Namba D, A, C kwenye magari zinamaanisha nini?

IZENGOB

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2014
Posts
323
Reaction score
317
Wadau kama thread hapo juu inavyojieleza namba hizo zinzkua zinaaanisha nini? kama yupo anayezijua maana yake anisaidie manake.

Ninataka natafuta gari naambiwa ngari ipo vizuri namba D Mwingine ananiambia usijali hata kama ni namba C, B haijalishi kwani Prado na gari zilizo nz cc juu ya 2,000 huwa haijalishi Namba kikubwa ni matunzo.

Nipeni uzoefu ndugu zangu nisije ingizwa mjini.
 
Unamaanisha plate number au?

Kama plate no wengi huamini no D kwa sasa ndio latest ingawa zipo no D zina miaka miwil kama DDS.

Hiyo no A ndio zile Gari za mwanzo kabisa zilipewa plate no hizo zinamiaka sio chini ya nane mfano AXY
 
Unamaanisha plate number au
Kama plate no wengi huamini no D kwa sasa ndio latest ingawa zipo no D zina miaka miwil kama DDS,
Hiyo no A ndio zile Gari za mwanzo kabisa zilipewa plate no hizo zinamiaka sio chini ya nane mfano AXY
Asante mkuu,je unaweza pata Plate namba A ikawa nÅŗuri? Sababu kuna jamaa anajza prado 19M ila ni namba A na millage 150,000 nitaishi nayo muda mrefu kweli?
 
asante mkuu,je unaweza pata Plate namba A ikawa nÅŗuri?Sababu kuna jamaa anajza prado 19M ila ni namba A na millage 150,000 nitaishi nayo muda mrefu kweli?
Mtafute fundi unaemuamini ukakague gari kabla ya kununua (maana kuna mafundi vicheche anauza mechi) anakulengesha gari bovu halafu muuzaji anampa hela kidogo
 
Gari inategemea na matunzo, mfano unaweza ukanunua gari kwa mdosi wa town Dar ambalo ni namba A litakuwa na afadhali kuliko namba C linalomilikiwa na jamaa wa kilosa huko.( huo ni mfano tu).

Ni muhimu kujua historia ya mmiliki wa gari kabla kwa kuangalia kadi ya gari( namba za wamiliki) itakupa picha ya hiyo gari, pia uwe na fundi wako au mkodishe mpate muda wa kuichunguza gari kwa kupiga safari ndefu kuijaribu gari, kuna jamaa alinunua gari namba D aweka wese la kutosha akafanya test Dar kwenda Moro, kabla hajafika chalinze akagundua gari ina majanga balas
 
Gari inategemea na matunzo, mfano unaweza ukanunua gari kwa mdosi wa town Dar ambalo ni namba A litakuwa na afadhali kuliko namba C linalomilikiwa na jamaa wa kilosa huko...
Umenifurahisha kutaja Kilosa
 
Gari inategemea na matunzo, mfano unaweza ukanunua gari kwa mdosi wa town Dar ambalo ni namba A litakuwa na afadhali kuliko namba C linalomilikiwa na jamaa wa kilosa huko.( huo ni mfano tu)..

Umeona hii Gari namba C (kwa kuitazama tu).

Kuna mtu anataka kuniuzia kwa 5.5m.

Je, kwa wewe unaona inathamani hiyo ama napigwa cha juu?

Nipe ushauri wako
 
Umeona hii Gari namba C (kwa kuitazama tu)
Kuna mtu anataka kuniuzia kwa 5.5m.
Je kwa wewe unaona inathamani hiyo ama napigwa cha juu? Nipe ushauri wako
Mkuu, itategemea siwezi kusema 5.5m umepigwa au la! cha msingi tafuta fundi wako akaikague gari.
 
Kutembelea gari yenye namba D ni fahari ya kila mtanzania.. Utaheshimika zaidi ukitembelea Passo yenye namba D kuliko Prado yenye namba A.
Zamani nilikuwa naona mtu mwenye latest namba ndo mjanja.

Ila nina gari yangu namba C ila ni nzuri kuliko gari nyingi zenye namba D tena hata zenye DN au DP.

Gari ni matunzo, service kwa wakati na kuendesha kistaharabu.

Ingekuwa mwingine hii gari ingeshakuwa juu ya mawe.
 
Kutembelea gari yenye namba D ni fahari ya kila mtanzania.. Utaheshimika zaidi ukitembelea Passo yenye namba D kuliko Prado yenye namba A.
WEWE JAMAA UNACHEKESHA KWELI NAMBA SIYO ISHU KWENYE GARI.....ISHU NI MATUNZO YA GARI ZIPO GARI NI NAMBA D LAKINI UKIZIANGALIA TU UNACHOKA YAANI KIMUONEKANO IPO CHINI KULIKO NAMBA A KUNA WATU WANAPIMP MAGARI YANAPENDEZA BALAA
 
WEWE JAMAA UNACHEKESHA KWELI NAMBA SIYO ISHU KWENYE GARI.....ISHU NI MATUNZO YA GARI ZIPO GARI NI NAMBA D LAKINI UKIZIANGALIA TU UNACHOKA YAANI KIMUONEKANO IPO CHINI KULIKO NAMBA A KUNA WATU WANAPIMP MAGARI YANAPENDEZA BALAA
Jamaa kaandika reality iliyopo mtaani .kiukweli gari hata imeremete vipi ikiwa namba A ata kugeuka nyuma kuiangalia shingo inapata kaugumu na kauzito flani.
 
Unamaanisha plate number au?

Kama plate no wengi huamini no D kwa sasa ndio latest ingawa zipo no D zina miaka miwil kama DDS.

Hiyo no A ndio zile Gari za mwanzo kabisa zilipewa plate no hizo zinamiaka sio chini ya nane mfano AXY
Hahahah namba A unasema miaka zaidi ya 8? Namba A zilianzaga 2007 mkula...Kwasasa ni gari za miaka kati ya 11-13 toka zisajiliwe nchini.

Hio DD ni gari ya registration ya mwaka 2015 nchini which means ni gari ya miaka 5 nyuma na si miwili kama unavyodhani.

Hizi Plate number zinakupa picha ya gari imetumika kiasi gani nchini. Gari nzuri za kununua kwa sasa ambazo ni walau ziko current kuanzia mwezi June mwaka jana to date. DQ,DR,DS,DT,DU hapo unakuta gari kama liko kwa mtu makini basi still linakuwa OG sana.
 
Yeah! Ila Niliandika si chini ya miaka nane inamaana miaka nane kwenda juu.

Na hii post kamanda ilikua ni ya 2018 kamanda
 
Hata ka gari matunzo ila namba A na namba B kwa sasa hapana asee kwanza litakua na kilomita ngapi gari ulitoa japan 2006 hadi leo miaka 14 ukipiga hesabu ya kilomita efu 10 kwa mwaka inakuja kilomita laki moja na efu 40.

Mengi namba A yapo juu ya mawe na kwa yanayotembea kwa sevice zetu hizi za kibongo injini zitakua zishabadilishwa unless yale makubwa makubwa kama Landcruiser Landrover
 
Zipo Prado namba A zimenyooka kuliko D ambazo zimetoka japan miezi 6 iliopita😁
 
Nora ununue namba A ya long trip kuliko namba D ya town trip.
D ya mjini imechoka injini kwa kuwasha na kusima mara kibao tu, breki kila mita 50.
 
Kuna gari namba B haijafikisha km 90,000.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…