimani city.. ukitaka receipt 45,000/= bila receipt 32,000/= ... ikitoka nje gari imevunjwa kioo mlinzi yupo pembeni unamuuliza anakujibu sio kazi yangu kulinda magari. Wizi tz umeanza kutoka mlinzi wa getini mpk _________. Tujirekebishe watanzania na haka katabia
Wapi Imalaseko?
Watanzania tunapenda sana kulalamika, binafsi ninapenda sana Wakenya walivyo firm on issues, very aggressive, with good customer care. Na hawa jamaa wa NAKUMATT nawajua vizuri, wako mbele ya Customer Care, (kuna kitu inaitwa Customer Experience). Nadhani ujio wao utakuwa na Positive Demonstrational Effect kwa wazawa (watanzania) kwani kila wakiambiwa kwa maneno wabadilike wanakuja juu, sasa ni wakati wa kuona na kujifunza kwa vitendo.
Karibuni Tanzania
@Komandoo umesema ukweli unaouma. Ila watz hata tukiunganisha nguvu uaminifu hamna. Angalia kilichotokea NICO ambapo tulitegemea walau wawe chachu ya kuunganisha nguvu baina yetu. Kwa kweli tutalia hadi siku ya kiama bila mafanikio. Nadhani Nakumatt watakuwa wapangaji pale inapojengwa complex ya AICC kwa kushirikiana na LAPF. Na kama hilo litatolea utakuwa ndio mwisho wa shoprite Arusha kutokana na business location kuwa-favour NAKUMATT. Poor TZ!
WAKUU, MIMI SIONI TATIZO KWA HAWA WAKENYA KUJA KUWEKEZA TANZANIA, TUJIULIZE
1. Kuna kampuni ya Tanzania imejaribu kwenda kuwekeza kenya ikazuiwa?
2. Watanzania Tutaendelea kuwafanyia kazi hao wakenya kwa sababu ya upumbavu wetu wenyewe, NITATOA MFANO WA KWENYE MAHOTELI, KUNA KAMPUNI MOJA INAYO MILIKI HOTELI KADHAA HUSUSANI KWENYE HIFADHI ZA SERENGETI, NA NGORONGORO,
1. Mwanzoni wafanya kazi karibia wote walikuwa Watanzania, kukaibuka vitu vifuatavyo
- WIZI WA VITU VYA HOTELI KAMA VILE GLAS, VIJIKO, MASHUKA, VIKOMBE NA KAZALIKA
- Kampuni ilikuwa inabidi kila mwezi wanunue vitu vya kureplace vilivyo potea katika mazingira ya kutatanisha,
- Kampuni baada ya kufanya uchunguzi na kuweka mitego walibaini kuna chein ya wizi ya kufa mtu, kuanzia kwa wafanya usafi, walinzi, wahudumu kwenye vyumba vya kulaa wageni, Baa na Hoelini
- Walijenga Chaini Huyu wa Baa akivusha glass basi na wewe wa kwenye room jitahidi uvushe mashuka na taulo il baadae wafany buter trade.
HAPA MNATEGEMEA NINI? KWA NINI WASIAJIRI WATU WA NJE?
- WATANZANIA TUTABAKI KULALAMA SANA MPAKA MWISHO WA DUNI
- NAKUMBUKA RAIS MSTAAFU MKAPA ALIWAHI KUSEMA" WATANZANIA BILA YA KUUNGANISHA MITAJI HATUTAWEZA KUSHINDANA NA MAKAMPUNI MAKUBWA YA NJE"
COME TO THE POINT, ALIKUWA ANAMAANISHA HAYA YAFUATAYO
1. Kila mtanzania anataka awe na FUSO lake mwenyewe la kubebea mizigo ya watu,
- Je utaweza kushindana na makampuni makubwa ya usafirishaji yatakayo kuja kuwekeza Tanzania?
2. Kila mtanzania anataka awe na Basi lake, awe Haice zake mwenyewe, awe na Tex zake mwenyewe, Awe na mashine ya kusaga nafaka
- Je yakaja makampunu makubwa na kuivest kwenye mabasi ya kubeba abilia ni nani ataweza kufurukuta?
