Namba zinanuka: Naunga mkono TANESCO ifumuliwe, na ikiwezekana ibinafsishwe kabisa, Makamba yupo sahihi 100000%. TANESCO ni janga

Namba zinanuka: Naunga mkono TANESCO ifumuliwe, na ikiwezekana ibinafsishwe kabisa, Makamba yupo sahihi 100000%. TANESCO ni janga

Cha msingi ,mtu aipate huduma ya umeme kwa bei rahisi.

Tz tunanunua unit moja kwa bei rahisi kuliko uganda.na kuunganishiwa umeme ni wastani wa 27,000.kwa hiyo ni bei nafuu kwa mtu wa kawaida.na hilo ndio lengo kuu la huduma za umma
Ni bei nafuu ila kwa kusubiria miezi 6 au zaidi huo muda una thamani kuliko hio elfu 27!
Siku tukijua kuthamini muda watanzania tutafanikiwa kuondoa umaskini japo kwa 50% toka tulipo sasa!
 
Mimi ukiniuliza kwa namba, TANESCO ya Magufuli imefanya kazi kubwa kuliko Tanesco yoyote toka tupate uhuru.

Kabla ya 2015 TANESCO ilikua na wateja 1.8m, yaani kwa miaka 55 tanesco iliweza kuunganisha watenja 1.8m pekee.

Kwa miaka 5, yaani 2016 hadi 2021 tanesco imeunganisha wananchi 1.2m, kwa maana kwamba ukiwapa tanesco miaka 55 kama tanesco ya kabla ya 2016, wataunganisha wananchi 13.2m.

Magufuli alifanya mambo mengi mazuri na mabaya lakini mnapomponda msisahau facts basi ama muwe na facts na sio chuki tu kama vile mtu alietembe ana mkeo ama mpenzi wako.

Mbaya zaidi kwa kupindi hicho cha Magufuli TANESCO imeweza ku post faida ya 52B, angalia vitabu vya hesabu vya mwaka 2020 kutoka kwa CAG.

Sasa wewe nisaidie kujua ni tanesco gani ilikua nzuri zaidi ya hii ya Magufuli? Ile ya jakaya ya kukatika umeme siku 8? Ama nyingine? Ile ya jakaya ya Dowans, Symbion, Agreko, IPTL, Capacity charges, service charges, kuunganisha umeme kwa zaidi ya laki 3 kwa mjini ama tanesco ipi?

Tumponde Magu kwa facts kidogo basi.
Gambino ni MWONGO. Katika mashirika ambayo hayakukaguliwa na CAG kwa mwaka 2019/20 ni pamoja na TANESCO. Swali hiyo faida unayoisema wewe imethibitishwa na nani?
 
Hata kwa macho ya kawaida yasiyohitaji kuumiza kichwa..TANESCO ya mwendazake IMEOZA.

JMakamba ana mzigo mzito sana, akijichanganya na Siasa kwenye hii reformations anayotegemea kuifanya amekwenda na Maji.
Duuu kwa hiyo sababu ya kuweka kuanzia 2016 ni kujustify mnachotaka kufanya na kuonyesha kwamba Magu alivurunda TANESCO,haya sawa
 
Gambino ni MWONGO. Katika mashirika ambayo hayakukaguliwa na CAG kwa mwaka 2019/20 ni pamoja na TANESCO. Swali hiyo faida unayoisema wewe imethibitishwa na nani?
Screenshot_20210927-220123_Adobe Acrobat.jpg
Screenshot_20210927-220142_Adobe Acrobat.jpg

Mkuu haikukaguliwa CAG hizi findings alizitoa wapi?

Kuna vitu havikukaguliwa lakini sio vyote, nilifuatilia huo mtanange hadi kwenye kamati za bunge kwa mashirika yale ambayo yalisemekana hayakukaguliwa.

Tuwe tunajitahidi kusoma kwanza, usipende tu kupewa summary.
 
View attachment 1955030View attachment 1955032
Mkuu haikukaguliwa CAG hizi findings alizitoa wapi?

Kuna vitu havikukaguliwa lakini sio vyote, nilifuatilia huo mtanange hadi kwenye kamati za bunge kwa mashirika yale ambayo yalisemekana hayakukaguliwa.

Tuwe tunajitahidi kusoma kwanza, usipende tu kupewa summary.
Nimemnukuu Spika Job Ndugai alivyosema alipokuwa anahitimisha mkutano wa Bunge mwezi June.

