Chaguo la Robertinho.
View attachment 2487910
Mgunda anasogezwa pembeni kijanja, ajiongeze..
Ni jambo la kawaida timu inapoleta kocha mpya benchi la ufundi hubadilika.
Kuna makocha hupendekeza assistants wao kuna wengine huwa hawana shida wanafanya kazi na mtu yoyote.
Msimu wa 2017/2018 Pierre Lenchantre alikuja na msaidizi wake licha ya uwepo wa Masoud Djuma.
2018/2019 baada ya Uchebe kuajiriwa Simba alikuja peke yake lakini alishindwa kuendana na Masoud Djuma ikabidi aondolewe. Baadae Uchebe alifanya vizuri tu akiwa na Dennis Kitambi pamoja na Adel Zrane.
Similarly Sven Vandenbroek aliajiriwa pamoja na Suleiman Matola wakafanya kazi vizuri tu na Adel Zrane.
Didier Gomez Da Rosa alikuja peke yake alifanya kazi vizuri tu na Seleman Matola pamoja na Thiery Hitmana.
Pablo alikuja peke yake ila alidemand kocha wa viungo tofauti na akafanya kazi vizuri tu na Matola.
Zoran Maki Alitaka benchi lake analolifahamu yeye aliletewa watu wake hata kuondoka aliondoka nao wakati huo Matola walikuwa naye.
Hata sasa kama Robertinho anataka assistant wake tofauti na Mgunda apewe tu binafsi sioni kama Robertinho ni kocha msumbufu mithili ya Sven, Uchebe, Lechantre au Maki. Robertinho anaonekana kuwa mtu humble tu asiye na makuu.
Tuache uswahili hata timu za Ulaya makocha pro ambao ni assistant huwa wana resign kama kocha mkuu ameondoka na kocha mpya akapatikana.