Habari za mida wakubwa, naomba kusaidiwa katika hili.
Kuna rafiki yangu mmoja ambaye tulikua tukifanya biashara pamoja na kutokea kuaminiana sana, kuna kipindi biashara yake iliyumba kidogo ikabidi anikope mimi hela, nilimkopesha shilingi laki nne bila mshahidi wala kuandikisha popote kutokana na kumuamini sana. Kwa sasa jamaa amebadilika na amekua mtu wa kunizungusha na promise zisizokua na ukweli. Umepita muda mrefu kidogo sasa na dalili za kulipwa sizioni.
Nataka kuchukua hatua za kisheria ila nashindwa kujua nianzie wapi kwa sababu tulipeana hela bila shahidi, napata wasiwasi kwamba anaweza kunikana.
Naomba ushauri wenu wakubwa, ni hatua gani naweza kufata ili nipate haki yangu kisheria? Kumbuka nilimpa hela bila shahidi wala kuandikishiana popote. Msaada tafadhali...