Nakusudia kuanzisha Ranch/Kufuga ng’ombe wa nyama- Naomba ushauri

Hapana ndiyo nimeanza,bado wachache.
Umepata mbegu mapacha ? Hao ulionao umewanunua wapi.
Nipo ktk fikra ya kuamua niweke ranchi au nilime mazao. Najaribu kutafuta mbuzi wa mapacha walio wanene
Kama unajua alie nao wazuri unijulishe. Shamba lako lipo wapi ?
 
sawa.
Mbuxi 100 wanakula mwaka mzima hio heka. Hawajitaji majani mengine.
Halafu umeonesha sample moja tu. Nyinhine vipi ?
Uamuzi ni wako mimi wangu nawalisha majani hayo ninayolima na yanatosha.Ninachoongeza ni majani ya mikunde,majani ya viazi vitamu hybrid na miti malisho ili kuwaongezea vitamins,madini na protini.
 
Uamuzi ni wako mimi wangu nawalisha majani hayo ninayolima na yanatosha.Ninachoongeza ni majani ya mikunde,majani ya viazi vitamin hybrid na miti malisho ili kuwaongezea vitamins,madini na protini.
Sasa swali lisema hao mbuzi 100 unawalisha heka 1 mwaka mzima ?
 
Uamuzi ni wako mimi wangu nawalisha majani hayo ninayolima na yanatosha.Ninachoongeza ni majani ya mikunde,majani ya viazi vitamin hybrid na miti malisho ili kuwaongezea vitamins,madini na protini.
Miti nayo unapanda ? Au ya porini ?
 
Umepata mbegu mapacha ? Hao ulionao umewanunua wapi.
Nipo ktk fikra ya kuamua niweke ranchi au nilime mazao. Najaribu kutafuta mbuzi wa mapacha walio wanene
Kama unahua alie nai wazuri unujulishe. Shamba lako lipo wapi ?
Shamba lipo Ruvu karibu na Mlandizi-Kibaha.
Mbuzi nafuga Isiolo nililetewa kutoka Kenya.
Mbuzi wanozaa mapacha niliwanununa Mbinga -Ruvuma
Kondoo nafuga Dorper.
Ng'ombe wa maziwa nafuga Friesian.
Ng'ombe wa nyama nafuga Boran.
Utakapokuwa tayari tuwasiliane 0756625286.
 
Sasa swali lisema hao mbuzi 100 unawalisha heka 1 mwaka mzima ?
Ndiyo kila mwezi unavuna majani,mfano tarehe 1 Jan. Unavuna mashina
200,mpaka tarehe 30 Jan. unakuwa umevuna mashina 6000,ukifika shina la 6000,unarudi kuvuna mashina 200 uliyovuna Jan 1.Yanachipua kwa haraka pia yana mchipukizi mengi yanayofika 100 kwenye shina moja.Kwahiyo unakuwa unarudia rudia kuvuna na kama ni mengi unayahifadhi(saileji)
 
Bado najifunza japo umenipa mengi.
Sasa mbuzi 100 wanawezaje kudhiba mashina 200 au kuna suplus food unawaongezea kutoka mashamba mengine ?
Swali langu lililenga uwezo wa kuwalisha mbuzi 100 na kuwatosheleza. Kama ni ranchi maana yake mifugo itategemea hio ardhi tu.
 
Shamba langu lipo mpakani mwa Songea na Njombe. Nimesoma mtandaoni kuwa heka moja inatosha kulisha mbuzi 8. Sasa naona tofauti na maelezo yako kuwa heka 1 mbuzi 100.
Kitu kingine je, ranchi lazima iwe na mabanda au wanalala tu popote. Nimewahi pita kitulo kwenye ng'ombe sijaona mabanda.
Sijawahi ona ranchi ya mbuzi
 
Kimsingi soko lipo Dar es salaam
 
Je mbuzi unawasafiriisha kwa staili gani ?
Je hio mbegu ya mapacha ni nzuri kwenye kuongezeka uzito. Bei za hao wa Songea zipoje.
 
Je mbuzi unawasafiriisha kwa staili gani ?
Je hio mbegu ya mapacha ni nzuri kwenye kuongezeka uzito. Bei za hao wa Songea zipoje.
Kama Kuna mtu unayemfahamu Songea mwambie akutafutie,sipo huko, au subiri niwaulizie watu ninaowafahamu nikipata mawasiliano yao nitakupatia.Bei inategemewa 30,000-70,000 inategemea wakati gani wakati wa mavuno inapanda wakati wa mvua (kifuku)inashuka.
 
Unawasafirisha kwenye gari pickup au Lori.
 
Haya majani ninalima kisasa,ninamwagilia,ninaweka mbolea ya samadi na kiwandani na ninapima afya ya ardhi kwa mwaka mara 2.Ninamwagilia kwa wiki mara 3 ndiyo maana kila baada ya siku 30 ninavuna,mashina mawili tu yanatosha kulisha mbuzi 1 kwa siku. Majani yake ni marefu,mapana na shina moja linafikia machipukizi 100.
Maji ya kumwagilia navuna ya mvua na kisima.
Mbuzi na kondoo wanalala kwenye banda lililojengwa juu, chini kunakuwa na uwazi,mchana wanatoka ng'ombe wanatakiwa waishi kwenye banda.
 

Attachments

  • Screenshot_20231130-093839_1.jpg
    61.1 KB · Views: 49
Majani local Ni sawa eka moja mbuzi 8,hayo hayatunzwi,Mimi yangu namwagilia kwa wiki mara 3,naweka mbolea ya samadi kwa mwaka mara 4,naweka ya kiwandani ya kukuzia kwa mwaka mara 4,napalilia nk.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…