Nakuomba Waziri Mbarawa ukajionee wizi na uozo unaolitafuna Shirika la Reli ya Kati kipande cha Tabora - Mpanda

Nakuomba Waziri Mbarawa ukajionee wizi na uozo unaolitafuna Shirika la Reli ya Kati kipande cha Tabora - Mpanda

The Phylosopher

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2015
Posts
1,968
Reaction score
2,957
Ni jumapili iliyopita nilipojaribu kusafiri Kutoka kijijini Ukumbi kakoko kilichopo mpakani mwa mikoa ya Katavi na Tabora kuelekea Tabora mjini, ambapo kwa bahati mbaya siku hiyo treni ilichelewa kupita hivyo nikalazimika kusafiri kesho yake yaani jumatatu.

Nilichokishuhudia kwenye hii safari yangu kilinifanya nijiskie uchungu sana wa namna shirika letu lilivyogeuzwa kuwa kitegauchumi cha watu binafsi, huku kukiwa hakuna dalili ya kiongozi yeyote kuguswa na uozo wizi ubadhirifu na ufisadi unaofanywa na maofisa na watumishi wa treni hiyo.

Hebu nieleze kwa ufupi namna ufisadi unavyofanyika:

Mosi: Maofisa wa reli hufanya mazingira ya shida ya usafiri iliyopo maeneo hayo kuwa ngumu zaidi kwa makusudi, kwa kupeleka mabehewa machache ukilinganisha na mahitaji yaliyopo. Jambo hili hupelekea ugumu wa usafiri kuongezeka na kufanya rushwa iwe suluhisho la haraka kufanikisha usafiri na usafirishaji.

Pili: wahudumu wa treni maarufu kama tt huchukua tiketi za abiria waliofika mwisho wa safari na kuziuza kwa abiria wengine pasipo kupeleka chochote kwenye shirika.

Tatu: kuna watu wanaosafiri kwa kumpa mhudumu nauli mkononi pasipo mhudumu kumpa tiketi yoyote na ukidai tiketi unaulizwa "wewe shida yako si kufika unakokwenda?" Hapo ukizingatia ugumu niliouseema pale mwanzo unalazimika kuwa mpole.

Kwa mtindo huu katika vituo vyote ambavyo havikatshi tiketi, ambavyo ilipaswa tiketi ziuzwe ndani ya treni pesa yake huliwa na wahudumu.

Hii ni mifano michache tu ya namna pesa zinavyopigwa bila woga Wala haya.
 
Massanja Kadogosa ndie Mkurugenzi Mkuu wa TRL hebu ngoja atupe jibu😆😆😆😆
Ngoja tumtag hapa kupitia yule verified member wake wa JF, ndugu Tanzania Railways Corp hebu chunguzeni huu ubadhirifu.

Alafu siyo huko tu, hata pale main station gerezani kuna madudu yanafanyika kwa abilia wanaokatisha tiketi.

Mfano, ukienda pale kukata tiketi jamaa wanajifanya hawapokei keshi means lazima ulipie through mitandao ili upeleke payment slip wao wakupe tiketi.

Kinachofanyika ni kulazimisha mtu alipie kwa wale mawakala waliojazana pale station wakati mtu anaweza kulipia kupitia simu yake, hii ya kulipia kwa wale mawakala ni business ambayo jioni kuna posho wanapewa kutokana na wateja waliolipia kwao.

How mnalizimishe abilia alipie pale 🤔?.
 
Acha tu. Ebu tazama hii clip ujionee uozo zaidi.
 
Back
Top Bottom