Nakushauri Juma Mgunda, waachie Simba timu yao kasake riziki mahali pengine

Hata huyo mzoefu kuna sehemu alianza akavumiliwa na akaaminiwa mpaka akawa mzoefu......hata Mgunda angeaminiwa na kuvumiliwa angekuwa mzoefu.......
Huyu Mgunda angefungwa makundi nyie ndio mngekuwa wa kwanza kutukana viongozi kwa kumtegemea kocha kama Mgunda. Acheni tuboreshe benchi la ufundi tuache kukariri.

Hivi siku ile tunaenda kucheza Malawi Mgunda ndio kasafiri na timu unafikiri kuna mbinu alifundisha? Lakini timu ilishinda! Mgunda ana sifa zake lakini uwezo wake una ukomo kwa game ngumu.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Wacha ufala saivi watu wanaangalia maslahi na sio heshima. Unajua mgunda pale ssc anapata bei gani ikifananisha na hizo timu nyingine? Leo hii feitoto anawaita yanga utopolo sababu hawajakidhi maslahi yake.
 
Chaguo la Robertinho.View attachment 2487910

Mgunda anasogezwa pembeni kijanja, ajiongeze..
Ni jambo la kawaida timu inapoleta kocha mpya benchi la ufundi hubadilika.

Kuna makocha hupendekeza assistants wao kuna wengine huwa hawana shida wanafanya kazi na mtu yoyote.

Msimu wa 2017/2018 Pierre Lenchantre alikuja na msaidizi wake licha ya uwepo wa Masoud Djuma.

2018/2019 baada ya Uchebe kuajiriwa Simba alikuja peke yake lakini alishindwa kuendana na Masoud Djuma ikabidi aondolewe. Baadae Uchebe alifanya vizuri tu akiwa na Dennis Kitambi pamoja na Adel Zrane.

Similarly Sven Vandenbroek aliajiriwa pamoja na Suleiman Matola wakafanya kazi vizuri tu na Adel Zrane.

Didier Gomez Da Rosa alikuja peke yake alifanya kazi vizuri tu na Seleman Matola pamoja na Thiery Hitmana.

Pablo alikuja peke yake ila alidemand kocha wa viungo tofauti na akafanya kazi vizuri tu na Matola.

Zoran Maki Alitaka benchi lake analolifahamu yeye aliletewa watu wake hata kuondoka aliondoka nao wakati huo Matola walikuwa naye.

Hata sasa kama Robertinho anataka assistant wake tofauti na Mgunda apewe tu binafsi sioni kama Robertinho ni kocha msumbufu mithili ya Sven, Uchebe, Lechantre au Maki. Robertinho anaonekana kuwa mtu humble tu asiye na makuu.

Tuache uswahili hata timu za Ulaya makocha pro ambao ni assistant huwa wana resign kama kocha mkuu ameondoka na kocha mpya akapatikana.
 
Nimeshasema several times Simba recently imejikusanyia kundi kubwa la mashabiki wajinga wajinga wamejaa mihemuko tu.

Ni muhimu kocha mpya kuja na assistants wake ni jambo la kawaida kwenye football.
 
Simba kweli wamepania safari hii huko CAF. Hapo mmoja anajua vizuri mbinu za Vipers, mwingine anajua vizuri mbinu za Wamorocco. Msiojua kinachoendelea tulieni ackson.
Kocha wa simba hawezi kujua mbinu za vipers, anaweza kuwajua kiufundi tu, mbinu ni swala la kocha aliye na timu.
 
Baadae timu ikifanya vibaya huyo mbrazil na muarabu wanafukuzwa Kisha timu anakabidhiwa Mgunda na Matola.

Waafrika hatuna thamani hata ktk ardhi yetu wenyewe.
 
Simba kweli wamepania safari hii huko CAF. Hapo mmoja anajua vizuri mbinu za Vipers, mwingine anajua vizuri mbinu za Wamorocco. Msiojua kinachoendelea tulieni ackson.
Mgunda pale simba anavuta 10m plus. Akirudi coastal au hizi timu nyingine atalipwa 2m au chini ya hapo. Akijaribu tu kuondoa mguu simba, itakula kwake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…