namaliza chuo kikuu naenda mtaani hebu niambieni kukoje huko kibiashara?

Julius Husseni

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2016
Posts
1,435
Reaction score
1,192
Nakaribia kumaliza chuo Nina mtaji wa laki 8 sijui nikaziweke wapi hizi pesa kibiashara! Lengo La kwanza ni kwenda kuuza bidhaa ndogondogo za urembo..

Option ya pili nikainunue salon ya kiume Kuna jamaa nasikia anauza hiyo kitu.

Hapa nilipo nina huo ujuzi Sasa wakuu kabla sijaingia kichwa kichwa hizi pesa nisije jutia badae Naombeni wakuu nisaidieni mawazo hapa.

Chondechonde wakuu nisaidieni mawazo chanya msije nitia mchanga wa uso nikaona giza mbeleni. Asanteni!
 
Acha woga....Kwan umesoma kozi gan
 
Karibu sana kaka uraiani, kwa ufupi hakuna jipya mji upo, watu wapo, kikubwa ni kujiongeza na kujitafutia riziki za halali
 
Hyo saluni uliambiwa inauzwa pesa ngapi?
Labda tuanzie hapo
 
Kijana honestly , mambo yamebadirika sana. Mambo mtaani ni magumu.


Mimi nakushauri Fanya jambo lolote litakalokupa Pesa halali. Usichague kazi kwasababu una degree. Elimu yako weka pembeni. Usiangalie Ndugu,majirani na marafiki watakuonaje.


Kama ukiishi kwa hiyo energy utaenda kwenye graduation wanafunzi wenzako wanataka uwape madili.
 
Asante mkuu nimekuelewa Sana
 
Laki nane ?
Njoo kitaa ufungue goli la chipsi jirani na kijiwe cha dada Poa utatoboa ila ukija mtaani na ubishoo wa chuo hivyo vihela havimalizi hata week.
Pia kama unapaka poda jihadhari kuna kifiro.!
 
Hiyo saluni ni choice nzuri lakini ni lazima utathmini ipo location gani yaani Kuna mzunguko wa watu wengi au kijijini ambako watu wananyoana kwa viwembe chini ya mti
Ngoja nikapacheki nikirudi kule sait
 
Laki nane ?
Njoo kitaa ufungue goli la chipsi jirani na kijiwe cha dada Poa utatoboa ila ukija mtaani na ubishoo wa chuo hivyo vihela havimalizi hata week.
Pia kama unapaka poda jihadhari kuna kifiro.!
Aah mkuu Habari za chips Sina uzoefu nazo hata kidogo sijui naanzia wapi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…