Mganguzi
JF-Expert Member
- Aug 3, 2022
- 1,604
- 3,715
Tetesi za kweli zisizo na shaka hata kidogo ni kwamba CCM wanakaribia kufanya usajili mzito na kila kitu kipo tayari! Baada ya yule jamaa kutambulishwa juzi, usiku wa kuamkia leo majira ya saa 12:20, kulikuwa na mazungumzo nyeti yakimhusisha namba mbili, jamaa wa Iringa pamoja na mwenyekiti mkuu wa chama kwa njia ya mkutano wa video.
Bwana yule ameahidiwa kupewa jukumu kubwa la kitaifa na kimataifa haraka iwezekanavyo! Jamaa huyo aliumizwa vibaya na utawala uliopita, hivyo akawa anataka kwanza watu wamalize kile kamchango. Hata hivyo, boss amemwambia atampa gari mpya zaidi ya ile anayoiwaza!
Habari za uhakika ni kuwa mwezi ujao jamaa ataachana na chama chake na atapokelewa rasmi katika chama cha kijani na blue! Mapokezi yamepangwa kufanyika Arusha ambapo kutakuwa na shughuli maalum. Siasa ni ugali!