Aidha wewe mwenyewe umekiri kuwa kuna baadhi ya vitu havikukaguliwa na CAG. Kwa hiyo hayo majedwali uliyoweka yatumie tu kama course work ya chuo. Ila siyo conclusive kwa kupimia utendaji wa Taasisi
 
Ndio maana serikali imeamua kuteua wajumbe wa bodi wanabiashara Ili kulisaidia shirika kujiendesha.

Na imesema haitaingilia mambo ya management na Kwa maana Hiyo serikali ilipe madeni yake.
Mkuu, hii ni ngumu aisee. Hakuna mwananchi wa kawaida atayeweza kulipa tsh 600 kwa unit moja ya umeme! Na Znz haitakubali kuanza kulipia umeme sasa, hii pia itafanya bei ya umeme ipande zaidi.

Biashara ni kuuza kwa faida. Ngeleja alifikiria kufanya hivyo kwa kuligawa shirika vipande vitatu, UZALISHAJI, USAFIRISHAJI na USAMBAZAJI, kwamba serikali ibakiwe na Usafirishaji tu. Hoja ikawa, Uzalishaji na Usafirishaji wataweza kufanya biashara ya faida, mzigo utabaki kwa huyu msambazaji ambaye ukiachilia mbali wezi wa umeme, ataweza kusubiri malipo ya serikali yamachuwe? Kwamba watumie leo wakulipe baada ya mwaka mmoja? Yeye atapaswa kununua umeme kwa cash kutoka kwa wazalishaji ambao kwa wakati huo sasa ni kina Dowans, Symbion, IPTL, Richmond, Aggreko n.k kisha alipie usafirishaji kwa serikali mwenye hiyo miundombinu, lakini kwakuwa anamdai serikali, atafidia hapo, hivyo kampuni ya Usafirishaji umeme ya serikali itakumbwa na ukata, ishindwe kuhudumia miundombinu, kisha nini kitatokea?

SA na Escom yao sasa hivi ni majanga, kisa ni miundombinu inakufa kwakuwa serikali haiwezi kuihudumia, jamaa wana mgao siku hizi.
 
Duuu kwa hiyo sababu ya kuweka kuanzia 2016 ni kujustify mnachotaka kufanya na kuonyesha kwamba Magu alivurunda TANESCO,haya sawa
Hapa wanafeli kwakweli, hata zile stori za maji kukauka ziliisha kipindi cha mwana, mimi mwananchi wa kawaida nimewahi kuishi miezi 3 mfululizo bila kuona katizo la umeme, hili ni jambo lililokuwa muujiza kwa miaka 55 ya uhuru.

Kama wafanyakazi wa Tanesco hawakuwa na furaha kipindi cha jiwe lakini umeme ukawa wa uhakika, basi waendelee tu kununa kwa manufaa ya nchi na huo ndio uzalendo.

Waulize wenye viwanda, tatizo la availability lilishaisha, lilibakia tatizo la quality. Ila sasa, tafuta mtu mmoja aliye kwenye magroup ya Tanesco akuambie jinsi malalamiko yalivyo mengi.
 
unajjua impact ya kubinfsisha shirika kama tanesco wewe? hapo ni sawa sawa kusema hospitali kubwa kama muhimbili ibinafsihwa. tanesco ikibinafsishwa lazima umeme utauzwa bei kubwa, oparation cost ya viwanda itaongezeka na definately products zitapanda bei. hapo cost of living itaongezeka na std of living ya wananchi itashuka. kubinafsisha tanesco ni hatari mno. ndio maana tuna mixed economy kind of economic system. acheni mihenko
 
Hata kwa macho ya kawaida yasiyohitaji kuumiza kichwa..TANESCO ya mwendazake IMEOZA.

JMakamba ana mzigo mzito sana, akijichanganya na Siasa kwenye hii reformations anayotegemea kuifanya amekwenda na Maji.
Kwani ya JK ilikuwaje, tuletee na hio bwashee!
 
1. Form za maombi ya kuunganishiwa umeme ziliondolewa tukashangilia

2. Service charge ziliondolewa tukashangilia.

3. Service line cost zilishushwa mpaka Tsh 320,900/= kwa single phase ndani ya mita 30 tukashangilia.

4. Service line cost zimeshushwa mpaka Tsh 27,000/= kwa wateja walio na umbali mpaka mita 120 tukashangilia.

5.Gharama za uzalishaji kila siku zinapanda

Kutokana na hayo hapo juu mnategemea TANESCO ifanye vizuri?

