Nalipongeza jeshi la polisi mkoa mjini magharibi Unguja.

Nalipongeza jeshi la polisi mkoa mjini magharibi Unguja.

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
8,734
Reaction score
5,750
Natoa pongezi kwa RPC wa mkoa mjini magharibi unguja kwa kufanya kazi kwa weledi na kumfukuza kazi askari ambaye alimkamata mtuhumiwa na kumpeleka kwa wananchi wenye hasira na kisha kumuua mtuhumiwa.
Imekuwa ni tabia mbaya sana wananchi wamekuwa wanachukua sheria mkononi na kuua watuhumiwa bila kufuata sheria na taratibu za nchi.
Hili ni fundisho pia hata kwa askari na watendaji wa kata ambao wamekuwa wakikiuka maadili ya kazi na kuruhusu watuhumiwa kupigwa na kuteswa wakiwa mikononi mwao kwa kisingizio tumechoshwa na wezi au vibaka
Mwizi au kibaka akikamatwa anatakiwa ashughulikiwe kwa misingi ya sheria kama alivyosema RPC Awadh.
Huu ni mfano mzuri kwa wananchi waelewe kuwa nchi inaendeshwa kwa kufuata misingi ya sheria.
Kujichukulia sheria mikononi ni moja ya mambo ambayo yamekuwa na madhara makubwa katika jamii kwa sababu baadhi ya watuhumiwa hufariki na kuacha yatima. Wananchi watambue mahakama ndio chombo pekee cha kumtia hatiani mtuhumiwa.
Mfano ni tukio lililotokea hivi karibuni huko kasulu kigoma ambapo watu walichukulia sheria mkononi na kuua wanafamilia wanne kwa kuwachoma moto.
Huko Mwanza tar 26/10/2019 Mwanajeshi na Migambo waliwatesa watuhumiwa ndani ya ofisi ya mtendaji wa kata ya kahama wilaya ya ilemela bahati mbaya mtuhumiwa mmoja alifariki.
Matukio kama haya ni kinyume na misingi ya haki za binadamu.
 
Back
Top Bottom