Zanzibar 2020 Namba 27: Pereira Ame Silima amechukua fomu ya kugombea Urais Zanzibar kupita CCM

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Mapema asubuhi ya leo kada mwengine wa CCM ndugu Pereira Ame Silima amejitokeza katika ofisi kuu za Chama cha Mapinduzi Kisiwandui na kuchukua fomu Idadi ya wagombea wa kuteuliwa kugombea urais Zanzibar kupiti tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM wamefikia wagombea 27

EbV6r_qWsAAU_Os.jpg

Mfahamu Kiundani
Pereira Ame Silima (PAS) ni mmoja ya makada wa CCM katika orodha ya watu zaidi ya 10 ambao mpaka sasa wametajwa kuwa na nia ya kuipata nafasi ya kuteuliwa na CCM kugombea Urais Zanzibar mwaka huu. Kihistoria PAS kazaliwa Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja tarehe 14 Machi mwaka 1959 na Machi 14 mwaka huu alikata keki na kufanya dua ya kutimiza umri wa miaka 61.

PAS kakulia Unguja ambako ndiko alikosoma na kuhitimu elimu yake ya Kidato cha Nne na kisha kusomea na kupata Stashahada (Diploma) katika mambo ya misitu.Baada ya masomo yake aliajiriwa SMZ kwa nafasi za chini kabla ya kupanda hadi kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo na baadae Wizara ya Biashara, Utalii na Masoko Zanzibar.

Mwaka 2010 aliamua kujitosa katika siasa na kufanikiwa kuchaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Chumbuni kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na akiwa katika nafasi hiyo akateuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani (2010 - 2015).

Awamu ya uchaguzi iliyofuatia yani 2015 wana Chumbuni wakamkataa kuendelee kuwa Mbunge wao hivyo akatupwa nje ya siasa za uwakilishi wa wananchi. Moja ya sababu za kukataliwa na wananchi zinatajwa kuwa ni kushindwa kwake kushughulikia matatizo ya watu wake jimboni na dharau kwa wapiga kura wake ambao kimsingi ndio mabosi zake.

Baada ya anguko hilo, PAS akakaa nje ya ulingo wa siasa na ilipofika mwaka 2017 akateuliwa kuwa Katibu wa Oganaizesheni wa CCM nafasi anayoendelea nayo hadi leo. Kwa tabia PAS ni mtu mkimya na mtaratibu asiyependa kuzungumza sana, sifa nzuri kwa watendaji wa taasisi lakini mbaya kwa kuongoza wananchi. Huenda hii inaelezea kwa nini chama chake kilimpa kazi ya Ukatibu wa Oganaizesheni (taasisi) baada ya kushindwa Ubunge (kazi ya wananchi).

Mbali na ukimya wake, PAS ana mapungufu mbalimbali. Mfano akiwa Katibu Mkuu Kilimo kwa kutumia madaraka yake alijimilikisha eneo ambalo ni moja katika viwanja vya wizara ya kilimo vilivyopo Mazizini bila kufuata taratibu na sheria na baadaye kutumia kiwanja hicho kujenga nyumba yake ya kifahari. Nyumba ndio makazi yake toka ilipokamilika hadi sasa.

PAS pia ana tuhuma za kujimilikisha mashamba ya serikali ya mikarafuu Mtambwe Pemba, Cheju, Selem, Kizimbani, Mwachalale na maeneo ya Mahonda, ardhi ambayo wananchi wanasema kama serikali iliona haitaki tena kuimiliki basi wangepewa wananchi masikini kuendesha shughuli za kilimo na nyenginezo.

