Zanzibar 2020 Namba 8: Shamsi Vuai Nahodha achukua fomu ya kuwania Urais wa Zanzibar kupitia CCM

Zanzibar 2020 Namba 8: Shamsi Vuai Nahodha achukua fomu ya kuwania Urais wa Zanzibar kupitia CCM

Status
Not open for further replies.
Waziri kiongozi mstaafu wa Zanzibar ambaye alihudumu kuanzia mwaka 2000 – 2010, Shamsi Vuai Nahodha amechukua fomu ya kuwania kuteuliwa kugombea urais Zanzibar kwa tiketi ya CCM mapema leo asubuhi katika ofisi kuu ya CCM Zanzibar Kisiwandui.

WASIFU
Shamsi Vuai Nahodha alizaliwa 20/11/1962 na kupata elimu yake katika Skuli ya Msingi Kiongoni huko Makunduchi na kuendelea Sekondari katika Skuli ya Benbella na kisha kufanikiwa kujiunga katika Taasisi ya Kiswahili na Lugha za Kigeni. Ana Shahada ya kwanza aliyoipata Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika fani ya elimu na pia stashahada aliyoipata katika Chuo cha Diplomasia hapo Dar.

Huko mitaani hujulikana kama mtoto wa mkulima na mkwezi alizaliwa shamba Makunduchi Wilaya ya Kusini, Mkoa wa Kusini Unguja.

Nahodha ni Kijana msomi wa Chuo Kikuu mwenye shahada, mtaalamu wa lugha, mwanadiplomasia, mwandishi, mwenye kipaji na mwerevu. Historia yake haioneshi kuwa na dhamana yoyote kubwa kabla ya kujitosa katika siasa na kugombania uwakilishi katika jimbo lake na kuibuka mshindi. Kilichobakia baada ya hapo ni historia kwani nyota yake ghafla ilipaa kutoka Ofisa Habari katika Wizara ya Habari mpaka Waziri kiongozi

Katika mwaka 2000 akiwa na umri wa miaka 38 tu, alikabidhiwa moja ya vyeo vya juu kabisa katika nchi ya Zanzibar kwa kuteuliwa na Rais wa wakati huo Aman Abeid Karume kuwa Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Deserves to compete.
 
Mnyukano wa uteuzi ni mkali Zanzibar. Tunamsibiri Makame Mbarawa halafu finally wanakuwa ni Watatu ambao ni Hussein Mwinyi, Makame Mbarawa na Nahodha kumpata mmoja.
 
Huyu atakatwa tu maana ana misimamo sana ya uzanzibari sawa kabisa na MAALIM au GHALIB BILAL
Naikubali hoja yako, huyu wakati waziri kiongozi yeye na rais wake waliidhinisha serikali ya umoja wa kitaifa na kusababisha wasiyempenda kuwa makamu wa kwanza rais. Na Sasa maalim kaamua kugombea urais kwa hiyo CCM hawawezi kuwapa maswahiba wawili wagombee urais znz.
 
Msindikizaji,Rais wetu Wanzanzibar ni Dr Hussein Mwinyi
 
Nilikutana naye Mwanza 2010-2011 akiwa Waziri wa mambo ya ndani aliongozana na Abbasi Kandoro kwenye Vurugu za wa Machinga yupo simple sana,anastahili.!
 
Aiseee! Hiyo CV....!!! Yaani alisoma masomo ya sekondari kwa mwaka mmoja (1979), basi ni "genius" wa ukweli.
 
Huu ni mtihani mkubwa wa kwanza wa kisiasa Zanzibar mara nyingi Zanzibar wanakuwa na machaguo yao ndio maana wakina Bilal walipoondolewa walipewa nafasi kubwa kuwapooza hata Amani Karume alipitishwa pamoja na kutokuwa na sifa ya degree kwa sababu lilikuwa chaguo la wazanzibar asipocheza karata zake vyema ndio atajua sio kila sehemu vitisho vinafanya kazi
 
Hayaaaaaa nilijua hatachukua huyu Nahodha, basi tena, mpira umempata Messi, huyu nampa 100% kuwa Rais wa Zanzibar, akikosa huyu basi Mbarawa. Ila huyu najua ni best so far. Let's wait, Zanzibar kumenoga
 
Kama Kura zitakuwa huru bila shinikizo wala kubebwa wala kulazimishwa.
Basi Ndugu SHAMSI VUAI NAHODHA ndiye Raisi Stahiki wa Zanziba.
Ni Mzanzibari aliyeitumikia Zanzibar kwa kipindi kirefu, kwa vyeo mbalimbali, kwa uaminifu mkubwa na kwa Uzalendo uliotukuka.

Huyo Mwinyi ni kiongozi wa huku Bara na hana mchango mkubwa kwa Wananchi wa Visiwani Zanzibar.
Tuache dhana za kurithishana madaraka, Familia nyingine pia zina haki ya kuiongoza Zanzabar.
Karume na mwanaye wameitawala Zanzibar kwa miaka mingi.
Mwinyi, Mwanaye naye anataka aitawale Zanzibar.
Mwisho sasa tutawarithisha hadi Wajukuu.
Hebu tujifunze kuridhika na madaraka tuliyonayo.
Wengine nao wapewe nafasi.
Ni Swala la Busara tu.
Mzee umeongea point sana!. Tatizo la Mwinyi ni kuwa aliahidiwa miaka mingi sana. ..ni kama Lowasa au Membe.

Sasa akiukosa huo urais atakufa kwa pressure.

Dk.Bilal kipindi kile ilibidi ahongwe umakamu wa Rais ili kumtuliza..
 
mkuu huyo jamaa unamfahamu kiundani?
Acha kutisha watu. CCM tuache siasa za majitaka. Mnataka mseme ni mwarabu?? Si ndio? Sasa huyo ni mweusi tii na muunguja pure!

Sijui mtatunga uongo gani?
 
Kama raisi wa zanzibar hatapangwa kutoka dodoma Shamsi ndiye mtu sahihi kwa sasa ukiachana na wale wa ule ukoo wa ubwenyenye na usultani
Dodoma ndio tunaamua nani w
awe rais. Hivi tusipo wa control wazanzibari si tutavuna mabua[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Namfahamu sana, ni Mtu Mzalendo, Muadilifu na Mwenye tabasamu la Moyoni mda wote.
Yaani ni mtu Mwema.
Sio kwamba nampigia Debe ila naeleza Ukweli, yuko vizuri katika hadhi ya Uongozi wa juu na alishatumikia nafasi ya.
Waziri Mkuu wa Zanzibar ( wenyewe wana jina lao) na akafanya vizuri sana.
Naodha ,anastahili Zanzibar...km hamna Rafu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom