Namaingo na mkakati wa kuunga mkono jitihada za Serikali kuboresha kilimo

JAMHURI

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2010
Posts
449
Reaction score
60
Namaingo na mkakati wa kuunga mkono jitihada za Serikali kuboresha kilimo.

Na, MOHAMED HAMAD-DAR ES SALAAM

Serikali na mashirika ya umma hapa nchini, wamekuwa na mikakati mbalimbali ya kuboresha sekta ya kilimo ili wakulima waweze kunufaika na sekta hiyo.

Kilimo kimeajiri zaidi ya asilimia 80% ya watanzania, hivyo kwa kuona umuhimu wa sekta hii jitihada mbalimbali zimekuwa zikifanyika kuhakikisha zinawakomboa kuondokana na umaskini wa kipato.

Kampuni ya Namaingo Bussines agency ltd, yenye makao yake makuu jijini Dar es Salaam, ambayo ilisajiliwa mwaka 2012, imeunga mkono jitihada za Serikali kutumia fursa ya ardhi kufanya mambo matano kuwakwamua wananchi na umaskini wa kipato.

Mkurugenzi mtendaji, Biubwa Ibrahim akiwa kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa kampuni hiyo Jijini Dar es Salaam, alitaja maeneo matano waatakayounga mkono jitihada za Serikali kwa wananchi kuwa ni kumiliki wa ardhi kisheria, kuwapa elimu ya kiuchumi, kusimamia upatikanaji wa mitaji, masoko na kuwawezesha wananchi kupata makazi bora.

Katika kipindi cha uhai wa kampuni hiyo, Mkurugenzi huyo ametembea mikoa 19 ya Tanzania kuongea na wananchi zaidi ya laki nne na kuwapa elimu ya ujasiriamali, ambapo waliweza kujiunga kwa pamoja na kuanzisha miradi mbalimbali ikiwemo kilimo cha kibiashara, ufugaji wa nyuki wa asali, na hata ufugaji wa mifugo aina ya sungura.

Alisema toka apate ufahamu akiwa mdogo alitamani kuona watu wakibadilika kimaendeleo…akidai hata yeye aliweza kubadilika kwa kuamua kubadilika ingawa alitoa katika familia duni ambayo ilikuwa inamiliki ardhi kisheria ambayo ndiyo iliyochangia mafanikio makubwa aliyonayo.

Kuhusu suala la umaskini mkurugenzi huyo alisema, nchi kama Tanzania yenye ardhi na misitu ya kutosha sambamba na amani kwa watu wake, kuna uwezekano mkubwa wa kubadilisha maisha ya watu na kuwa matajiri wakupindukia.

“Tusikatae kuwa tuna wajibu wa kufanya mabadiliko wenyewe, baadhi ya maeneo hapa nchini wakitaja suala la umaskini mimi nashangaa.. wanafikiri kuwa ni maskini kumbe sio maskini.. ndugu zangu umaskini unakaa kwenye ubongo na unaweza kuondolewa haya kwa kukemea” alisema Mkurugenzi Biubwa.

Aliwaambia wanachama hao kuwa hali aliyonayo, alianza na biashara ya hafkeki na juice mwaka 1999 na baada ya miaka nane aliweza kuwa na milioni mia mbili kutokana na kufanya maamuzi ya kutaka kuwa tajiri.

Alisema umaskini ni dhabi itakayo waingiza watu motoni, kwani uchumi ukiwa mbovu wakifa wataacha kizazi chenye mashaka na watakapokufa pepo kwako itakuwa ni ndoto, hivyo juhudi za maksudi zinahitajika kupiga vita shetani ili kuuona ufalme wa mbinguni.

“Ndoto yangu ni kuunganisha watu pamoja na kutafuta na ridhaa ya Mwenyezi Mungu kwani wingi wetu.. Mwenyezi Mungu atakuwa pamoja nasi, hivyo nawasii wanachama kuwa na mshikamano kwa sababu umaskini ni mnyama na mdudu ambao anaweza kutolewa kwa nguvu za watu wengi na hata kuzomea” alisema Mkurugenzi huyo.

Aliomba Serikali kuunga mkono jitihada za kampuni hiyo ambayo imehusisha makundi mbalimbali ya watu wenye nyazifa tofauti ndani ya nchi ili wawe sehemu sahihi ya kutuliza nyoyo na joto baada ya kustaafu kwani kuna jukumu la kuwalea na kuwatia moyo katika maisha yao.

