Namkubali Rais Samia, lakini suala la Mbowe linapunguza mapenzi yangu dhidi yake

Tatizo la watawala ni kuogopa kukosolewa na kuwajaza elimu ya kujitambua wananchi.

Watawala wanahofu kubwa sana siku wananchi wakijua haki zao basi ccm ndiyo itakuwa kwaheri
Kuna kitabu fulani cha fasihi ya kiswahili kinaitwa "Usiku utakapokwisha......"
 
Kwahiyo kumbe sio ugaidi bali makongamano [emoji1]
 
Aisee Omitontozi umenena kama nilivyokuwa nafikiria. Hapo mama ameingizwa chaka bila kujua. Ni bora ashtuke mapema!
 
Toka ameingia ametangaza ajira kibao taasasi mbalimbali au haupo nchi hii!!? Ila nachotaka na kutamani ni amwachie
Mbowe sio mhalifu hata kidogo aache kumtesa
Hata Mimi hapo kwa Mbowe inanipotezea mahaba kwa mama
 
Habari sn
 
kwa hiyo mkuu kama maza akimwabia DPP wake kwamba kesi ifutwe basi utakuwa huna tatizo naye jengine? kama ni hivyo basi utakuwa umekosea sana maana kinachofanya Mbowe ashikiliwe si Ugaidi bali ni madai yake ya Katiba mpya, anaisumbua Dola isitawale kwa kupumua na anawachochea wananchi wasifanye maendeleo badala yake waanze vilinge vya kudai katiba mpya.

Je ndugu huna mashaka na katiba iliyopo sasa ? kwamba haiendani na wakati uliopo? kwamba inashindwa ku-balance kati ya Watawala, watawaliwa na watunga sheria na watoa haki? kwa maana hiyo watawala wanapoka madaraka mengi maana katiba haipo specific? unaonaje madaraka ya Rais?
 
Sio wewe tu. Yaani watanzania wote wapenda haki na amani wamemdharau. Imegundulika kumbe hayuko tayari kubadilika.
 
Katiba muhimu sana asante kwa elimu
 
Rubbish.
 
Ukiacha la Mbowe unampendea Tozo au mgao wa maji na umeme ?
Nimefika mkoani Tabora tangu jumatano, mgao wa umeme ukiwatesa wananchi. Joto kali na ac haiwaki, hakuna umeme. Tangu jumapili mpaka leo umeme haujakatika, na msongo wa mawazo umepunguza. Najiuliza, huu umeme umetoka wapi? Kilikuwa kinatikiswa kibiriti?
 
Binafsi nampenda lkn swala la Mbowe linaninyima furaha
Marejeo ya kinacho endelea mahakamani, kama repoti ya mashahidi wa serikali zinafika bila kurekebishwa, ni bora zisiletwe. Zimejaa ulaghai wa wazi.
 
Tunategemea kupata ufumbuzi wa matatizo yetu toka kwao watendaji walio yaanzisha, wakatimuliwa na kisha kurejeshwa kundini.
 
Anatapakaza madarasa,zahati,Vituo vya afya,barabara za vijijini,muswada bima ya afya kwa wote unaenda kuwasilishwa na mengine mengi,,,Kibaya ni kumfunga mzee Mbowe
Hizo ni ngonjera tu. Uhalisia ni tofauti. Km vituo vya afya na zahanati vina uhaba mkubwa wa watumishi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…