KERO Namba ya huduma kwa waeja ya benki ya NMB: 0800002002 ni kero kubwa, haipokelewi

KERO Namba ya huduma kwa waeja ya benki ya NMB: 0800002002 ni kero kubwa, haipokelewi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Kwa kweli hii namba ni kero sana., unapiga dakika za kutosha(kumi na zaid), unakata kisha unapiga tena simu haipokelewi. Badala yake, unaambiwa uendelee kusubir mpaka unaamua kuacha /kukata.

Simu nilianza kupiga tangu juzi ila mpaka leo sijafajikiwa, na sababu ya kuwapigia ni matatizo yanayosababishwa na system yao.

Unaamua kwenda kwenye tawi lao, nako ni yale yale yaani ni foleni mwanzo mwisho. Kwa kifupi NMB mnaboa na huenda mna wateja kuliko uwezo wenu wa kuwahudumia ingawa mtaani vijana wasio na ajira ni wengi tu.

Hayo mabilioni mnayopata kama faida kila mwska kwanini msyatumie kuajiri wafanyakazi wapya mkatupunguzia kero?

Hakika NMB mnakera sana.

Hovyo kabisa!
 
Hawa ni wahuni, nilipoteza kadi yangu ya benki nili tumia siku mbili kuwapata ili waifunge kadi yangu nisiibiwe vijisenti vyangu, nilipowata niliwashauri pia waache kuweka matangazo kwenye namba hiyo ili mtu akipiga aongee na mtoa huduma moja Kwa moja Lakini niwagumu sana kuelewa.
 
Sio uongo,nimewahi kuwapigia mara kadhaa bila mafanikio,nadhani waiondoe sasa ijulikane kabis hakuna namba ya huduma kwa wateja kuliko kuwepo alafu hawapokei.
 
Bora muwa expose hivyo hivyo. Angalau CRDB wanapokea. Japo kitengo cha huduma kwa wateja kwa njia ya whatsapp ni kichomi. Sms unatuma asubuhi unakuja kujibiwa jioni. Au unatuma sms asubuhi halafu automatically unajibiwa usiku mwema
😁😁😁
 
Hawa ni wahuni ,nilipoteza kadi yangu ya benki nili tumia siku mbili kuwapata ili waifunge kadi yangu nisiibiwe vijisenti vyangu,nilipowata niliwashauri pia waache kuweka matangazo kwenye namba hiyo ili mtu akipiga aongee na mtoa huduma moja Kwa moja Lakini niwagumu sana kuelewa.
Kuna umuhimu wa kushawishi vijana wanaojiriwa wasipitishe mshahara wao kwenye hii benki ni wazi wamezidiwa na wateja na hawajiongezi.
 
Ndugu mteja tunajua shida yako hujaona mshahara tafadhali wasiliana na muajiri wako tatizo siyo letu
 
Back
Top Bottom