Nalazimishwa Kutofanya Mapenzi Bila Kupenda!

Nalazimishwa Kutofanya Mapenzi Bila Kupenda!

Alfred

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2008
Posts
2,093
Reaction score
2,843
Ilikuwa February 2011 nilipopigiwa simu kupitia mwl. Wa Bweni letu wakati huo nipo kidato cha tatu.. Nikasikia sauti ya mama ikiniambia Sulle..(Jina langu la Nyumbani) Babu anakuita (Mara ya Mwisho Nilionana nae 2008).. akaniambia toka mwaka jana mwishoni babu amekuwa akiumwa mara kwa mara anataka uje umjulie hali.. (Kweli hata miaka miwili nyuma babu alisihi sana nimtembelee ila shule ilinibana kidogo).. Kwa kuwa Babu alikuwa rafiki yangu Mkubwa toka utotoni sema baada ya kumaliza darasa la 7 sikuenda kijijini kwa Babu tena.. Nikapanga Safari ya kwenda Kwa Babu!

Siku ya siku asubuhi yenye Baridi Kali nakumbuka nilipanda Gari toka Pale Moshi mtaa wa Magereza nikielekea kwa Babu yangu Kijijini Mama Isara (Mbulu).. Nilifika kwa babu nilipokelewa kwa furaha sana na Babu akafurahi sana..

Asubuhi yake Babu alikuwa na nafuu kidogo tukapiga story nyingi sana, babu akiniambia sasa nimekuwa Mwanaume.. Ninaweza kumtamani mwanamke na hata kufanya nae Mapenzi.. tukacheka kidogo.. Kisha babu akaniambia Sulle.. huwa unapata Maumivu ya Kichwa.. nikamjibu ndiyo..akauliza tena.. je maumivu juu ya kiuno nikamjibu ndio.. akasema tena je mgongoni karibu na Mabega nikamjibu ndio.. na ni kweli kabisa babu hakuwa akikosea..hayo maumivu huwa nayapata na yanakuwa makali sana.. japo hudumu kwa dakika kama 5 tu na kwa mwezi huja kama mara 3 tu..

Kisha babu akaniambia kuna ndoto ya namna hii huwa unaota mara kwa mara na huwa inakutia hofu sana.. (na kweli huwa naota ndoto ya hivyo).. Kisha Babu akaniambia Mjukuu wangu Sulle ulivomaliza shule ya msingi kuna vitu umepandikiziwa katika mwili wako..nikashangaa inawezekanaje..akaniambia ulitakiwa ufe siku nyingi au katika masomo yako ushindwe siku nyingi ila kitendo cha wewe kutokuja kijijini mara kwa mara kimekusaidia na Mungu wako amekupigania..

Babu akazidi kuniambia kuwa kuna vitu vyako pia vimechukuliwa.. Nikazidi kuduwaa.. Babu akaniambia nivue tshirt yangu (Nakumbuka nilivaa tshirt ilikuwa imeandikwa HIP-HOP) nikampa.. Babu akaweka ile tshirt kwenye kidude flani kisha akalala chini akajifunika.. baada ya dk kumi akaamka akaniambia nimletee kile kidude nillichowekea tshirt..tukakuta kuna kimalboro cheusi kimefungwa mithili ya mpira mdogo.. babu akanyunyizia dawa flani mle.. kisha akafunua..tulikuta kipisi cha sh 1000, kinyesi ambacho ni old(yeye ndio alikuwa anaweza kutambua).. kisha tukakuta nywele, jiwe, kucha, karatasi, na kalamu pia na mkaa (Wataalamu walioko Humu watasaidia Kutafsiri vina maana gani)!



Kisha Babu akaniita ndani akaniambia kanunue wembe nikaenda.. kurudi akaniambia nikae kwenye Kigoda kisha akachukua kitu kama mkia wa Ng’ombe akanizungushiwa kichwani mara tatu, kiunoni mara tatu na Miguuni mara tatu, Kisha akaanza kunichana sehemu ambazo zilikuwa zinaniuma.. Babu akaweka anaweka kitu mithili ya Pembe.. baada ya dk 5 nikaanza kuhisi kama kuna vitu vinavutwa... babu akaja akatoa zile Pembe.. akaanza kunionyesha.. Aisee inatishaa alitoa vitu kama vipisi vya Mifupa kwenye Mwili wangu (Mpaka leo sijawahi kuumwa tena).. Nilishangaa na Kutishika sana huku Babu yeye akionekana yupo kawaida tu..



