Namfananisha Rais Magufuli na Mfalme Nebkadneza

Namfananisha Rais Magufuli na Mfalme Nebkadneza

daza steven

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2016
Posts
359
Reaction score
358
Nimemsikiliza leo huyu Mzee kwa umakini mkubwa ndiyo nimemwelewa vizuri kwa mara ya kwanza kuwa Rais wa awamu ya 5 Ndugu na Daktari Joni Pombe Magufuli ni kiongozi si waajabu lakini nimemfananisha na Mfalme Nebkadneza ambaye yeye wakati wa utawala wake alikuwa anategemea wataalam wa mwili yaani kidunia na wataalam wa mambo ya roho yaani vitu visivyo onekana katika mwili hili kufanikisha mambo katika utawala wake.

Ukimsoma vizuri Mfalme Nebkadneza katika kitabu cha Daniel utaona wazi alikuwa akihitaji sana ushauli kutoka kwa mainjinia, wataalam wa hesabu na wataalam wa kijamii lakini vilevile alikuwa anawatumia wanajimu, waganga wa asili, watu wanao wasiliana na roho, wabashiri na watu wanaoamini Mungu na miungu yeye akuwaacha walikuwa washauri katika Ikulu yake na walikuwa na posho, mshahara kama wafanyakazi wengine.

Mfleme Nebkadneza alikuwa akulupuki hata sikumoja na hakuwa na kazi za makosa au kukosea kosea, Ninamfananisha na DKT Pombe magufuli, leo amedadavua kitu ambacho lazima uchanganye elimu ya dunia na roho pia uweze kupata jibu. Wakati dunia imekosa majibu yeye Magufuli anayatafuta majibu, unaelewa?

Wapinzani hususani Chadema wamekuwa wakipiga kelele kila kuchao wakisema, tu lokudauni tena neno la kizungu kama lilivyo wamelileta kama lilivyo tufanye kama wazungu wanavyofanya lakini Mhs. Amilijeshi Mkuu wa Majeshi amechomoa na kupigilia msumali kwa kusema na yeye kizungu Neva. Hakuna Dar kufungwa wala hakuna mtu yeyote kufungiwa ndani hadi kieleweke.

Sitaki kusema mengi ila natoa ushauri kwa makundi mawili yaani wananchi na kundi lingine ni wanasiasa hasa wapinzani:
Watanzania mimi nawashauri kwa kuwa nimemwelewa huyu mtu wekeni imani yenu kwake hakulupuki hata kidogo anaingia kote kote kupata majibu.

Wanasiasa hasa wapinzani mtakuwa na kazi ngumu zana tena kama mtaendelea kushindana na huyu mtu mimi nawaambia ukweli huyu ni noma na msipo angalia mtakosa lijitimasi katika jamii ya watanzania kwani ninyi mnapambana naye katika mwili tu na katika mwili vilevile hamko vizuri ni lazima mtakuwa mnafeli kilasiku ndiyo maana tangia jamaa aingie madarakani hakuna hata kiki moja iliyowai kupiga ikawaka amshagai? Msimuangalie kwa huruma jamaa anatoa doctrine kutoka katika biblia na misahaf na vitabu vingine vya imani. Anakusanya data bila kulala, usiku kucha anatafuta alafu ninyi mnaamka asubui saa 4 mnaanza kumpinga hakika mtapata taabu sana.

Sasa angalia hasara ya kucheza ngoma za wazungu, walisema lokudauni lakini leo kule Marekani wananchi wametoka wote nje tena wanaandamana kama hakuna korona, wamekataa kufungiwa ndani na rais trump amewasapoti, tujifikirie.
Alafu ni hatari kuwa na viongozi ambao jambo wakifanya watu wa dunia ya kwanza naye anataka na sisi dunia ya pili tufanye hivyo huyo si kiongozi au viongozi. Viongozi kama hawa lazima tuwaogope sana ni hatari.

Ukiamgalia utaweza kushangaa sana kama ni mfwatiliaji mambo katika nchi za dunia ya kwanza zote kadri walivyozidi kulokudouni ndiyo maambukizi yalivyokuwa yanazidi kuongezeka sasa hili uwezi kuliona katika mwili lazima uwe Nebkadneza.
Hakika Magu msimwangalie kwa huruma ni noma tulieni hadi apite wallah amumwezi.

Watanzania namaliza kwa kusema msimwangalie Mzee Magu kama mnaangalia kipala chake ni zaidi ya vile mnavyomwona wekeni imani yenu kwake hakika mtapona katika hii vita ya korona na uchumi wa Tanzania.
Nimejaribu kupunguza maneo sana mwenye masikio na asikie.
 
Jaman watanzania hatutokufa na kakorona haka
Watu 10 ndio wamekufa hata ajali ya baiskeli haiui hivyo
Hapa shughuli ni hofu tu
 
Mara ombeni Mungu, mara tumieni muarobaini na tangawizi. [emoji848]
IMG-20200422-WA0040.jpg
IMG-20200422-WA0042.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hafanani na Nebuchadnezzar bali anafanana na Mfalme Caligula.

Gaius Caesar aliyepewa jina la Caligula “kiatu kidogo” alizaliwa Augst 31 mwaka 12 Baada ya Kristo yaani B.K. katika mji wa Antium kwa sasa unaitwa Anzio huko Italia. Alikuwa mtoto wa tatu katika watoto sita walizaliwa na Germanicus na mkewe Agrippina mkubwa. huyu alichukua uongozi toka kwa Tiberius akiwa ni mtawala wa Roma kuanzia mwaka 37 B.K na kuchukua jina la Gaius Caesar Germanicus.

Kumbukumbu zinaonesha alikuwa ni mmoja ya watawala wakatili sana asiye na huruma, asiyetabirika na mwenye roho mbaya.alikamata watu wote ambao walikuwa wakimpinga na kuwa hukumu kifo.

Gaius alikua karibu sana na baba yake kipindi akikua. Akiwa na miaka 3 alianza mara nyingi kuwa akimsindikiza Germanicus katika shughuli zake za kivita. Hivyo mara nyingi alikuwa akitoka naye na akiendelea kutunza tamaduni zao yeye alipendelea kuvaa sare na tu buti tudogo na hivyo kupelekea kupewa jina la Caligula yaani Tu buti tudogo. Jina ambalo lilidumu naye kwa maisha yake yote.
 
Mkuu Kuna watu wanakuja na porojo humu kupumbaza wa tz wakati hawana dhamana kubwa kushinda serikali,nilichangia andiko humu kuwa baadhi ya watu hawaelewi dhana ya ki uungu Leo wameumbuka-hawatoi constructive ideas Bali kutukana na kukosoa serikali tu,warembo wa mjini wanasema yule Kaka mchakarikaji(serikali)huyu Kaka kila siku kijiweni(waleta porojo miaka ya 90 tulikuwa tunawaita akina chande)ninachoshukuru Hawa Ni akina harmorapa (watafuta kick) sio innovative (mkemia baba-jpm)nakumbuka enzi za great depression rais Franklin Delano Roosevelt akiwa raise wa USA kwa wakati huo alipokuja na the new deal(ikiwa na 3R's-relief,recovery na reforms-vitu ambavyo Roosevelt wa tz amezifanya leo)(jpm ndie Roosevelt wa korona mtabwabwaja Sana,eleweni nafasi ya dini na jamii yake katika jamii(uchaguzi ukifika mnawafuata kuombewa ndio maana mnaangukia pua Sabu hamna Imani ya ki uungu)mtateseka Sana kuwaona watu wa Mungu hawafai
 
EBU SOMA DANUELI 4Danieli 4:1

[1]Mfalme Nebukadreza, kwa watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, wanaokaa katika dunia yote; Amani iongezeke kwenu.Danieli 4:1-33

[1]Mfalme Nebukadreza, kwa watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, wanaokaa katika dunia yote; Amani iongezeke kwenu.

[2]Mimi nimeona vema kutangaza habari za ishara na maajabu, aliyonitendea Mungu aliye juu.

[3]Ishara zake ni kubwa kama nini! Na maajabu yake yana uweza kama nini! Ufalme wake ni ufalme wa milele; na mamlaka yake ni ya kizazi hata kizazi.

[4]Mimi, Nebukadreza, nalikuwa nikistarehe katika nyumba yangu, nikisitawi katika nyumba yangu ya enzi.

[5]Nikaota ndoto iliyonitia hofu; mawazo niliyokuwa nayo kitandani mwangu, na njozi za kichwa changu, zikanifadhaisha.

[6]Basi nikatoa amri kwamba wenye hekima wote wa Babeli, waletwe mbele yangu, ili kunijulisha tafsiri ya ndoto ile.

[7]Ndipo wakaingia waganga, na wachawi, na Wakaldayo, na wanajimu; nikawahadithia ile ndoto; wao wasiweze kunijulisha tafsiri yake.

[8]Bali hatimaye Danieli akaingia mbele yangu, ambaye jina lake ni Belteshaza, kwa kufuata jina la mungu wangu; tena ndani yake inakaa roho ya miungu watakatifu; nikamhadithia ile ndoto, nikisema,

[9]Ee Belteshaza, mkuu wa waganga, kwa sababu ninajua ya kuwa roho ya miungu watakatifu inakaa ndani yako, na ya kuwa hapana neno la siri likushindalo, niambie njozi za ndoto yangu niliyoiona, na tafsiri yake.