Tunapenda vitu cheap na ndio maana matatizo ni mengi.
 
Nitauliza swali hili Tanesco ya uganda ina hudumia wateja wangapi ukilinganisha na hii ya Tanzania?

Umeme ni huduma kwa wananchi au ni biashara inayo takiwa iingizie serikali faida? Matumizi ya kodi ni kwa ajili ya nini? Kwa nini wananchi wanalipa kodi?

Nimeangalia CV ya CEO mpya unabaki unashangaa tu. Shirika la Kitaaluma kama Tanesco unatakiwa umuweke anaye liongoza awe anaongea lugha moja na watendaji wa core function ya shirika. Kwanza ni kama kuwa dhalilisha mainjinia wa nji hii. Na huyu CEO linapokuja suala la utaalamu wa co function ya shirika itabidi awe mpole na tegemezi tu. Hata hivyo kuhujumiwa inakuwa rahisi sana. Sijui members wa body kama kuna hata engineer mmoja wapo atakaye ongea lugha moja na waendesha shirika huku chini?
Aliyependekeza JM apewe uwaziri wa nishati has done us a favour this was a ‘litmus test’ for him on his long term political ambitious.

Mtu yoyote mwenye uelewa wa kawaida tu wa biashara, without trying to be the ‘prophet of doom’ maamuzi yake ya awali tu ameshafail.

Matatizo ya TANESCO ukisoma statement yao na malalamiko ya wananchi kuna issue za engineering technicalities na capacity planning za project management; mfano kwenye statement niliyosoma mimi wameshachukua zaidi ya billioni 2 za kuwafungia watu umeme kazi ambayo aijafanyika hiyo ni loss of income tatizo ni nini? uzembe au limited resources ya kuongeza kasi. Solution yake unahitaji mtu mwenye skills za project management za infrastructure au engineer.

Then kuna issue ya kukatika umeme ideally you need an engineer with succession planning ambae ameshapewa managerial training along the way za kusimamia hilo tatizo a substitute is someone with energy management qualification.

Put it this way logic says huyo mtu ameshafeli kabla hata ajafungua mlango wa ofisi.

Muhimu zaidi lengo la Magufuli lilikuwa ni kuzalisha umeme at low unit cost karibu na nchi za west zineweza ivyo; sasa mtu kama Nehemia solution zake ni price hike.

Personal nimeshamfuta Makamba as a likely future presidential candidate, alikuwa na hiyo risk he is too unrealistic ambitious.

Watch this space hiyo team yake inaenda tengeneza matatizo zaidi TANESCO.
 
1. Form za maombi ya kuunganishiwa umeme ziliondolewa tukashangilia

2. Service charge ziliondolewa tukashangilia.

3. Service line cost zilishushwa mpaka Tsh 320,900/= kwa single phase ndani ya mita 30 tukashangilia.

4. Service line cost zimeshushwa mpaka Tsh 27,000/= kwa wateja walio na umbali mpaka mita 120 tukashangilia.

5.Gharama za uzalishaji kila siku zinapanda

Kutokana na hayo hapo juu mnategemea TANESCO ifanye vizuri?

Tunapenda vitu cheap na ndio maana matatizo ni mengi.
Lengo la Magufuli lilikuwa ni kutumia vyanzo vyenye unit cost nafuu or a mixture of different sources which reduces the average unit cost, kumpa unafuu mtanzania.

So msianze mambo ya NHC public housing kupanga rent za private landlords; muende waumiza watu wenye income ndogo with price hike ambazo awawezi zimudu kama ilivyotokea NHC chini ya Nehemia.
 
Mabadiliko ni muhimu ila kuwaweka waliowekwa wenye dosari za kiutendaji kwenye rekodi zao kumepoteza maana ya mabadiliko aliyofanya.

Wapigaji hawakutakiwa kuingizwa kwenye hiyo menejimenti, haitakiwi urafiki uwe kigezo cha kuteua wajumbe, bali ni sifa na weledi wao kiutendaji, hili ni doa zaidi hata kwa waziri mwenyewe mwenye rekodi mbovu.
Kuna kitu kinaandaliwa kwa ustadi mkubwa sana, huoni puppets wa February wanazidi kujaa humu? Ngoja tusubiri
 
Lengo la Magufuli lilikuwa ni kutumia vyanzo vyenye unit cost nafuu or a mixture of different sources which reduces the average unit cost.

