halafu wakishakupigia inakuwaje!au wanakuambia nini!!
mmojawapo anakupigia anajifanya kukufahamu pia anaweza kuwa ashakufatilia,anakupa deal kuwa kuna mzungu anatafuta kemikali fulani na deal la million 11-15 au zaidi.mara anakata simu ghafla.
harafu unapigiwa simu na nigga mmoja anajifanya mzungu pia anaongea kingereza anakwambia kwamba amepewa namba yako na jamaa wa kwanza aliokupigia simu pia anakwambia yuko njiani anakuja mkoa uliopo pia anakwambia yuko na cash million 11-15 au zaidi na anajifanya ata kukuuliza hotel gani nzuri karibu na ulipo ( wakat mwingine akuulizi hotel gani)harafu simu inakatika.
baada ya hapo unapigiwa simu na jamaa wa kwanza anakwambia ashapata mtu ambaye anauza hiyo kemikali ila anahiuza laki 3 na anakwambia anakupa namba yake ili umtumie pesa kwa mpesa na ata unaweza ukaongea naye anakwambia yuko mbali kidogo ila utume pesa wakuletee mzigo wakat mwingine anakuruhusu utume ata nusu kwanza yani 150,000 ili hakifika na kukupa mzigo ummalizie,
pia yule mzungu anakupigia tena simu kukuuliza mzigo ushapata maana yuko na cash taslimu million 11 au 15 ata zaidi.
ukituma pesa tu wote hawapatikani simu zao,unakuwa umeliwa,watu wengi wapenda utajiri wa fasta wamelizwa .
mkumbuke kwamba yule jamaa wa kwanza kupiga anakuwa na maneno matamu kwamba yeye amekuona wewe ndio mtu muaminifu na anakupa deal ilo la pesa ndefu sababu anakuamini sana,yani anaongea maneno matamu.
kuweni makini wana JF