Kashfa nyingine inayomuandama PAS ni ile kituko cha yeye na kaka yake (yeye akiwa Katibu Mkuu Biashara na Utalii kaka yake Mussa Ame Silima akiwa Waziri katika Wizara hiyo) kujinufaisha kama familia na kutumia ofisi ya umma na madaraka yao kujipatia maeneo ya fukwe Nungwi na Matemwe ambako wamejenga mahoteli wakiwa ubia kisiri na watu mbalimbali. Mussa Ame Silima kwa sasa ndiye Mwenyekiti wa Wazazi CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Watu wakimya wana mambo walisema wahenga, katika hili, PAS kaonyesha kweli kwani amewahi kuwa katika ugomvi mkubwa na aliyekuwa Waziri wa Fedha SMZ wakati huo Omar Ali Yussuf kwa wawili hao kuweka “heshima” zao mfukoni na kugombania mmoja katika makada wa Umoja wa Vijana wakati huo aliyeitwa Bi Nadra.

Nadra huyu si haba, ni mmoja katika wanawake ambae ameshagombanisha watu wengi Zanzibar, Dodoma na Dar es Salaam na ni maarufu wa kuchanganya wanaume. Zipo taarifa kwamba hivi sasa Nadra ndiye mama watoto wa PAS.

Wataalamu wa siasa za Zanzibar wanasema kitendo cha PAS kutaka kuchukua fomu ya Urais Zanzibar kinaweza kuwa na lengo la kujilinda asitupwe. Hiyo inadadavuliwa kuwa kwa sababu sasa uwezo wake katika CCM una dosari na haoneshi kuimudu nafasi yake kama Katibu wa Oganaizesheni na kuna dalili ya kuondolewa nafasi hiyo mda wowote PAS anatafuta pa kutokea kwamba walau atakumbukwa kuwa aliwahi kutangaza nia na labda atapata uteuzi wa namna fulani. Inasemekana anapanga kuchukua fomu kisha kumuunga mkono mgombea atakayepita ili amlipe fadhila. Wananchi wengi wa Zanzibar na wachambuzi wa siasa wanamuona PAS kama mtu asiye na nafasi yoyote ndani ya mbio za Urais wa Zanzibar 2020.

Bado wa wagombea wawili watakaochukua fomu kupitia CCM ili wafike 30 nijishindie 300,000. na Bonus ya 200,000.
 
Inaonekana huyu Pereira anakubalika na Wazanzibar ña kona zote za ushindi anazijua! Andiko la post ni kama vile anaogopwa!
 
Mapema asubuhi ya leo kada mwengine wa CCM ndugu Pereira Ame Silima amejitokeza katika ofisi kuu za Chama cha Mapinduzi Kisiwandui na kuchukua fomu Idadi ya wagombea wa kuteuliwa kugombea urais Zanzibar kupiti tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM wamefikia wagombea 27

View attachment 1488397

Mfahamu Kiundani
Pereira Ame Silima (PAS) ni mmoja ya makada wa CCM katika orodha ya watu zaidi ya 10 ambao mpaka sasa wametajwa kuwa na nia ya kuipata nafasi ya kuteuliwa na CCM kugombea Urais Zanzibar mwaka huu. Kihistoria PAS kazaliwa Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja tarehe 14 Machi mwaka 1959 na Machi 14 mwaka huu alikata keki na kufanya dua ya kutimiza umri wa miaka 61.

PAS kakulia Unguja ambako ndiko alikosoma na kuhitimu elimu yake ya Kidato cha Nne na kisha kusomea na kupata Stashahada (Diploma) katika mambo ya misitu.Baada ya masomo yake aliajiriwa SMZ kwa nafasi za chini kabla ya kupanda hadi kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo na baadae Wizara ya Biashara, Utalii na Masoko Zanzibar.

Mwaka 2010 aliamua kujitosa katika siasa na kufanikiwa kuchaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Chumbuni kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na akiwa katika nafasi hiyo akateuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani (2010 - 2015).

Awamu ya uchaguzi iliyofuatia yani 2015 wana Chumbuni wakamkataa kuendelee kuwa Mbunge wao hivyo akatupwa nje ya siasa za uwakilishi wa wananchi. Moja ya sababu za kukataliwa na wananchi zinatajwa kuwa ni kushindwa kwake kushughulikia matatizo ya watu wake jimboni na dharau kwa wapiga kura wake ambao kimsingi ndio mabosi zake.