[10]Njozi za kichwa changu kitandani mwangu zilikuwa hivi; naliona, na tazama, palikuwa na mti katikati ya nchi, urefu wake mkubwa sana.

[11]Mti ule ukakua, ukawa na nguvu, urefu wake ulifika mpaka mbinguni, na kuonekana kwake mpaka mwisho wa dunia.

[12]Majani yake yalikuwa mazuri, na matunda yake mengi, na ndani yake chakula cha kuwatosha watu wote; wanyama wa kondeni walipata uvuli chini yake, na ndege wa angani walikaa katika matawi yake; kila kitu chenye mwili kilipata chakula kwake.

[13]Nikaona katika njozi za kichwa changu kitandani mwangu, na tazama, mlinzi, naye ni mtakatifu, alishuka kutoka mbinguni.

[14]Akapaza sauti yake, akasema, Ukateni mti huu, yafyekeni matawi yake, yapukusieni mbali majani yake, na kuyatawanya matunda yake, wanyama na waondoke hapo chini yake, na ndege katika matawi yake.

[15]Walakini kiacheni kisiki cha shina lake katika ardhi, pamoja na pingu ya chuma na shaba, katika majani mororo ya kondeni; kikapate maji kwa umande wa mbinguni, na sehemu yake iwe pamoja na wanyama katika majani ya nchi;

[16]moyo wake ubadilike, usiwe moyo wa binadamu, na apewe moyo wa mnyama; nyakati saba zikapite juu yake.

[17]Hukumu hii imekuja kwa agizo la walinzi, na amri hii kwa neno la watakatifu; kusudi walio hai wapate kujua ya kuwa Aliye juu anatawala katika ufalme wa wanadamu, naye humpa amtakaye, tena humtawaza juu yake aliye mnyonge.

[18]Mimi, Nebukadreza, nimeiona ndoto hii; na wewe, Ee Belteshaza, eleza tafsiri yake, kwa maana wenye hekima wote wa ufalme wangu hawawezi kunijulisha tafsiri yake; bali wewe waweza, maana roho ya miungu watakatifu inakaa ndani yako.

[19]Ndipo Danieli, aliyeitwa jina lake Belteshaza, akashangaa kwa muda, na fikira zake zikamfadhaisha. Mfalme akajibu akasema, Ee Belteshaza, ndoto ile isikufadhaishe wala tafsiri yake. Belteshaza akajibu, akasema, Bwana wangu, ndoto hii iwapate wao wakuchukiao, na tafsiri yake iwapate adui zako.

[20]Ule mti uliouona, uliokua, ukawa na nguvu, urefu wake ukafika mpaka mbinguni, na kuonekana kwake mpaka dunia yote;

[21]ambao majani yake yalikuwa mazuri, na matunda yake mengi, na ndani yake chakula cha kuwatosha wote; ambao chini yake wanyama wa kondeni walikaa, na ndege wa angani walikuwa na makao yao katika matawi yake;

[22]ni wewe, Ee mfalme, uliyekua, na kupata nguvu; maana ukuu wako umekua na kufika mpaka mbinguni, na mamlaka yako yamefika mpaka mwisho wa dunia.

[23]Tena, kwa kuwa mfalme alimwona mlinzi, naye ni mtakatifu, akishuka kutoka mbinguni, akisema, Ukateni mti huu, mkauangamize; ila kiacheni kisiki cha shina lake katika ardhi, pamoja na pingu ya chuma na shaba, katika majani mororo ya kondeni; kikatiwe maji kwa umande wa mbinguni, na sehemu yake iwe pamoja na wanyama wa kondeni, hata nyakati saba zipite juu yake;

[24]tafsiri yake ni hii, Ee mfalme, nayo ni amri yake Aliye juu, iliyomjia bwana wangu, mfalme;

[25]ya kuwa utafukuzwa mbali na wanadamu, na makao yako yatakuwa pamoja na wanyama wa kondeni, nawe utalazimishwa kula majani kama ng’ombe, nawe utatiwa maji kwa umande wa mbinguni, na nyakati saba zitapita juu yako; hata utakapojua ya kuwa Aliye juu ndiye anayemiliki katika ufalme wa wanadamu, naye humpa yeye amtakaye, awaye yote.

[26]Na kwa kuwa waliamuru kukiacha kisiki cha shina lake; ufalme wako utakuwa imara kwako, baada ya wewe kujua ya kuwa mbingu ndizo zinazotawala.

[27]Kwa sababu hiyo, Ee mfalme, shauri langu lipate kibali kwako; ukaache dhambi zako kwa kutenda haki, ukaache maovu yako kwa kuwahurumia maskini; huenda ukapata kuzidishiwa siku zako za kukaa raha.

