Nalia na gazeti la zamani Sanifu, Sani, Tabasamu, By Kingo, Bongo na kadhalika, kwani ni matajiri katika ulimwengu wa sasa wa katuni

Kizazi cha dhahabu kimeshapita, sasa hivi kipo kizazi kipya ambacho kimepoteza ubunifu
 
UNAMSAHAU SOKOMOKO
 
Walipo kwa sasa baadhi ya wahusika wa gazeti la Sani na Bongo.
Sokomoko ni mgonjwa wa ini sababu ya unywaji Sana wa pombe Yuko kwao kigogo,
Ndulakuwili alipigwa nusu kufa kwa Tabia zake za wizi na utapeli kariakoo sasa hivi anabeba mizigo mabibo sokoni.

Kipepe na Njomba Nchumali walinusurika kuliwa na simba na baada ya Hilo tukio wakasitisha shughuli za uwindaji na sasa ni wakulima.

Lodi lofa baada ya kuwa na majibu mabaya kwa watu na kwa traffic alishindwa kulipa mkopo wa gari hivyo alinyang'anywa na sasa hivi ni dereva wa gari za serikali, mdomo wake mchafu umeisha [emoji28]

Pimbi hajawai kuwa na bahati, katika kupata wanawake ambapo mara ya mwisho kafanyiwa fumanizi hotel ya legacy Sinza Akala kipigo na sasa hamna mkono mmoja, [emoji28]

Madengee alikataa shule babake akamfukuza nyumbani sasa hivi ni fundi masofa pale keko, [emoji28]

Zena na Betina wako segerea sababu ya ugomvi wap toka kipindi kile.
Mapung'o Golden Boy, baada ya team aliyokuwa anachezea mbeya kushuka daraja aliamua kuacha mpira na kurudi kwao kimbiji kuwa mvuvi.[emoji1787]
 
Ni ngumu mno nimepite bila kucoment kwenye huu uzi aisee raha ya zile katuni asikwambie mtu tu tu katuni tamu.
Mazoezi ya zile timu born town na bush stars hayakuwa ya sayari hii na vile vimaneno vyao vya kutukanana wanspokabana uwanjani acheni tu..
Kifupi jama walijua kuchora, walijua kutunga hadithi, walijua kuchekesha
The way walivyokuwa wanawachora wale wanawake mhh
Ngoja niishie hapa tu ahsante mdau kwa kuturudishia memory yale majarida yameniathiri mpaka leo napenda catoon sana nikinunua gazeti naanza kusoma katuni kwanza stori zingine baadae au nafunga na gazeti kabisa
 
Hahahah nimecheka mbaya daah hili gazeti nalikumbuka sana
 
Dah Msako wa Mr X sijaumalizaga ila jamaa walikua noma sana
 
Dennis Raymond Makete
 
Hahah ila Kapteni Mapungo alikuwa na mikwara sana Aisee

Mie nakumbuka tu yale mazoezi yao huku wamejifunga mawe miguuni.

Kilichokuwa kinanifurahisha ni yale maneno yake akiwa uwanjani ubabe juu ya ubabe.

Ukweli kuna vitu tunavimiss.
Mapungo alikuwa akionewa sana na Bob Mikwara
 
Mapungo mbona mara ya mwisho alienda kusajiliwa Arsenal, aliunganishwa na Nwanko Kanu
 
Mzee meko alienda dar kununua trekta akakutana na bob mazishi akamtafutia pisi kali ikawa ni bata kila siku mpaka pesa zikaisha akawa hoe hae
 
Hapa born town pale bush stars
bonge la mechi kuliko simba na yanga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…