Nakushauri ndugu yangu Emmanuel Mbasha, hata wajinga huzeeka

Ambakucha

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2019
Posts
317
Reaction score
520
Wadau poleni kwa majukumu. Kuna picha mitandaoni inayomwonesha muimba nyimbo za Injili, Emmanuel Mbasha akiwa beach (nadhani), amevaa taulo tu huku sehemu ya boxer ikionekana.

Wachangiaji wamemshauri kwa hekima kwamba, angejisitiri vizuri maana yeye ni mtumishi wa Mungu (pengine kweli).

Lakini pia siku za nyuma, huyuhuyu Mbasha aliwahi kupost picha ya nyani (au sokwe) wakijamiiana!! Nayo ikazua balaa. Pia aliwahi kupost picha akiwa Zanzibar na binti yake (huku ikijulikana kwamba hakuwa na mkewe, walishaachana).

Sasa mimi najiuliza, Mbasha kama kweli ni mtumishi wa Mungu kwa nini hawi kioo?

Mambo anayoyafanya si kielelezo hata kidogo kwamba, kwa matendo yake mwingine anaweza kusema 'awe kama yeye.'

Ninavyojua Mimi, mtu anayejipambanua kuwa ni mtumishi wa Mungu anatakiwa awe kielelezo. Afanane tabia na uadilifu wa jamii yake. Huwezi mtaani kusema umeokoka au unamwimbia Bwana huku unaoneshewa kidole kwa matendo yako yenye kutia shaka.

Yesu walipomshutumu kwamba alikuwa kinyume na mafundisho ya uadilifu, aliwataka mafarisayo wataje kazi zake mbaya, mafarisayo wakashindwa kuzitaja (hazikuwepo).

Uadilifu wa Yesu uliingia mpaka kwa wanafunzi wake. Walimuiga kila kitu. Ndiyo maana Petro alipomfuata Yesu, kwa Kuhani Mkuu baada ya kukamatwa, watu waliomuona walimjua kuwa, alikuwa mwanafunzi wake, licha ya Petro kukataa.

Lakini wakasema 'hata kutembea kwake' kunafanana na Yesu, achilia mbali ongea yake. Mtu anayesema ameokoka anategemewa awe mfano mzuri kwa matendo yake ili watu waseme zamani alikuwa hivi, kabadilika, kweli wokovu upo (Kama jambazi anapoacha ujambazi wake).

Ndugu yangu Mbasha amekuwa kama ameokokea fasheni. Akumbuke zamani alikuwa Muislamu, akaenda ukristo. Kwa hiyo anatakiwa kusimama sawasawa bila kutia mbwembwe.

Nasema mbwembwe kwa sababu anayoyafanya huwezi kusema 'ni ubinadamu', bali anajiendekeza na kujipuuza, pia hajijali kwamba yeye ni nani!

Anasahau kwamba, kuwa mtumishi wa Mungu maana yake Mungu ndiyo bosi (mkuu), Sasa inakuaje mkuu awe mwema, lakini msaidizi wake ndiyo Mbasha? Mimi namshauri Mbasha kutafakari sawasawa, ayafanyayo hayana ubinadamu bali ni ushamba au kutotumia akili kuwaza sawasawa kabla ya kuamua kutenda.

Vyema kila mara kumwomba Mungu hekima kwani mwisho wa siku uzee utamfika na watu hawataweza kumpa cheo cha 'ana hekima' kwa sababu ya uzee kwani hata wajinga nao huzeeka!!

Kwa matendo yake ya mitandaoni, itafika nahali watu hawatakuwa na shaka na yeye, bali huyo mchungaji wake, kwamba anashindwa wapi kumnyoosha 'bwana mdogo' kama Mbasha?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu jamaa ni msanii kama wasanii wengine ,sioni kosa lake

Ni msaka riziki kama wajanja wengine , Anajipendekeza kwenye Utawala huu , anaimba nyimbo za kusifu na si kukosoa

Kwahiyo acha ale bata

Mwenye shida ni wewe unayemuona ni mtumishi , Wakati yeye anajiona ni msanii kama wasanii wengine
 
Umenena. Kweli 'great thinker'

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ungetumia huo muda kiufanya shughuli zako binafsi za maendeleo ungekua mbali kuliko kufatilia maisha ya mwanaume mwenzako
Mkuu hii ni forum,siyo kila kinachochapishwa humu lazima ucomment.......kuna taarifa unazopenda wewe wengine hawapendi so kila mtu ukimfuatilia utapata tabu sana.


Then,next week nitakuja niangalie ile project yako ya ujenzi wa ghorofa lako kama umeshafanya finishing maana unaonekana upo busy sana na mambo ya msingi
 
Mathayo 7:16-21

Mtawatambua kwa matendo yao. Je, watu huchuma zabibu katika miti ya miiba, au tini katika mbigili? La!

Basi, mti mzuri huzaa matunda mazuri, na mti mbaya huzaa matunda mabaya.

Mti mzuri hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mbaya hauwezi kuzaa matunda mazuri.

Kila mti usiozaa matunda mazuri utakatwa na kutupwa motoni.

Kwa hiyo, mtawatambua kwa matendo yao.

“Si kila aniambiaye, ‘Bwana, Bwana’, ataingia katika ufalme wa mbinguni; ila ni yule tu anayetimiza matakwa ya Baba yangu aliye mbinguni.
 
Umeona mkuu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tujitahidi kutofautisha kujiajiri na kumtumikia Mungu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…