3 Kila mtanzania anataka kuwa na Duka lake mtaani na kwingineko, kila mmoja
4. Kila mtanzania anawaza kuanzisha Min supermarket
- Hizi min Supermarket tunazo jivunia zitaweza kusimama kwa haya makampuni yenye mitaji ya kufa mtu?
- Tutaweza kushindana na Shoprite?
- Je tutawaweza NAKUMATT
- Tutawaweza UCHUMU SUPERMARKET?
- Watanzania Tutabali kulia, C jajua hapa Serikali ifanye nini, kwani hao wakenya wamepewa fedha na serilkali yao waje kufungua biashara Tanzania?
- Cheki kwenye mabenk, Je serikali inahusika vipi? Kenya comercial Benk walipewa fedha na Serikali yao waje kuwekeza Tanzania?
WATANZANIA KILA MTU AKITAKA AMILIKI, FUSO LAKE, MASHINE YA KUSAGA YA KWAKE, MIN SUPERMAKET YAKE, BASI LAKE NA KAZALIKA TUTAKUJA KULIA KILIO KILICHO KIKUU.
WATU WENGINE WANAAMUA KUUNGANISHA MITAJI YAO NA KUJA NA KAMPUNI MOJA YENYE NGUVU SISI HUKU NI KILA MTU ANATAKA AONEKANE ANAZO PESA HAIJARISHI ANAMILIKI NINI.
-YATAKUJA MAKAMPUNI MENGI SANA KUTOKA NJE WEEZA KWENYE USAFIRI WA MABASI TENA YA LUXURY NA BEI NAFUU SISI TUTABAKI KULAUMU SERIKALI
WATAKUJA WATAWEKEZA KWENYE UBEBAJI WA MIZIGO KWA UFANISI NA KWA BEI YA CHINI, SISI NA USANII WETU TUTABAKIA NA FUSO ZETU TUNAZO MILIKI KILA MTU
WATAFUNGUA SUPERMARKET KUBWA SANA, SISI TUTABAKIA NA MIN ZETU TUTAJIKUTA TUNAGEUKA KUWA WANUNUZI KWENY CAMPUNI ZETU WENYEWE
TUSIPO BADILIKA NA KUUNGANISHA MITAJI YETU HAKIKA TUTAKUJA KUJUTA, TUTAJIKUTA TUNA KUWA THE CONSUMER OF HIS/HER OWN GOODS AND SERVICES
Hata kama tukijenga zetu, umeshashuhudia "customer services" zetu?
Yaani watu wanatka kazi, wakishaipata, maadili na uchapaji kazi unasahaulika mara moja!
Hii ni ktk kila sekta, benki, serikalini na hata walio na biashara zao, tuko tuko tu, mwenye duka, anaweza kuwa ameishia stock za bidhaa fulani, inaweza kumchukua wiki hata mwezi hadi atakapo nunua tena stock, anachekelea na kufurahia kabisa anapokujulisha kuwa kitu ukitakacho hakipo!
Wache wageni waje watufundishe adabu kidogo!
Watu wengi bado tunapenda kwenye masoko ya kawaida na maduka madogo na hii inatokana na unafuu wa bei.Bidhaa za supermarket ni bado anasa.bado tunasafari kubwa ya kuelimisha wafanyabiashara juu ya soko la hisa ...mi siamini kabisa kwamba sisi hatuna mtaji wa dola mil 1.4 au hata dola mil 10 ....imagine wafanyabiashara kama mohammed ent na bakhresa wakaanzisha supermarkets zao na kuuza bidhaa za kutoka viwandani mwao na tanzania ...sasa hata ukiwa na watu kama 10 tu ka hao industry itabadilika ..ndo maana wakenya wanatupiga bao
Jamani tusikimbie ukweli,
Tatizo sio uaminifu wa wafanyakazi kama watu wengi wanavyojaribu kuelezea maana hata hao Nakumatt na Uchumi kama ilivyo Shoprite, Games etc, etc kisheria bado watendelea kuajiri wabongo hao hao ukiondoa labda wafanyakazi wachache senior.