Baada ya anguko hilo, PAS akakaa nje ya ulingo wa siasa na ilipofika mwaka 2017 akateuliwa kuwa Katibu wa Oganaizesheni wa CCM nafasi anayoendelea nayo hadi leo. Kwa tabia PAS ni mtu mkimya na mtaratibu asiyependa kuzungumza sana, sifa nzuri kwa watendaji wa taasisi lakini mbaya kwa kuongoza wananchi. Huenda hii inaelezea kwa nini chama chake kilimpa kazi ya Ukatibu wa Oganaizesheni (taasisi) baada ya kushindwa Ubunge (kazi ya wananchi).

Mbali na ukimya wake, PAS ana mapungufu mbalimbali. Mfano akiwa Katibu Mkuu Kilimo kwa kutumia madaraka yake alijimilikisha eneo ambalo ni moja katika viwanja vya wizara ya kilimo vilivyopo Mazizini bila kufuata taratibu na sheria na baadaye kutumia kiwanja hicho kujenga nyumba yake ya kifahari. Nyumba ndio makazi yake toka ilipokamilika hadi sasa.

PAS pia ana tuhuma za kujimilikisha mashamba ya serikali ya mikarafuu Mtambwe Pemba, Cheju, Selem, Kizimbani, Mwachalale na maeneo ya Mahonda, ardhi ambayo wananchi wanasema kama serikali iliona haitaki tena kuimiliki basi wangepewa wananchi masikini kuendesha shughuli za kilimo na nyenginezo.

Kashfa nyingine inayomuandama PAS ni ile kituko cha yeye na kaka yake (yeye akiwa Katibu Mkuu Biashara na Utalii kaka yake Mussa Ame Silima akiwa Waziri katika Wizara hiyo) kujinufaisha kama familia na kutumia ofisi ya umma na madaraka yao kujipatia maeneo ya fukwe Nungwi na Matemwe ambako wamejenga mahoteli wakiwa ubia kisiri na watu mbalimbali. Mussa Ame Silima kwa sasa ndiye Mwenyekiti wa Wazazi CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Watu wakimya wana mambo walisema wahenga, katika hili, PAS kaonyesha kweli kwani amewahi kuwa katika ugomvi mkubwa na aliyekuwa Waziri wa Fedha SMZ wakati huo Omar Ali Yussuf kwa wawili hao kuweka “heshima” zao mfukoni na kugombania mmoja katika makada wa Umoja wa Vijana wakati huo aliyeitwa Bi Nadra.

Nadra huyu si haba, ni mmoja katika wanawake ambae ameshagombanisha watu wengi Zanzibar, Dodoma na Dar es Salaam na ni maarufu wa kuchanganya wanaume. Zipo taarifa kwamba hivi sasa Nadra ndiye mama watoto wa PAS.

Wataalamu wa siasa za Zanzibar wanasema kitendo cha PAS kutaka kuchukua fomu ya Urais Zanzibar kinaweza kuwa na lengo la kujilinda asitupwe. Hiyo inadadavuliwa kuwa kwa sababu sasa uwezo wake katika CCM una dosari na haoneshi kuimudu nafasi yake kama Katibu wa Oganaizesheni na kuna dalili ya kuondolewa nafasi hiyo mda wowote PAS anatafuta pa kutokea kwamba walau atakumbukwa kuwa aliwahi kutangaza nia na labda atapata uteuzi wa namna fulani. Inasemekana anapanga kuchukua fomu kisha kumuunga mkono mgombea atakayepita ili amlipe fadhila. Wananchi wengi wa Zanzibar na wachambuzi wa siasa wanamuona PAS kama mtu asiye na nafasi yoyote ndani ya mbio za Urais wa Zanzibar 2020.

View attachment 1488515
Hongera Sana
 
Back
Top Bottom