Baada ya Hapo Babu akaanza Kuniambia.. Mjukuu wangu Sulle Katika Safari yako ya Mafanikio Adui yako Mkubwa ni Mwanamke yaani NGONO, Akasema Wabaya wako au mtu atakayetokea kuwa mbaya wako hatokuweza isipokuwa kwa njia ya Mwanamke.. akanisihi sana kuwa makini na wanawake.. sio kila mwanamke unafanya nae Ngono..

Babu akavuta Pumzi akionekana kuniambia jambo la Muhimu Zaidi.. Akasema Sulle kuna wanawake wazuri sana duniani wa kila Rangi, lakini wewe Mjukuu wangu Kamwe usiwe na Mwanamke Mweusi, Mwanamke Mweusi hajaumbwa kwa ajili yako, Kamwe Mambo yako hayataenda utakavyo ukiwa na Mwanamke mweusi.. ukiweza Oa Mwanamke Mweupe.. itakuwa vizuri Zaidi… Babu Akaishia Hapo..

Baada ya kukaa kwa Babu wiki Moja, nikarudi shule Bahati Mbaya baada ya siku mbili toka nifike shule napigiwa simu kuwa Babu Amefariki, Roho iliniuma sana huku nikikumbuka Nasaha zake (Pumzika kwa Amani Babu Yangu).



Kwanini Naandika Uzi Huu?

Leo asubuhi nilichelewa kuamka kidogo, nilikuta Missed call kama 5 za Namba geni kwenye simu Yangu.. nikapiga na kusikia sauti ya Mwanamume ikiniambia Haujambo Sulle (Nikagundua alikuwa Mdogo wake Babu yangu), kwa bashasha tele nikamuitikia na kukumbushana kidogo enzi tukichunga wote Ng;ombe zake.. akaniambia Mjukuu wangu umeadimika sana, Pole kwanza na Masomo yako..



Kisha akaniambia Naona kama kuna wanawake wanajirahisi sana kwako (Na ni kweli kama hii wikiendi wanawake kama 5 hivi wanataka niwagegede, na nilishashawishika), akaniambia kuwa Makini utaharibiwa (Kijadi sisi tunaamini Mwanamke kupitia Ngono anaweza kuharibu Nyota ya Mwanaume).. Nilistuka Kidogo, kisha akasisitiza sana kuwa Makini na kwa kautani akasema Kuliko ugegede piga hata nyeto!



Kweli Nilijikuta Moyoni Namshukuru sana,

Wanaume Wenzangu tuwe Makini, Magonjwa tutazuia kwa Condom ila Je Spirit na zile nguvu za Giza na Mapepo zilizopo kwenye Ngono tutazuia na nini?

ila wanaJF nimejikuta nawaza Hii si kulazimishana useja jamani? Yaani Nisigegedane? Sometimes naona wazee wanatubania tu kwa Mila zao..



Karibuni!



ALFRED
 
Bado unaamini mambo ya giza namna hiyo, utaendelea kuwa mtumwa hadi lini, unaishi kwa kuongozwa na watu pembeni amka kijana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha kuwa mtumwa wa Shetani n usipende Sana kukumbatia mambo ya uchawi n uganga vitapoteza furaha n Amani yako Anaejua siku yako y kufa n Muumba wako tu wengine wanajivika utabiri ili akikupiga mziga usiache kumpa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha kuwa mtumwa wa Shetani n usipende Sana kukumbatia mambo ya uchawi n uganga vitapoteza furaha n Amani yako Anaejua siku yako y kufa n Muumba wako tu wengine wanajivika utabiri ili akikupiga mziga usiache kumpa

Sent using Jamii Forums mobile app
Alikuwa Babu yangu Mkuu hata Pesa hakuwa akihitaji!
 
Don't let such things dictate your life.

Do you hommie, you decide how you wanna live it!
 
Back
Top Bottom