So msianze mambo ya NHC public housing kupanga rent za private landlords; muende waumiza watu wenye income ndogo with price hike ambazo awawezi zimudu kama ilivyotokea NHC chini ya Nehemia.
Sijapinga lengo la JPM ni zuri sana. Na kati ya kitu ambacho nilikubaliana na JPM ni hicho. Kabla hatujafikia huko hapa tuna survive vipi kila kitu kiende sawa. Taarifa zinasema mwaka jana TANESCO ilikusanya 1.8T na kilichotumika ni 1.8T maana yake hakuna faida. Sasa bei zimeshushwa za Service line tutarajie matumizi makubwa kuliko mapato maana yake ni hasara.
Tukumbuke vitu vizuri vyote ni gaharama.
 
Matumizi na mapato kulingana, ni either haukusanyi vizuri mapato au unatumia vibaya unachopata.
Kwa issue ya Tanesco ni kwamba hawakusanyi vizuri, ilipaswa wakusanye zaidi ya hiyo 1.8T. bado Hadi leo Kuna taasisi nyingi za serikali zinatumia umeme bure.
Fikiria tu Zanzibar umeme wao unatoka bara, Ila wanachokusanya kinabaki hukohuko.
Kuna mwaka jiwe alikuja na amri ya KATA, Yani kwa kila wanaodaiwa wakatiwe umeme. Uliibuka mgogoro mkubwa sana Kati ya Zanzibar na jiwe. Shein hakupenda Hilo suala.
Hivyo tulikosea tokea zamani, kutoka hapa tulipo sio kazi ndogo. Maana kuwaambia wote wanaodaiwa walipe na zile taasisi ambazo hazilipi umeme zianze kulipa sio kazi ndogo.
 
Mtoa mada amepotelea kwenye usomi usio na uhalisia hata kidogo. Huo mfananisho na uwiano hauna uhalisia hata kwa ⅛ ya ukweli halisi.

Labda tumuulize mtoa mada, anajua MDAIWA SUGU wa Tanesco ni serikali kuu? Anajua umeme unaotumiwa visiwani unatoka huku ila makusanyo yote yanaishia kule kule? Una fahamu shirika lina zaidi ya wafanyakazi 6000 na takribani nusu ya wafanyakazi wanapewa unit 750 kila kwezi kwa gharama isiyozidi shilingi 12,000?

Sasa kama Tanesco wataongeza assets ili kuzalisha na kusambaza umeme, halafu wasikusanye sawa na assets zao, utawalaumu? Fikiria Mkurugenzi wa Tanesco anaenda kuidai IKULU, kambi za jeshi kupitia wizara, mahospitali kupitia wizara, shule n.k, hao wote hawalipi ujue!

Sasa binafsisha au liendeshe kibiashara tuone unapataje faida na kupandisha ufanisi! Netgroup solutions walikata umeme Ikulu, sijui kama unakumbuka? Enzi za Idrisa, kisa cha kujiuzulu ni Tanga cement kudaiwa zaidi ya 900ml na hawataki kulipa kwakuwa mkubwa anafahamiana na waziri na m/kiti wa bodi ambao wanashinikiza deni lisilipwe.

Jamaa walifikiria kuzima umeme uendao visiwani pia.

Sijui kama huu wa namba unajua yote hayo, na hata hivyo, kuifananisha Tanesco na kakitu kadogo ka Uganda ni kuizalilisha. Enzi za Julius, Tanesco ilikuwa shirika bora Africa, nambari uno. Sasa hatuna haja ya kwenda mbali kuchukua namba kujifunza, tufute mavumbi yale madocs, tugelezee tu.
Umemjibu vizuri Sana

Kwanza Tanesco makusanyo wanakabidhi hazina..

Unakuja walaumu kwa lipi??
 
Aliyependeza JM apewe uwaziri wa nishati has done us a favour this was a ‘litmus test’ for him on his long term political ambitious.

Mtu yoyote mwenye uelewa wa kawaida tu wa biashara, without trying to be the ‘prophet of doom’ maamuzi yake ya awali tu ameshafail.

Matatizo ya TANESCO ukisoma statement yao na malalamiko ya wananchi kuna issue za engineering technicalities na capacity planning za project management; mfano kwenye statement niliyosoma mimi wameshachukua zaidi ya billioni 2 za kuwafungia watu umeme kazi ambayo aijafanyika hiyo ni loss of income tatizo ni nini? uzembe au limited resources ya kuongeza kasi. Solution yake unahitaji mtu mwenye skills za project management za infrastructure au engineer.

