Nakupatia bure "Idea ya fursa", ukifanikiwa usinisahau

Stability

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2020
Posts
306
Reaction score
706
Hello wanaJamii,

Sitaki kujisifia kuwa hiii Idea ni bora au kabambe kuliko zote ila ni idea ambayo ni unique kwa hapa Tanzania na kama ukiwa serious unaweza toboa.

KWA NINI MIMI BINAFSI SIJAINVEST:
Sio kwa sababu ni ngumu au haina mashiko ila ni kutokana na kuwa na "options" za ideas nyingine so nikawa na uhuru wa kuselect idea tofauti. So naweza sema kulikuwa na factors tofauti (excluding capital) ambazo ziliweza kunilimit kuinvest hii idea.

KWA NINI NIMESHARE:
Wote tuna jukumu la kuwa na utu. So kwa nini niifiche hii idea wakati kuna watu wanatafuta fursa.

Kama mnavyoelewa kwa sasa Pesa inatembea kwa kasi katika biashara zinazohusiana na Teknolojia na Mtandaoni (online) e.g AMAZON, EBAY, TESLA..n.k. Kumekuwa na ongezeko la watu kwenda na kasi ya Teknolojia hapa nchini thus uhitaji wa huduma za kiteknolojia kuongezeka.

IDEA YENYEWE:
Inahusiana na site ya mtandaoni (ONLINE SITE) inayosaidia watu katika nyanja mbili muhimu.

1: Kutangaza UJUZI NA SKILLS ili wajipatie kibarua au tenda.

example;
NAME: John Michael
CONTACT: 0755xxxxxx
LOCATION: Tarime, Mara, Tanzania
EXPERTISE/SKILLS: Gypsum board decoration
DESCRIPTION: maelezo juu ya kazi zake
PREVIOUS PROJECTS: kama atakuwa na ushahidi wa kazi alizozifanya (maelezo au picha)
CERTIFICATION: kama anawez kuwa na certificate (cheti) juu ya exepertise au juu wake anaweza kuppload.
RECOMMENATION: Kwa watu watakao kuwa wana mfahamu kwa kazi zake wanaweza kumu - endorse

2: Kutangaza KAZI, KIBARUA au TENDA itakayohitaji ujuzi wa mtu.

example;
NAME: Viviana Joseph
CONTACT: 0763xxxxxx
CATEGORY OF EXPERTISE NEEDED: Pyschology and Counselling
DESCRIPTION: Nahitaji mtu aliebobea katika saikolijia na ushauri, kwa msaada wa kunitoa katika hili janga la depression.

Kwa Ujumla, zifuatazo ndio contents nilizotaka kuziweka katika hii site.

● MWANZO
-sign up
-log in

About us:
-sign up
-summary
-vision
-mission
-values
-links on social media

● THEN BAADA YA KU-SIGN UP
Mtumiani atahitaji kujiregister kama expertise au mtafutaji wa expert.

■ Expert:
-photo
-name
-contact
-description
-links
-expertise
-location
-previous projects
-certifications
-recommendation

■ Expert searcher:
-choose a category
-post a job
-description

Pia katika site yako, utahitaji kutofautisha ujuzi katika makundi tofauti ili iwe rahisi kwa watu kujitangaza au kutangaza vibarua vyao.

■ CATEGORIES:
1.Consulting, Writing And counselling
-legal consulting
-business consulting
-financial and social securities
-counselling & therapy
-proposal/project writing

2. SERVICES:
-decorations
-entertainment
-clearing & forwading
-relaxation
-food & catering

3. CONSTRUCTION, TECHNICAL AND FABRICATION
-interior design
-artitecture
-repairing
-elecrical
-mechanical
-welding
-painting and wall paper

4. DESIGNING AND CREATIVE
-fashion and clothing
-graphic designing
-photograph
-videograph
-drawing
-craftry

5. ACCESORIES AND GADGETS
-phone repair
-computer repair
-other gadgets repair
-TV, decoder services

6. AGENT
-trade Brokers
-real state brokers

7. INFORMATION TECHNOLOGY
-web building
-software/application dealers

8. PERSONAL CARE AND SAFETY
-security
-maid
-personal shopper
-delivery

9. OTHER EXPERTISES

● KUTANGAZA BIASHARA
So as long as hii ni biashara na wewe utahitaji kujitangaza ili wananchi wafahamu kuhusiana na online site yako.
Waweza kutumia njia zifuatazo

-social media advertising (kupitia Twt, FB, inst, etc )
-fika kwa watu wenye hizo expertises na uwapatie elimu ya site yako
-advertise on radio/tv
-attend conferences zinzohusiana na online businesses
-long tail keyword
-webinars

●MAPATO
-Itabidi uchunguze na ujifunze njia za wewe kupata kipato katika biashara ya online. Njia za kawaida za kupata kipato ni kama kutangaza biashara za watu wengine, malipo ya matangazo maalum ya ujuzi..etc

-Lakini pia baada ya platform yako kuwa maarufu unaweza kutengeneza "PREMIUM" site ambayo wewe tena ndio utakuwa agent wa moja kwa moja kwa hawa watafuta watu wa ujuzi. Watatakiwa kulipa montly charges za wao kuwa premium au wewe kupata commission katika kila malipo yao watakayo yapata. So utatakiwa usiweke contacts katika profile zao ili mtafutaji asiende kwao direct bali kupita kwako kwanza ili experts ndio wapate hizo projects.

