Naantombe Mushi
JF-Expert Member
- Oct 16, 2015
- 6,253
- 15,748
Wanasiasa wanajaribu kutumia nguvu kuaminisha wananchi kwamba uchumi wa Tanzania unakua na maisha ya watu yanaimarika. Ila wanasahau kwamba namba hazipo upande wao na takwimu hazidanganyi.
Wao pengine wana maana yao kusema kwamba uchumi unakuwa, kwa sababu ni mtaji wa kisiasa, ukisema uchumi unakuwa ina maana wananchi watapenda uendelee kuwaongoza.
Naamua kupingana na wanasiasa, na yeyote yule ambaye anaamini ya kwamba uchumi wa nchi hii upo vizuri.
Nimefanya utafiti wangu na nimetumia takwimu zilizopo wizara ya fedha na banki kuu, nilichokiona baada ya utafiti wangu ni kwamba uchumi wetu bado upo chini, sio mzuri kama tunavoaminishwa.
Ntaelezea baadhi ya viashiria ili na nyie muweze kutafakari
1) ‘Currency in circulation to GDP ratio’ (Mzunguko wa pesa ukifananisha na GDP)
Dhana ya uchumi unaokuwa huwa ni kwamba, uchumi unakuwa unadhalisha bidhaa na huduma katika rate ambayo inakuwa inaongezeka. Kutokana na kuongezeka kwa bidhaa na huduma zinazozalishwa kwenye nchi, ndipo sasa kunakuwa na msukumo wa pesa kuweza kuongezeka kwenye mzunguko. Sasa ki nadharia uchumi unapokuwa, utaona pia kwamba hata ile hatua ya pesa kuongezeka kwenye uchumi inakuwa kubwa ukilinganisha na zao ghafi la nchi (GDP)
Sasa kwa Tanzania, kwa miaka ya hivi karibuni, hakujakuwa na improvement yoyote kwenye currency in circulation kama chart inavojionesha hapa chini. Hii inakupa picha moja kubwa kwamba; msukumo wa mahitaji ya pesa kwenye uchumi umekuwa ukipungua in relative terms, na hii ni ishara kwamba level ya shughuli za kiuchumi sio nzuri kama ilivokuwa.
Ukisoma report nyingi za benki kuu wamekiri wazi, money supply ya uchumi wetu ilipaswa kukua kwa wastani wa Zaidi ya asilimia 10 kwa mwaka lakini ukiangalia vizuri kwa miaka ya hivi karibuni huo ukuaji wa money supply wa Zaidi ya silimia 10 haujawahi kuonekana, ikiwa ina maana ya ni wazi kwamba level ya shughuli za kiuchumi bado sio ya kuridhisha.
2) ‘Stock market performance’ or ‘Assets prices’
3) Commercial banks’ balance sheets to GDP ratio (afya kwenye sekta ya benki)
Kiashiria kingine kinapima uimara we sekta ya kibenki na namna inavo respond kwenye ukuaji wa uchumi. Ki nadharia kwenye uchumi wowote unaokuwa, ina maana kunakuwa na ongezeko kubwa la shughuli za kiuchumi ambazo hupelekea mikopo kwenye taasisi za fedha kuweza kuongezeka kadri uchumi unavopanuka.
Kwa Tanzania, miaka ya hivi karibuni, mikopo ambayo ndo assets kuu ya mabenki ya kibiashara, nayo imekuwa kweye mkwamo mkubwa. Both kwenye ubora na kwenye ukuaji wake.
Unaweza kuona katika chart hapa chini, kwamba balance sheet za mabenki na uwiano wake umekuwa ukienda chini, hii ikimaanisha kwamba level ya uchumi sio ya kuridhisha.

| Figures in '000 | 2016 | 2017 | 2018 | 2019 |
| GDP at market price | 97,011,409,300 | 103,317,150,905 | 108,999,594,204 | 116,084,567,828 |
| Currency in circulation | 4,374,339,542 | 4,354,606,292 | 4,646,962,897 | 4,965,202,559 |
| Currency in circulation to GDP ratio | 4.51% | 4.21% | 4.26% | 4.28% |
Ukisoma report nyingi za benki kuu wamekiri wazi, money supply ya uchumi wetu ilipaswa kukua kwa wastani wa Zaidi ya asilimia 10 kwa mwaka lakini ukiangalia vizuri kwa miaka ya hivi karibuni huo ukuaji wa money supply wa Zaidi ya silimia 10 haujawahi kuonekana, ikiwa ina maana ya ni wazi kwamba level ya shughuli za kiuchumi bado sio ya kuridhisha.
2) ‘Stock market performance’ or ‘Assets prices’
- Uchumi wowote unaokuwa huwa unasababisha assets prices ziweze kuongezeka. Assets kama nyumba, viwanja, hisa n.k. Hii ni kwa sababu, uchumi ukiwa unakuwa, watu wanakuwa na pesa, mzunguko wa pesa unakuwa mkubwa, mahitaji yanakuwa makubwa, hivo kupelekea bei za hivi vitu kupanda. Ndo mana wataalamu huwa wanasema stock market na assets ni thermometer ya uchumi wowote ule duniani.
- Kinyume chake ni kweli, ukiona bei ya assets kama nyumba, viwanja, na hisa, zinashuka hiyo ni dalili tosha kwamba uchumi upo kwenye mdororo.
- Angalia hii chart hapa ni index ya stocks pale DSE, picha nadhani inajieleza yenyewe. Kwenye masoko ya nyumba na viwanja, nadhani madalali watakuwa wasemaji wazuri lakini kote huko bei zimedondoka, ikiashiria hakuna pesa zinazunguka kununua hizo assets, wawekezaji hawana appetite tena na Tanzania, hakuna capital flow yenye tija, sekta binafsi inadorora n.k
- Hii picha inabeba maneno elfu moja kuhusu uchumi wetu
3) Commercial banks’ balance sheets to GDP ratio (afya kwenye sekta ya benki)
Kiashiria kingine kinapima uimara we sekta ya kibenki na namna inavo respond kwenye ukuaji wa uchumi. Ki nadharia kwenye uchumi wowote unaokuwa, ina maana kunakuwa na ongezeko kubwa la shughuli za kiuchumi ambazo hupelekea mikopo kwenye taasisi za fedha kuweza kuongezeka kadri uchumi unavopanuka.
Kwa Tanzania, miaka ya hivi karibuni, mikopo ambayo ndo assets kuu ya mabenki ya kibiashara, nayo imekuwa kweye mkwamo mkubwa. Both kwenye ubora na kwenye ukuaji wake.
Unaweza kuona katika chart hapa chini, kwamba balance sheet za mabenki na uwiano wake umekuwa ukienda chini, hii ikimaanisha kwamba level ya uchumi sio ya kuridhisha.
| GDP at market price | 97,011,409,300 | 103,317,150,905 | 108,999,594,204 | 116,084,567,828 |
| Commercial bank balance sheet | 16,005,103,200 | 16,187,487,200 | 16,734,098,200 | 18,129,789,900 |
| Commercial bank balance sheet to GDP ratio | 16.50% | 15.67% | 15.35% | 15.62% |