Mhe Amina Mollel mbunge viti maalumu, alikuwa mgeni rasmi katika mkutano huo wa wanachama katika hatua hiyo aliwapongeza kwa kufanya maamuzi ya kuunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya tano kuwa pamoja na kufanya kazi kwa kutumia fursa mbalimbali zilizopo katika maeneo yao.

“Tajiri mmoja aliwahi kusema, ukijilaumu kuzaliwa katika familia maskini, wewe ndio chanzo cha tatizo…unapaswa kujitambua kwa kutumia fursa hiyo kuondokana na umaskini, vijana wengi wanategemea ndugu, eti yuko baba, shangazi, na mama..ndugu yangu utajiri utauleta kwa mikono yako mwenyewe” alisema Mhe Mollel.

Alisema kwa mujibu wa kampuni hiyo kuna elimu ya ujasiria mali inayotolewa kwa wanachama, akidai Serikali ya awamu ya tano ya Dr. John Pombe Magufuli, ndio inayo wahitaji watu kama hao walioungana pamoja kuendeleza Tanzania ya Viwanda.

Aliwataka wanachama hao kutumia fursa waliyonayo ya kumpata Mkurugenzi huyo ambaye ana karama ya kuwatoa watu katika umaskini wa kipato na kuwafanya matajiri huku akiwaasa kutofikiri utajiri wa haraka kwani mwishilio wake ni kuishia magereza ya Ukonga, Segerea na Keko.

Mratibu wa Kampuni hiyo mkoa wa Lindi, Abdala Saidi Mwambiko, alisema katika ukanda wao wamejipanga kutekeleza miradi ya wananchi na sio maneno kwani Serikali ya awamu ya tano inahitaji vitendo ili watu waondokane na umaskini wa kipato.

Mkuu wa kitengo cha mawasiliano ya kapuni hiyo Jijini Dar es Salaam, Yusus Aboud alisema,Kampuni imejipanga upya kwa kuunda kamati za kusimamia miradi ya wanachama kila mkoa ili kuleta tija katika miradi hiyo.

Mipango huenda sambamba na usimamizi hivyo tumejipanga upya sambamba na malengo ya Serikali hii ambayo inataka wananchi kufanya kazi zenye tija kwao na kwa Taifa kwa ujumla.

Kwa upande wa viongozi wa dini akiwemo shekh wa wilaya ya Ubungo, Maulidi Kidebe, alisisitiza wananchi kuwa tayari kuelimishwa watapata mafanikio ya kupata mali ambayo italeta mali na ufaume, huku Mchungaji Jackob Mwakibinga akiwataka wanachama hao kutambua kuwa bado wana muda wa kufanya mabadiliko ya maisha yao.

Mwisho

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Attachments

  • IMG-20190106-WA0105.jpg
    IMG-20190106-WA0105.jpg
    46.4 KB · Views: 31
  • IMG-20190106-WA0106.jpg
    IMG-20190106-WA0106.jpg
    68 KB · Views: 31
  • IMG-20190106-WA0095.jpg
    IMG-20190106-WA0095.jpg
    56.2 KB · Views: 30
  • IMG-20190106-WA0096.jpg
    IMG-20190106-WA0096.jpg
    54.7 KB · Views: 28
  • IMG-20190106-WA0102.jpg
    IMG-20190106-WA0102.jpg
    65.7 KB · Views: 27

Washenzi hawa
 
MATAPELI...NA WEWE BOYA WALIYEKUTUMA HUMU TAFADHALI PIGA KIMYA MANAKE WATU TUNA HASIRA NA HELA ZETU MLIZOTUTAPELI...IKO SIKU MTAZIKUNYA..
 
Hao ni matapeli wakubwa mnoo wametapeli watu huku kyela na kutokea kusiko julikana... Wanaboa ahadi za kitoto sanaa.. sijui oh utafuga nyuki ama utalima...

Hivyo utaletewa mtaalam huyo mtalaama atakua anasimamia shughuli zako zote... Utafunguliwa account bank... Baada ya mazo kuvunwa watachukua hayo mazao wao namaengo then wakiuza watakuingizia pesa kwenye account yako...

Haya changeni pesa... Baada ya hapo wanatokomea... Watakuuzieni t-shirt n.k

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kilimo kimevamiwa. Siku hizi watu wanafanya kilimo offisini. Na unakuta mtu mzima anaenda ofisini akikuta viti, komputa na ac bac anawaamini watu kama hawa. Wanachofanya hasa ni kukuonesha picha za kudownload.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom