Namkumbuka Rafiki Yangu Gershom Chihota (1950 - 2023)

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
NAMKUMBUKA RAFIKI YANGU WA UDOGONI GERSHOM CHIHOTA (1950 - 2023)

Kiasi cha kama siku tatu zilizopita nimepokea taarifa kutoka kwa Ally Max Marekani.
Ajabu jinsi kifo kinavyoweza kufungua majalada ndani ya ubongo wa binadamu.

Nataka kuanza na Ally Max.

Ally Max ni mdogo sana kwetu hapa nakusudia kwangu mimi na kwa marehemu Gershom kwani siku Ally alipokuja St. Joseph's kuanza shule mimi nilikuwa nimesimama sehemu tukiita ''School Compound.''

Ally alikuwa kashikwa mkono na dada yake Eyshe (Allah amrehemu).

Nyumba ya Mzee Abbas Max muasisi wa TANU Iringa na nyumba ya kina Chihota zilikuwa zimetenganishwa na uwanja mdogo wa mpira ambao watoto wa hapo mtaani wakicheza.

Ally Max akimjua Gershom toka udogo wake.
Hapa ni Magomeni Mikumi sisi vijana wa wakati ule tukipaita ''Soulville.''

Hii ilikuwa miaka ya mwishoni 1960 umri wetu ulikuwa wastani wa miaka 15.

Soulville ilikuwa kipande tu cha Magomeni Mikumi ambako wazee wetu wengi wao waliokuwa na nyadhifa kubwa serikalini walijenga nyumba zao hapo: Nyerere, Machapati, Muhuto, Mgone, Bakuname, Mwakinyo, Kandoro, Kambona, Chief Fundikira, Ntare, Mzena na Abdul na Ally Sykes kwa kutataja wachache.

Hii Soulville ni nini?

Huu ulikuwa wakati wa muziki wa ''Soul'' muziki uliokuwa unaeleza maisha ya mtu mweusi Amerika.

Wazimu wa muziki huu na sisi ulitusibu Dar es Salaam na tuliweza hata tukaupiga na ulikuwa unatoka Detroit mji ambao Ally Max leo anaishi.

Siku ya Jumatano shule ilikuwa mwisho saa sita mchana.

Hii ndiyo ilikuwa siku mchana wake na Jumamosi na Jumapili tunakutana Mikumi kupiga magitaa.

Gersom alikuwa ''Bassist'' hodari sana akitumia mkono wa kushoto.

Mimi nikimtania nikimwambia anapiga bass mkono wa kushoto kama Paul Mc Cartney wa The Beatles.

Gershom akicheza mpira vizuri sana akitumia mguu wa kushoto lakini mapenzi yake yalikuwa kwenye muziki.

Gershom Chihota tulikutana St. Joseph's mwaka wa 1967 na tukawa marafiki wakubwa sana tuko pamoja muda mwingi.

Kupitia kwake nikawajua kaka zake Raymond na Norman Chihota.

Norman akisoma Azania na alikuwa bingwa wa taifa wa mbio fupi mita 100 kiwango cha kimataifa kwani aliwakilisha Tanzania Michezo ya Commonwealth na kwengine kwingi.

Sifa ya Gershom ilikuwa ni upole kiasi tukampa lakabu tukimwita, ''Cool Kid.''

Kabla ya akina Chihota kuhamia Mikumi walikuwa wakikaa Temeke Wailesi na kupia kwake nikaja kufahamiana na vijana wenzangu wazaliwa wa Temeke Mick Jones (Mikidadi), Choggy Sly (Salum), Allah Brown (Ali Ngota) na nduguze wa kiume wote.

Baba yake Gershom, Mzee Chihota alihama Southern Rhodesia (Zimbabwe) kuja Tanganyika kutafuta maisha.

Ulipofunguliwa Ukumbi wa Arnautoglo Mzee Chihota akawa ndiyo meneja wake.

Mzee Chihota akapata nafasi ya kwenda kusoma Uingereza na huko akafariki na kuzikwa huko huko.

Nyumbani kwa kina Gershom kulikuwa na picha inamuonyesha mama yetu amekaa pembeni ya kaburi la mumewe.

Mama alikwenda Uingereza kulizuru kaburi la mume wake.

Mama yetu huyu alifanyakazi Ikulu hadi Zimbabwe ilipopata uhuru ndipo akarudi Zimbabwe miaka ya 1980.

Si muda mrefu watoto wake wakamfuata.
Mwaka wa 1993 nilikwenda Harare na nilimtafuta Gershom.