Then kuna issue ya kukatika umeme ideally you need an engineer with succession planning ambae ameshapewa managerial training along the way za kusimamia hilo tatizo a substitute is someone with energy management qualification.

Put it this way logic says huyo mtu ameshafeli kabla hata ajafungua mlango wa ofisi.

Muhimu zaidi lengo la Magufuli lilikuwa ni kuzalisha umeme at low unit cost karibu na nchi za west zineweza ivyo; sasa mtu kama Nehemia solution zake ni price hike.

Personal nimeshamfuta Makamba as a likely future presidential candidate, alikuwa na hiyo risk he is too unrealistic ambitious.

Watch this space hiyo team yake inaenda tengeneza matatizo zaidi TANESCO.

Kwenye viongozi wote wa Tanesco ambao ni mainjinia ukose mmoja wa kumpandisha awe CEO?!! Huu uteuzi mzima umebebwa na ile hoja ya mimi kama Waziri sitaki kupigiwa simu kuna nguzo imeanguka Kigamboni. Mfumo wa kidigitali kugundua fault ilipo ambao inawezekana Tanesco wataununua. Wala usishangae wakina maxmanini wakipewa tena kandarasi za kutuuzia LUKU.
 
Sijapinga lengo la JPM ni zuri sana. Na kati ya kitu ambacho nilikubaliana na JPM ni hicho. Kabla hatujafikia huko hapa tuna survive vipi o kitu kiende sawa. Taarifa zinasema mwaka jana TANESCO ilikusanya 1.8T na I kilichotumika 1.8T maana yake hakuna faida. Sasa bei zimeshushwa za Service line tutarajie matumizi makubwa kuliko mapato maana yake ni hasara.
Tukumbuke vitu vizuri vyote ni gaharama.

Magufuli ni mtu aliekuwa akifanya informed decision nadhani alielewa sana standing costs za shirika bado zipo juu kushinda income.

Mipango yake ni ya muda mrefu shusha bei ya kuunganisha umeme, lower production costs na unganishia watu wengi zaidi eventually utakuwa on profit.

Na it was working, sasa kaangalie tena customer reserve capital watu wangapi washalipia deposit bado awajafungiwa umeme hiyo ni future revenue loss kwa sababu ya uzembe unaacha wateja wakati wewe una fixed costs; how are you gonna break even.
 
Nimekuwa nikitafiti mwenendo wa performance wa shirika letu la umeme kwa muda mrefu, ila sikuweza kufanikiwa kupata takwimu kwa wakati. Nikimaanisha takwimu za kifedha za shirika letu hili. Nashukuru Mungu leo wameweka taarifa za kifedha na nimeweza kuendelea na utafiti wangu.

Ila kwa kweli ni kwamba hili shirika naweza kusema kabisa kwa performance kiduchu niliyoiona, nakubaliana kabisa na yeyote yule amabaye ana mtizamo wa kufanya mabadiliko kwenye shirika hili. Namba zinanuka zimeoza kabisa, kwa miaka mitano iliyopita hakuna performance yoyote ya kueleweka.

Ili tuweze kuelewa maana ya 'underperformance ya TANESCO, nimeamua kufananisha na shirika lingine la umeme la Uganda 'TANESCO ya UGANDA' ... yaani hii comparative analysis inaweza kukutoa machozi, na kuamini ni kwa jinsi gani watanzania tunakuwa wazembe kiasi hiki.

Siwezi kuandika naomba namba ziongee zaidi....

Ndo mana bado ntazidi kuamini ya kwamba nchi hii kuna mambo mengi sana tumepigwa mchanga wa macho.......

View attachment 1954796

Maelezo kwa faida ya wengi

Hii maana yake ni kwamba, Tanesco ya Tanzania wamerundika amana (assets) nyingi ambazo hazitengenezi mapato yoyote na hali imekuwa hivo ndani ya miaka mitano iliyopita. (Huu ni ukichaa wa aina yake) And mind you, hizi amana zimekuwa zikiongezwa kwa kutumia pesa za walipa kodi kwa sababu Tanesco ni mali ya serikali... Umewaza nini hapo???? Watanzania tumekuwa tukilipia hii inefficiency ya Tanesco for years.... Ni sawa sawa mtoto na kuwa unauza shamba ngombe zako kupeleka Ngombe shule... Thats it...

