Ngongo
Platinum Member
- Sep 20, 2008
- 20,654
- 35,887
Heshima sana wanajamvi,
Nimefuatilia maendeleo ya uongozi mpya wa CHADEMA bado sijaona ubunifu au utofauti wao baina ya uongozi wa zamani na uongozi mpya.
Nimeamua nitachangia lakini kwa sharti moja kubwa iwapo nitaweza kupata uthibitisho Mwenyekiti Lissu amechangia kiasi gani.
Wakati wa kampeni za uchaguzi uliomalizika zilikuwepo tuhuma nzito kwamba Lissu hana msukumo wa kuchangia chama.Katika uchaguzi huo Lissu aliwekewa kiwango cha kuchangia chama kiasi cha Tsh 30 Million hakutoa ndururu.
Wakati akiwa Mbunge ulikuwepo utaratibu wa wabunge kuchangia chama Lissu hakuwa akitoa hata cent tano.
Lissu sasa ni Mwenyekiti wa chama ni vyema na haki ikiwa ataonyesha mfano mzuri wa kuchangia chama si kuwataka watu wengine wachangie wakati yeye binafsi hataki kuchangia.
Ngongo kwasasa Mikocheni.