Nakumbuka mshangao alioupata baada ya kubisha hodi mlango wake na yeye akatoka akanikuta nimesimama mbele yake namtazama.

Gershom alikuwa wakati ule akifanya kazi Monamotapa Hotel moja ya hoteli kubwa sana Harare.

Wakati niko Harare Manu Dibango alikuwa mjini akifanya maonyesho.

Gershom na mimi tulimzungumza kidogo lakini nadhani rafiki yangu alitambua kuwa miaka imebadilika.

Gershom hakugusia kuniambia twende tukamsikilize Manu Dibango.

Ninachokumbuka tulizungumza kuhusu taarifa kutoka magazetini watu waliokwenda kwenye onyesho lake wakilalamika kuwa hakuwapigia nyimbo yake maarufu ''Soul Makosa,'' lau kama walimuomba afanye hivyo.

1687111727612.png
 
Mzee Mohammed Said Mwenyezi Mungu akuongezee kumbukumbu ulio nayo na umri wako. Hakika unastahili pongezi mashallah, mimi kuna mwanafunzi mwenzagu nimeonana nae mwaka jana hata jina lake nimemsahau.

Na shule nimemaliza juzi tu, yule jamaa aliona kama nimemdharau lakini hajui binaadamu tunapitia mambo mengi sana.
 
Watu wengi niliosoma nao primary nimewahau kwanza class tulikuwa 122
 
Mzee Mohammed Said Mwenyezi Mungu akuongezee kumbukumbu ulio nayo na umri wako. Hakika unastahili pongezi mashallah, mimi kuna mwanafunzi mwenzagu nimeonana nae mwaka jana hata jina lake nimemsahau.

Na shule nimemaliza juzi tu, yule jamaa aliona kama nimemdharau lakini hajui binaadamu tunapitia mambo mengi sana.
Killa....
Amin kwa sote.
 
Asante kwa kumbukumbu nzuri. Umenikumbusha Afro Jazz. Ngojs nimalizie siku kwa kusikiliza super kumba ya manu dibangu na expensive shit ya fela kuti
 
Pamoja sana, mimi nimekulia mitaa hiyo ya magomeni ingawa inaonyesha hao walikuwa wakubwa wetu, nilishi mitaa ya magomeni mikumi mambo yalikuwa mazuri sana by then
 
NAMKUMBUKA RAFIKI YANGU WA UDOGONI GERSHOM CHIHOTA (1950 - 2023)

Kiasi cha kama siku tatu zilizopita nimepokea taarifa kutoka kwa Ally Max Marekani.
Ajabu jinsi kifo kinavyoweza kufungua majalada ndani ya ubongo wa binadamu.

Nataka kuanza na Ally Max.

Ally Max ni mdogo sana kwetu hapa nakusudia kwangu mimi na kwa marehemu Gershom kwani siku Ally alipokuja St. Joseph's kuanza shule mimi nilikuwa nimesimama sehemu tukiita ''School Compound.''

Ally alikuwa kashikwa mkono na dada yake Eyshe (Allah amrehemu).

Nyumba ya Mzee Abbas Max muasisi wa TANU Iringa na nyumba ya kina Chihota zilikuwa zimetenganishwa na uwanja mdogo wa mpira ambao watoto wa hapo mtaani wakicheza.

Ally Max akimjua Gershom toka udogo wake.
Hapa ni Magomeni Mikumi sisi vijana wa wakati ule tukipaita ''Soulville.''

Hii ilikuwa miaka ya mwishoni 1960 umri wetu ulikuwa wastani wa miaka 15.

Soulville ilikuwa kipande tu cha Magomeni Mikumi ambako wazee wetu wengi wao waliokuwa na nyadhifa kubwa serikalini walijenga nyumba zao hapo: Nyerere, Machapati, Muhuto, Mgone, Bakuname, Mwakinyo, Kandoro, Kambona, Chief Fundikira, Ntare, Mzena na Abdul na Ally Sykes kwa kutataja wachache.

Hii Soulville ni nini?

Huu ulikuwa wakati wa muziki wa ''Soul'' muziki uliokuwa unaeleza maisha ya mtu mweusi Amerika.

Wazimu wa muziki huu na sisi ulitusibu Dar es Salaam na tuliweza hata tukaupiga na ulikuwa unatoka Detroit mji ambao Ally Max leo anaishi.

Siku ya Jumatano shule ilikuwa mwisho saa sita mchana.

Hii ndiyo ilikuwa siku mchana wake na Jumamosi na Jumapili tunakutana Mikumi kupiga magitaa.

