Ngoja nijaribu mkuu
Afrika ina nchi 54 ila wanachama wa CAF wapo 56 na ndugu zetu kama zanzibar na sehemu nyingine ambapo unakuta kwenye nchi kuna sehemu inajitegemea kimpira hivyo idadi kuwa 56 badala ya 54 twende kwenye mada sasa:–
Team zinazotakiwa kuanza preliminary stage ni 32 ila kiuhalisia team zote zinatakiwa zianze hatua ya awali ila kutokana na changamoto mbali mbali kama nchi kushindwa kushiriki kutokana na vita na kufingiwa na FIFA idadi hyo haofiki ambayo ilitakiwa iwe 64 ili zikicheza mtoano zibaki 32 sasa baada ya kuona Caf hlo haliwezekani ikabidi waweke utaratibu huu ifuatao,
Idadi ya wawikilishi wa Caf katika mwaka husika ndo inaamua idadi ya team zinazoanzia hatua ya awali au ya mtoano kwa mfano mwaka huu wawakilishi ni kutoka nchi 46 twende sasa
Idadi ya awali ni 64÷2=32 ambayo ndio inayotakiwa ila kwasababu wawakilishi idadi hyo kinafanyika hichi
44 ni wawakilishi wa mwaka huu katika Caf champions league hapo toa team 12 zinazotoa wawakilishi wawili wawili kila nchi hvyo itakuwa
44–12=32
12×2=24
24+32=56
64–56=8
Kwa hyo team nane tu ndo hazitaanza hatua ya awali msimu huo husika ambapo:–
44 – ni adadi ya wawakilishi katika mwaka husika.
12– ni idadi ya nchi ambazo zinatoa team mbili Caf champions league.
24– ni idadi ya team ambazo zinatoka katika wawakilishi 12 wa Caf .
32 – ni idadi ya wawakilishi wa caf iliyobakia katika wawakilishi 44 wa Caf baada ya kutoa 12.
56 – ni jumla ya team zote kutoka katika wawakilishi 44 wanachama wa caf.
64 – ni idadi halisi inayotakiwa ambayo kutokana na sababu mbali mbali haifikiwi.
8 – ni idadi ya team zinatozotakiwa kukamlishi team 64 na hizo nane ndo hazianzii hatua ya awali.