Vitu vya kuzingatia
1.upatikaji wa kutosha wa maji,pamoja na mifumo mizuri ya umwagiliaji Kwa ajili kukuzia shamba malisho
2.mbegu bora za wanyama,wanaoweza kufikia uzito mkubwa na wanaostahimili magomjwa
3.wafanyakazi wenye ujuzi(skilled)na wasio na ujuzi(non skilled(
Wenye ujuzi mfano :madaktari wa wanyama(doctor of veterinary medicine and animal health and production officers)
mafundi sanifu maabara ya wanyama(veterinary laboratory Technologist)
Wataalamu wa shamba malisho(range management officers)
Mhasibu(accountancy) na mtu wa uchumi(economist)
Mwendesha mitambo ya umeme mfano trekta
Mafundi mbalimbali mfano wa umeme,maji,magari na mashine
Wasio na ujuzi mfano:wachunga wanyama,
Walinzi wa Ranchi
Walimaji mashamba
4.Sehemu ya kisasa ya kuchinjia(abbatoir unit) au hata slaughtering slab si mbaya Kwa kuanzia
5.Eneo kubwa la ardhi lenye rutuba ambalo si chini ya ekari 1500
6.Mbegu bora Kwa ajili ya shamba malisho
7.Mpangilio mzuri wa njia pamoja na uzio kuzunguka mashamba malisho
8.Sehemu maalumu ya kuhifadhi wanyama wagonjwa Kwa muda fulani(quarantine area)
9.Sehemu ya kupandishia na kushushia wanyama kwenye Ranchi toka kwenye gari(Loading and unloading area)
10.Sehemu ya kutulizia au kushika wanyama(restraining area) Kwa ajili ya matibabu,uchunguzi au kufanya shughuli ndogo ndogo kama kukata au kupunguza pembe
Yote Kwa yote mambo yapo mengi lakini hayo ndo ya msingi zaidi