Gersom alikuwa ''Bassist'' hodari sana akitumia mkono wa kushoto.

Mimi nikimtania nikimwambia anapiga bass mkono wa kushoto kama Paul Mc Cartney wa The Beatles.

Gershom akicheza mpira vizuri sana akitumia mguu wa kushoto lakini mapenzi yake yalikuwa kwenye muziki.

Gershom Chihota tulikutana St. Joseph's mwaka wa 1967 na tukawa marafiki wakubwa sana tuko pamoja muda mwingi.

Kupitia kwake nikawajua kaka zake Raymond na Norman Chihota.

Norman akisoma Azania na alikuwa bingwa wa taifa wa mbio fupi mita 100 kiwango cha kimataifa kwani aliwakilisha Tanzania Michezo ya Commonwealth na kwengine kwingi.

Sifa ya Gershom ilikuwa ni upole kiasi tukampa lakabu tukimwita, ''Cool Kid.''

Kabla ya akina Chihota kuhamia Mikumi walikuwa wakikaa Temeke Wailesi na kupia kwake nikaja kufahamiana na vijana wenzangu wazaliwa wa Temeke Mick Jones (Mikidadi), Choggy Sly (Salum), Allah Brown (Ali Ngota) na nduguze wa kiume wote.

Baba yake Gershom, Mzee Chihota alihama Southern Rhodesia (Zimbabwe) kuja Tanganyika kutafuta maisha.

Ulipofunguliwa Ukumbi wa Arnautoglo Mzee Chihota akawa ndiyo meneja wake.

Mzee Chihota akapata nafasi ya kwenda kusoma Uingereza na huko akafariki na kuzikwa huko huko.

Nyumbani kwa kina Gershom kulikuwa na picha inamuonyesha mama yetu amekaa pembeni ya kaburi la mumewe.

Mama alikwenda Uingereza kulizuru kaburi la mume wake.

Mama yetu huyu alifanyakazi Ikulu hadi Zimbabwe ilipopata uhuru ndipo akarudi Zimbabwe miaka ya 1980.

Si muda mrefu watoto wake wakamfuata.
Mwaka wa 1993 nilikwenda Harare na nilimtafuta Gershom.

Nakumbuka mshangao alioupata baada ya kubisha hodi mlango wake na yeye akatoka akanikuta nimesimama mbele yake namtazama.

Gershom alikuwa wakati ule akifanya kazi Monamotapa Hotel moja ya hoteli kubwa sana Harare.

Wakati niko Harare Manu Dibango alikuwa mjini akifanya maonyesho.

Gershom na mimi tulimzungumza kidogo lakini nadhani rafiki yangu alitambua kuwa miaka imebadilika.

Gershom hakugusia kuniambia twende tukamsikilize Manu Dibango.

Ninachokumbuka tulizungumza kuhusu taarifa kutoka magazetini watu waliokwenda kwenye onyesho lake wakilalamika kuwa hakuwapigia nyimbo yake maarufu ''Soul Makosa,'' lau kama walimuomba afanye hivyo.

View attachment 2661769
Mkuu umenikumbusha zama zilizopita, miaka hiyooo!
Mimi namkumbuka Norman Chihota, ambaye alikuwa mwanariadha mahiri, sijui yuko wapi.
Vile vile walikuwepo wazee toka Malawi, kina mzee Mhango, mzee Gondwe na wengine.
Ahmed Max yuko wapi sasa hivi, class mate wangu.
 
Asante kwa kumbukumbu nzuri. Umenikumbusha Afro Jazz. Ngojs nimalizie siku kwa kusikiliza super kumba ya manu dibangu na expensive shit ya fela kuti
Ilikuwa Afro 70, mwanzoni wakifanya mazoezi kwa mzee wao, mScott akiitwa mzee Gordon, aliyekuwa pale Chang'ombe, mkabala na nyumba za Keko NHC.
Sisi tukikaa Govt Quarters Chang'ombe mtaa wa Basrah.

Bendi iliteka vijana wengi kwa kuishabikia.
Hiyo ni miaka ya mwisho wa 1960s.
 
Mkuu umenikumbusha zama zilizopita, miaka hiyooo!
Mimi namkumbuka Norman Chihota, ambaye alikuwa mwanariadha mahiri, sijui yuko wapi.
Vile vile walikuwepo wazee toka Malawi, kina mzee Mhango, mzee Gondwe na wengine.
Ahmed Max yuko wapi sasa hivi, class mate wangu.
Jidu...
Pole sana.
Ahmed Max kafariki miaka mingi.
 
Back
Top Bottom