Fortunatus Buyobe
JF-Expert Member
- Nov 9, 2011
- 463
- 1,127
Tarehe 9 mwezi wa pili mwaka 2020 Rais wa Afrika kusini Cyril Ramaphosa alikuwa mkutanoni Jijini Adis Ababa Ethiopia.
Huko nyuma nchini kwake katika shamba lake la wanyamapori la PHALA PHALA lililopo Jimbo la Limpompo linatokea tukio la kuvunja na kuiba.
Mfanyakazi wa ndani wa Rais pale shambani alishtuka kuona pesa in tune of 4 million US dollars katika kabati la Rais.
Mfanyakazi huyu aitwaye FLORIANA ambaye ni Mnamibia akampigia kaka yake simu kumjuza juu ya ugunduzi wake.
Akamtumia na picha pesa ziliko
Kaka yake alikuwa ni Nyamela mwenye mahusiano na Wakora kibao ndani ya jiji la Cape Town.
Naye baada ya “kuhack mchongo” akawauzia ramani ya Vita Wakora wenzake.
Kaka huyu kwa kushirikiana na wenzake waliokoko Cape Town wakaandaa mchoro wa kufata kitita kile.
Kweli wakavamia na kuibuka na mzigo wote.
Rais Zuma alipojulishwa juu ya hilo akawatuma walinzi wake wafatilie swala hilo.
Walinzi wale walishirikiana na timu ya makachero kutoka jeshi la polisi.
Walinzi wale wakatizama footages za Closed Circuit Television (CCTV)
Wakaona watu wanne wakikata security perimeter wire kisha wawili kati yao wakitambaa kwa magoti kwenda dirishani kwenye chumba cha Rais
Wawili kati yao wakabaki mlangoni.
CCTV iliwaonyesha hadi wanapochukua pesa na kuondoka.
Katika upelelezi wakagundua manyamela wawili ni wanamibia na wa wawili ni waafrika kusini.
Uraia wa namibia ukamweka karibu mfanyakazi wa ndani wa rais na sakata hilo.
Upelelezi ukaendelea na Ikabainika manyamela hao walifanya miamala mikubwa baada ya tukio hilo
Feb 14 2020 Mmoja aliyeitwa Mukekeni alinunua Ford Ranger 2.0 TDCi Wild track 4X4 ya mwaka 2019
Feb 15 na 16 2020 Mr. Shikongo alihamishia Rands 175,000 katika benki ya FNB
Feb 19 2020 Mr. Shaunmbwako akanunua na kusajili gari aina ya Volkswagen GTI
June 12 Mr David alikamatwa namibia akiwa na saa za kisasa za Rolex na TAG Hauer pamoja na noti 11 za US Dollar 100 kila moja.
Manyamela hawa walikamatwa kimya kimya na kuhojiwa na team ya walinzi wa rais.
Inasemwa walitembezewa kichapo cha kufa mtu kama fundisho
Lakini baadae👇
Rais alijua swala hili litaibua scandal kwa kiasi kikubwa cha pesa kukutwa shambani kwake.
Bado alikuwa akikumbuka jinsi shamba lake la zaidi ya ekari 11 lilivyokuwa likihusishwa na uwindaji haramu wa Vipusa vya tembo.
Akaamua kuwafunga mdomo wezi wake.
Mfanyakazi wake wa ndani alipewa Us Dollar 10,000 ili kutoongelea swala lile popote na akahamishwa shambani.
Wezi wengine nao “wakapozwa ili kuzima scandal ile.
Wakapewa Rands 50,000 cash
Lakini, hakuna siri ya zaidi ya mtu mmoja.
Siri hii ilidumu kwa miaka miwili pekee!
Tarehe 3 Mwezi huu na mwaka huu, Mkuu wa idara ya Ujasusi mstaafu ARTHUR FRASER aliitikisa Afrika kusini baada ya kuibua sakata hili mbele ya waandishi wa habari.
Kachero huyu alimtuhumu rais Ramaphosa kwa makosa ya Utekaji, ukwepaji kodi ,utakatishaji fedha na rushwa wakati akipeleleza swala hili.
Kachero huyu alitoa vielelezo vyote mbele ya wanahabari ikiwemo taarifa za kibenki na CCTV footages.
Kachero huyu akadai ameshasajili tuhuma hizi polisi ambao nao walidai wameanza kuchunguza sakata hilo.
Msemaji wa rais aliibuka na kujibu kuwa ni kweli kulikuwa na tukio la wizi wa pesa zilizotokana na mauzo ya wanyama pori.
Kadai kiasi kilichoibiwa ni kidogo kuliko kinachotajwa na rais hausiki na lolote kwani wakati wa tukio rais hakuwa nchini.
Utetezi huu ni kama uliwasha moto kwenye nyika ya waafrika kusini ambao tayari nao wamejiunga na “orchestra” ya kupigia kelele swala hili.
Ramaphosa alishawahi kujinadi huko nyuma kuwa tuhuza za rushwa kama ya mtangulizi wake Zuma zitakuwa za mwisho ndani ya chama cha ANC
Kiongozi wa chama cha Upinzani South Africa Julius Malema hakutaka swala hili limpite kando.
Tayari ameibuka na kusema wataitisha kura ya maoni ya kutokuwa na imani na rais kama walivyofanya kwa Jacob Zuma.
Bunge linatarajiwa kujadili sakata hilo.