Pia tatizo sio mtaji kwa maana yapo makampuni mengi tu ya kibongo yenye mitaji mikubwa sana mpaka hata kuwekeza kwenye nchi za nje. Mfano angalia Bakhresa group (Kenya, Uganda, Mozambique, Malawi, Rwanda, Zambia), Exim-Tanzania bank (Djibouti, Comoro), TANALEC Ltd, (Nchi zote za EAC na maziwa makuu), Precision Air etc, etc. Pia NICOL si iliweza ku-mobilize nchi nzima na kuuza hisa wakapata mtaji mkubwa lakini wakazitumia vibaya/bad investment decisions?.
Matatizo yetu makubwa:
Kama KOMANDOO na ben van mike walivyonena huko juu bado wafanyabiashara wetu particularly kwenye hili eneo la supermakets wanaendesha kienyeji sana (lack of professionalism and modernity). Hivyo basi elimu zaidi juu ya namna ya kuendehsa biashara kisasa zaidi inahitajika.
Creative minds za vijana zinahitajika sasa, matajiri wengi wakibongo (wengi wao wazee) bado ni waoga ku-take risks, kumbukeni hata Uchumi supermakets ilielekea kufa kufa mwaka mwaka mmoja tu uliopita hivi sasa ndio inarudi tena.
Concept ya Chain stores sio mpya hapa Tanzania, kwa sababu zamani/enzi za mwalimu tulikuwa nazo na tulikuwa tunaziendesha kwa ufanisi mkubwa tu japokuwa hakutuwa na variety kubwa ya bidhaa kwenye shelfs mpaka tulipoanza mambo ya uchumi huria. Mfano ni hayo maduka ya RTC, maduka ya shirika la ugawaji etc, etc. yalikuwa yamesambaa nchi nzima na ndio wananchi walikuwa wakiyategemea.
Tuache tabia ya kulalamika na kuogapa kila kitu, tunatakiwa kubadilika. Nakumatt, Uchumi Shoprite, Games hayo yote ni maduka tu hakuna cha zaidi. Hakuna kisichowezekana.
Mkuu unachosema ni kweli, but kumbuka hayo makampuni unayo yataja yanafanya biashara nyingine kabisa, na ni kweli yana mitaji mikubwa sana
- MIMI NINACHO SISITIZA NI SWALA ZIMA LA MITAJI.
1. JE IKAJA KAMPUNI MFANO KUTOKA NJE KUWEKEZA KWENYE USAFIRI WA MABASI NA WAKAJA NA MABASI KAMA 500 KUNA KAMPUNI YA BONGO ITAWEZA SIMAMA?
2. HATA SUPERMARKET KUNA MINSUPERMARKET KIBAO TANZANIA WANA CUSTOMER CARE YA KUFA MTU BUT HAWAWEZI SHINDANA NA KAMPUNI KAMA SHOPRITE AU UCHUMI SUPERMARKET KWA SABABU YA MITAJI.
- C KWAMBA KAMPUNI ZETU HAZIFANYI VIZURI ZINAFANYA VIZURI KABISA TATIZO NI MITAJI YA KUWEZA KUSHINDANA NA MAKAMPUNI KUTOKA NJE,
3. KAMPUNI KAMA DR EXPRESS WANAJITAHIDI SANA NA KUNA NYINGI ZA MABASI ZINAJITAHIDI ILA IKAJA KAMPUNI KUBWA NINA UHAKIKA HAKUNA JIWE LITAKALO SALIA JUU YA JIWE JINGINE.
WATANZANIA KILA MTU ANATAKA AONEKANE YEYE KAMA YEYE, ANATAKA AMILIKI KITU CHAKE MWENYEWE, HUKU TANZANIA MAMBO YA KUUNGANISHA MITAJI HAYAPO KABISA NA HII ITAKUJA KUTO COST SANA, KAMPUNI NYINGI HAZITAWEZA KUSHINDANA.
CHUKULIA MFANO WA BIASHARA YA MABASI, UTAKUTA KUNA MTU ANA MABASI MAWILI, MWINGINE MATATU, MWINGINE MATATANO NA KAZALIKA, HEBU JARIBU KUWAAMBIA HAWA WAUNGANISHE NGUVU KAMA WATAKUELEWA