Nalazimika kuwa adui wa rafiki wa rafiki yangu

Nalazimika kuwa adui wa rafiki wa rafiki yangu

Curtis De Mi Amor

Senior Member
Joined
Jan 9, 2022
Posts
136
Reaction score
514
Iko hivi, nina mshkaji wangu peace sana tunaelewana mtu wa kazi kazi.

Nayeye ana mshkaji wake sasa ilitokea wakagombana kisa mikopo maana mwana alienda kopa na mwana ndio alimdhamini. Sasa kwenye marejesho mwana kala chocho, hivyo msala ikabidi mshkaji ausolve ukaisha. Ghafla mwamba huyu hapa katimba, wakatemeana mbovu mixer kushikana mashati.

Kesi ikatimba kwa mapai jamaa akatoka kwa dhamana, kwanzia hapo ni paka na mbwa hawaelewani wala kusemeshana. Sasa majuzi nilikaa na mshkaji tunapiga stori za hapa na pale si rafiki yangu kaninunia kisa nimepiga stori na adui.

Sasa cjui kama mimi ndio nina kosa au yeye ndo mwenye kosa. Ila ukikutana na hali kama hiyo unaisolve vipi haswa mkikuta wote watatu ni marafiki na imetokoa wawili kati yenu hawaelewani?
 
Mwambie huyo shosti yako anayekununia kuwa huyo jamaa uliekuwa unaongea nae, ulikuwa unaongea nae kama mpita njia tu, Ushoga wako nayeye haujarudi bado..kwahyo asikususie maana hauna kosa
 
Hizi mambo hutokea kwa wanawake na wavulana,, nunianeni
 
Miafrika ni bure,ukimudhamini MTU maana yake umemwamini na chochote kitakachojitokeza rafikiyo akashindwa basi utachukua majukumu hayo.alidhani kumdhamini MTU ni kuweka sahihi na kuondoka.
 
Wanaume na nyie hua mnanuniana kumbe
 
Wewe ndiyo inabd ukae nao uwasuluhishe, huo sio uanaume kabisa, huo hatununuani sisi!
 
Rafiki yako yupo sawa kununa kwasababu wewe utakuwa mpeleka habari za huku na kule. Najua unajaribu kuwa neutral lakini ikiwa huyo jamaa kamzingua rafiki yake kwa hela hivi atakuwacha wewe?? a snitch nigga, that's that shit I don't like
 
Back
Top Bottom