TANESCO YA UGANDA (UMEME)
Revenue growth between (2016 - 2020)
22.28%​
Total assets growth (2016 - 2020)
19.72%​

TANESCO YA TANZANIA
Revenue growth between (2016 - 2020)
13.38%​
Total assets growth (2016 - 2020)
42.90%​

Kwa faida ya wengi.

Wasomi wa JF kama wewe kichefu chefu Sana

Unalaumu management ya Tanesco as if walikuwa na power ya kufanya lolote

Chini ya Magufuli mapato yote walikuwa wanapeleka hazina na matumizi yeyote lazima waombe kibali..
Mara nyingi vibali hawapewi zaidi ya matumizi ya kawaida
Nimekuwa nikitafiti mwenendo wa performance wa shirika letu la umeme kwa muda mrefu, ila sikuweza kufanikiwa kupata takwimu kwa wakati. Nikimaanisha takwimu za kifedha za shirika letu hili. Nashukuru Mungu leo wameweka taarifa za kifedha na nimeweza kuendelea na utafiti wangu.

Ila kwa kweli ni kwamba hili shirika naweza kusema kabisa kwa performance kiduchu niliyoiona, nakubaliana kabisa na yeyote yule amabaye ana mtizamo wa kufanya mabadiliko kwenye shirika hili. Namba zinanuka zimeoza kabisa, kwa miaka mitano iliyopita hakuna performance yoyote ya kueleweka.

Ili tuweze kuelewa maana ya 'underperformance ya TANESCO, nimeamua kufananisha na shirika lingine la umeme la Uganda 'TANESCO ya UGANDA' ... yaani hii comparative analysis inaweza kukutoa machozi, na kuamini ni kwa jinsi gani watanzania tunakuwa wazembe kiasi hiki.

Siwezi kuandika naomba namba ziongee zaidi....

Ndo mana bado ntazidi kuamini ya kwamba nchi hii kuna mambo mengi sana tumepigwa mchanga wa macho.......

View attachment 1954796

Maelezo kwa faida ya wengi

Hii maana yake ni kwamba, Tanesco ya Tanzania wamerundika amana (assets) nyingi ambazo hazitengenezi mapato yoyote na hali imekuwa hivo ndani ya miaka mitano iliyopita. (Huu ni ukichaa wa aina yake) And mind you, hizi amana zimekuwa zikiongezwa kwa kutumia pesa za walipa kodi kwa sababu Tanesco ni mali ya serikali... Umewaza nini hapo???? Watanzania tumekuwa tukilipia hii inefficiency ya Tanesco for years.... Ni sawa sawa mtoto na kuwa unauza shamba ngombe zako kupeleka Ngombe shule... Thats it...

TANESCO YA UGANDA (UMEME)
Revenue growth between (2016 - 2020)
22.28%​
Total assets growth (2016 - 2020)
19.72%​

TANESCO YA TANZANIA
Revenue growth between (2016 - 2020)
13.38%​
Total assets growth (2016 - 2020)
42.90%​

Kwa faida ya wengi.

Wasomi wa Jf kama wewe kichefu chefu sana
Tanesco chini ya Magufuli walikuwa wanakabidhi mapato yote serikalini na spending yeyote Ile tofauti na mishahara wanaomba kibali...

Hao waganda wanafanya kazi kwenye setu ya aina hii??..

Nina thread kama 3 humu nalalamikia centralisation ya Magufuli ilivyo haribu uchumi....

Dig deeper..
 
Magufuli ni mtu aliekuwa akifanya informed decision nadhani alielewa sana standing costs za shirika bado zipo juu kushinda income.

Mipango yake ni ya muda mrefu shusha bei ya kuunganisha umeme, lower production costs na unganishia watu wengi zaidi eventually utakuwa on profit.

Na it was working, sasa kaangalie tena customer reserve capital watu wangapi washalipia deposit bado awajafungiwa umeme hiyo ni revenue loss kwa sababu ya uzembe.

Max please ongea na huyu mod wako serious hana shida gani huyu mtu kichwani kwake, mbona yupo so addicted na mimi.

I can’t type right now the cursor is just jumping the other day (jumamosi) I was locked out of my iPhone.

Ongea na huyu mtu wako au mtafutie therapy hanijui mimi ni mchangiaji kama members wengine aachane na addictiony zake serious huyu mtu ni tatizo.

Nilifikiri ni mimi tu kuwa locked out hiyo j1 kumbe wako wengine. Ila kwa vile ni bure hapajF ilibidi kuwa mpole tu na najua hayuko wa kuzuia kusudi la Mungu.
 
Back
Top Bottom