That's it guys, hapo ndipo nilipofikia, kwa kupitia idea hii na wewe unaweza kuirekebisha au kuongeza vionjo vingine ili iwe nzuri zaidi.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ngoja nitranslate kwa kiingereza hii plan niongezee mbwembwe kidogo kisha nikaiuze kwenye platform Fulani ya sweden kama kawaida yangu
 
Hii idea ni kimeo. Kwa mtu ambaye hana msuli wa kutosha hata asijisumbue, atalia tu.

In short zipo agencies nyingi zinafanya. Sites za kutosha tu. Nyingine zinaoperate kimya kimya kwa kufanya CV - JOB Matching na wana connection za kutosha na waajiri wa makampuni, mashirika na taasisi mbalimbali.

Sio kila ambacho hukioni hakipo.
 
ahsante. ni kimeo kwako, kwa wengine ni mtaji.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona kuna jamaa humu anayo platform kama hiyo humu JF kilasiku anatangaza mpaka kachoka mara ya mwisho kupost kuotangaza kwakulazimisha watu wamempiga maneno.

Hizi zipo nyingi sana yaani na kwa Tz mbinde kutoboa.

Man Of October
 
H
Mbona kuna jamaa humu anayo platform kama hiyo humu JF kilasiku anatangaza mpaka kachoka mara ya mwisho kupost kuotangaza kwakulazimisha watu wamempiga maneno.

Hizi zipo nyingi sana yaani na kwa Tz mbinde kutoboa.

Man Of October
Kweli zipo nyingi sana na kuna za kibongo mpaka leo hazijachangamka kabisa miaka nenda miaka rudi
 
Ni wazo Zuri sana.Hata kama lipo tayari ni namna ya kutoka kwa njia nyingine kabisa au kuwa tofauti sana na hao waliopo.

Usikate tamaa..Kuna watu wameumbwa kurudisha watu.

Simamia unachoamini kwa nguvu zako.
 
Baada ya kuisoma idea yako, nimepata jibu sahihi kwanini umechagua kuzifanyia kazi idea zako nyingne na sio hii... Thank you
 
Ni wazo Zuri sana.Hata kama lipo tayari ni namna ya kutoka kwa njia nyingine kabisa au kuwa tofauti sana na hao waliopo.

Usikate tamaa..Kuna watu wameumbwa kurudisha watu.

Simamia unachoamini kwa nguvu zako.
Good
 
Nikikuita mchawi ntakosea?
Kwahio kwa sababu hivyo vi agencies vipo basi hata hio idea haiwezi kua implemented, basi hata hapa tanzania basi kungekua na kampun moja tu ya mabasi kwamba wao wameshaanzisha huduma za usafirishaji ..? Nonsensee!!
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sishangai watanzania ni wavivu sana , halaf pia kutoboa kwa kijana wa kitanzani itakua wachache sana, kwa staili hii ya kuangalia fulani kaanzisha kitu hakifanikiwi, na yeye anatoa conclusion haraka sana kwamba haina maana, bila kufanya analysis na research ya kutosha kwamba kwanini kitu fulani kisifanikiwe,
Mna safar ndefu sana vijana kwa staili hii, mtaendelea kuyasoma mafanikio kwa wengine mkiendelea na mentality hii mbovu
Mbona kuna jamaa humu anayo platform kama hiyo humu JF kilasiku anatangaza mpaka kachoka mara ya mwisho kupost kuotangaza kwakulazimisha watu wamempiga maneno.

Hizi zipo nyingi sana yaani na kwa Tz mbinde kutoboa.

Man Of October

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu zangu , tukianza kufikiria .."ohh kuna fulani ameisha ianzisha,...ooh..hii idea ni ngumu bongo, oooh sijui matapeli watakuwa wengi" hatutakaa kuendelea.

Usiniambie hauwez kuacha kuanzisha kampuni yako ya mabasi kutoka mwz hadi dar eti kisa kuna mabasi mengi ya kutoka dar hadi mwz.

Cha muhimu ni kuichukua idea yotote ile na kuitengeneza kuwa katika muundo ulio bora.

WaTanzania tusipende vitu virahisi tu, Virahisi vyote vilikuwaga vigumu then vikafanywa virahisi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…