[28]Hayo yote yakampata mfalme Nebukadreza.

[29]Baada ya miezi kumi na miwili, alikuwa akitembea ndani ya jumba la kifalme katika Babeli.

[30]Mfalme akanena, akasema, Mji huu sio Babeli mkubwa nilioujenga mimi, uwe kao langu la kifalme, kwa uwezo wa nguvu zangu, ili uwe utukufu wa enzi yangu?

[31]Hata neno lile lilipokuwa katika kinywa cha mfalme, sauti ilikuja kutoka mbinguni, ikisema, Ee mfalme Nebukadreza, maneno haya unaambiwa wewe; Ufalme huu umeondoka kwako.

[32]Nawe utafukuzwa mbali na wanadamu, na makao yako yatakuwa pamoja na wanyama wa kondeni; utalishwa majani kama ng’ombe, na nyakati saba zitapita juu yako, hata utakapojua ya kuwa Aliye juu ndiye anayemiliki katika ufalme wa wanadamu, naye humpa amtakaye, awaye yote.

[33]Saa iyo hiyo jambo hilo likatimizwa, likampata Nebukadreza; alifukuzwa mbali na wanadamu, akala majani kama ng’ombe, na mwili wake ulilowa maji kwa umande wa mbinguni, hata nywele zake zikakua, zikawa kama manyoya ya tai, na kucha zake kama kucha za ndege.
 
Mkuu Kuna watu wanakuja na porojo humu kupumbaza wa tz wakati hawana dhamana kubwa kushinda serikali,nilichangia andiko humu kuwa baadhi ya watu hawaelewi dhana ya ki uungu Leo wameumbuka-hawatoi constructive ideas Bali kutukana na kukosoa serikali tu,warembo wa mjini wanasema yule Kaka mchakarikaji(serikali)huyu Kaka kila siku kijiweni(waleta porojo miaka ya 90 tulikuwa tunawaita akina chande)ninachoshukuru Hawa Ni akina harmorapa (watafuta kick) sio innovative (mkemia baba-jpm)nakumbuka enzi za great depression rais Franklin Delano Roosevelt akiwa raise wa USA kwa wakati huo alipokuja na the new deal(ikiwa na 3R's-relief,recovery na reforms-vitu ambavyo Roosevelt wa tz amezifanya leo)(jpm ndie Roosevelt wa korona mtabwabwaja Sana,eleweni nafasi ya dini na jamii yake katika jamii(uchaguzi ukifika mnawafuata kuombewa ndio maana mnaangukia pua Sabu hamna Imani ya ki uungu)mtateseka Sana kuwaona watu wa Mungu hawafai
 
Hofu ni mbaya kuliko corona yenyewe" in jpm voice
 
Mkuu Kuna watu wanakuja na porojo humu kupumbaza wa tz wakati hawana dhamana kubwa kushinda serikali,nilichangia andiko humu kuwa baadhi ya watu hawaelewi dhana ya ki uungu Leo wameumbuka-hawatoi constructive ideas Bali kutukana na kukosoa serikali tu,warembo wa mjini wanasema yule Kaka mchakarikaji(serikali)huyu Kaka kila siku kijiweni(waleta porojo miaka ya 90 tulikuwa tunawaita akina chande)ninachoshukuru Hawa Ni akina harmorapa (watafuta kick) sio innovative (mkemia baba-jpm)nakumbuka enzi za great depression rais Franklin Delano Roosevelt akiwa raise wa USA kwa wakati huo alipokuja na the new deal(ikiwa na 3R's-relief,recovery na reforms-vitu ambavyo Roosevelt wa tz amezifanya leo)(jpm ndie Roosevelt wa korona mtabwabwaja Sana,eleweni nafasi ya dini na jamii yake katika jamii(uchaguzi ukifika mnawafuata kuombewa ndio maana mnaangukia pua Sabu hamna Imani ya ki uungu)mtateseka Sana kuwaona watu wa Mungu hawafai
Mpaka sasa Tanzania inaongoza kwa kasi ya maambukizi ya COVID-19 Afrika mashariki na kati, narudia tena inaongoza kwa "kasi", sasa hizo tambo zinatoka wapi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mpaka sasa Tanzania inaongoza kwa kasi ya maambukizi ya COVID-19 Afrika mashariki na kati, narudia tena inaongoza kwa "kasi", sasa hizo tambo zinatoka wapi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Na kwa nn dsm,znzbr na Arusha zaidi,jiulize ndipo uhoji Kasi na tupo wiki ya ngapi nipo nakula Kaka andiko linamapungufu nisamee nakula
 
Back
Top Bottom