Nimekuwa nikitafiti mwenendo wa performance wa shirika letu la umeme kwa muda mrefu, ila sikuweza kufanikiwa kupata takwimu kwa wakati. Nikimaanisha takwimu za kifedha za shirika letu hili. Nashukuru Mungu leo wameweka taarifa za kifedha na nimeweza kuendelea na utafiti wangu.
Ila kwa kweli ni kwamba hili shirika naweza kusema kabisa kwa performance kiduchu niliyoiona, nakubaliana kabisa na yeyote yule amabaye ana mtizamo wa kufanya mabadiliko kwenye shirika hili. Namba zinanuka zimeoza kabisa, kwa miaka mitano iliyopita hakuna performance yoyote ya kueleweka.
Ili tuweze kuelewa maana ya 'underperformance ya TANESCO, nimeamua kufananisha na shirika lingine la umeme la Uganda 'TANESCO ya UGANDA' ... yaani hii comparative analysis inaweza kukutoa machozi, na kuamini ni kwa jinsi gani watanzania tunakuwa wazembe kiasi hiki.
Siwezi kuandika naomba namba ziongee zaidi....
Ndo mana bado ntazidi kuamini ya kwamba nchi hii kuna mambo mengi sana tumepigwa mchanga wa macho.......
View attachment 1954796
Maelezo kwa faida ya wengi
Hii maana yake ni kwamba, Tanesco ya Tanzania wamerundika amana (assets) nyingi ambazo hazitengenezi mapato yoyote na hali imekuwa hivo ndani ya miaka mitano iliyopita. (Huu ni ukichaa wa aina yake) And mind you, hizi amana zimekuwa zikiongezwa kwa kutumia pesa za walipa kodi kwa sababu Tanesco ni mali ya serikali... Umewaza nini hapo???? Watanzania tumekuwa tukilipia hii inefficiency ya Tanesco for years.... Ni sawa sawa mtoto na kuwa unauza shamba ngombe zako kupeleka Ngombe shule... Thats it...
| TANESCO YA UGANDA (UMEME) | |
| Revenue growth between (2016 - 2020) | 22.28% |
| Total assets growth (2016 - 2020) | 19.72% |
| TANESCO YA TANZANIA | |
| Revenue growth between (2016 - 2020) | 13.38% |
| Total assets growth (2016 - 2020) | 42.90% |
Kwa faida ya wengi.